UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Naomba nijue hizo environmental impacts zilizozuia mradi huu kukubalika tangu enzi ya mjerumani, aliyeuza binadamau bila kujali social impacts.
 
Sikuwa najua kama chombo kama hiki kinaweza kuhujumu maendeleo ya nchi, sasa nimeamini,

Kumbe wanafurahia umaskini wetu
 
Tembelea Kinyerezi I ,150 MW kama uko Dar.
Kinyerezi II ,250MW iko under construction.
hahahahahaas wajinga wa CCM huwa mnanifurahisha sana hasa kwa.kupenda.kufurahia takwimu za.kwenye makaratasi na maneno ya majukwaani ya.waropokaji wenu huwa nawaona wapumbavu sana.nyie.watu unacho kiongea kuhusu kinyerezi sicho.kilichopo kinyerezi nimetoka huko tar 17 feb kwa kazi maalum hakuna haakuna hicho unavho kisema nyie watu ni wajinga sana aisee
 
Hahaha huwa mnawapiga risasi wanaowaambia ukweli mnasema eti ni vibaraka, muwapige risasi na hao UN sasa, au muwafukuze nchini.
 
Hakika.nakumbuka walivyo tulisha matango pori kuhusu gesi ya mtwara
 
Mtu kama wewe ungekuwa ni mkutano wa kujiandikisha washiriki, nina hakika tusingekuwa chumba kimoja. Maelezo na maoni kama haya yanatakiwa yatolewe na mwanasiasa mwenye lengo la kudanganya wapiga kura. Mtendaji huwezi kutumia lugha ya kusema, mfano kilimo na uvuvi nk. ....

Ni kilimo gani kisichotegemea mvua ambacho hakihitaji umeme? Uvuvi gani wa maana usiotegemea umeme? Suala la umeme wa gesi haizuii kuwa na umeme wa maji. Duniani nani ana gesi kuliko Russia? Je umesikia wakiacha nuklia eti kwa sababu wana gesi? Afrika kusini walitumia nuklia kwa miaka mingi bila umeme wa maji je, kwa nini sasa hivi wamerudi kwenye maji?

Tutoe mawazo ya kiufahamu badala ya lugha ya wanaoomba kura.
 
Un hawataki tuwe na umeme wetu.Ttehe tehe tehe.
Mbona ulaya imetapakaa vinu vya nyukilia na viwanda vinavyotoa moshi unaoharibu mazingira hawasemi kitu
 
Sawa kabisa JPM ajenge Stieglers Gorge watake wasitake, jenga Udart Ubungo to Pugu na posta - mbagala au kongowe kabisa. Baada ya hapo atawale mpaka jina lake litakapoitwa.Mambo mengine yatajirekebisha yenyewe hatujaanza leo. Kwa hiyo Climate change inaathari zaidi kwa TZ kuliko wengine mbona Ethiopia wanajenga Bwawa kubwa Afrika nzima. Gesi waulizeni walioanza atapoteza muda sana ku deal na gesi mbele kwa mbele St.Gorge Ijengwe fasta.
 
Sikuwa najua kama chombo kama hiki kinaweza kuhujumu maendeleo ya nchi, sasa nimeamini,

Kumbe wanafurahia umaskini wetu
Mkuu kuna watu humu na hata wengine serikalini wanawahusudu wazungu na kuamini kila wanachopikiwa.
Huu ni mfano hai kuwa Watanzania tujiamini kwa maendeleo yetu.

Hapa Magufuli anatujengea heshima, na hao wazungu wataanza kuelewa kuwa hatuwezi kufuata vitu wanavyotaka wao visivyo na manufaa kwa nchi.
 
Ulifika sehemu gani Kinyerezi.
Tuanzie hapo.
 
Inawezekana unajua umuhimu wa Stigler's Gorge Power Dam lakini hujui athari za mradi kimazingira na hasa Ecosystem na Climates...na isitoshe UN wameonya kwa faida.yetu si yao.....the vision of a hungry man is always short and temporary...
 
Tabia ya kuanzisha miradi na kuiacha hewani imekuwa ni mila na desturi kwa serikali hii ya CCM.Kilimo kwanza sijui kimepotekea wapi.Hawana kipaumbele kabisa.

Horace Kolimba:CCM haina dira,sera wala mwelekeo.
Kingunge:CCM imeishiwa punzi.

Roho zao zipumzike kwa amani.Amina
 
Kwa Magu wataula wa chuya! Prezdaa Magu songa mbele baba, kurudi nyuma, mwiko!
Kwa mazuri unayofanya tuko nyuma yako, yale mengine hapana!

Ujifunge na mkanda kwenye kulipa kodi maana unekulia mikopo kutoka Uzunguni.
 
ccm oyeeeeee cuf lipumba oyeeeeee
 
YOTE HAYA NI KWA SABABU RAISI WETU HAJAWAHI KUTEMBELEA NCHI ZA KIZUNGU.USHAMBA NI MZIGO ASEE ...YAANI KABLA HALIJAMALIZIKA MOJA LIMESHADANDIWA JINGINE NA MWISHO WA SIKU NI KUSUMBUANA KWENYE MAKODI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…