Unafahamu unachokiongea au wafurahisha genge tu hapa?
Hiyo shule asilimia 98/9 ya wanafunzi wa pale wanaishi nje ya Kurasini. Hawa anzia kwa Aziz Ali ambao bado ni wachache mno wanaoishi hapo, kuendelea mpaka Kisemvule.
Hii shule kimsingi, mazingira ya ile shule ni magumu mno kuanzia kwa walimu wenyewe mpaka wanafunzi. Shule hii unakuta wana mikondo mpaka 7 au 8 na kila darasa unakuta lina wanafunzi 100+ na walimu ni wachache mnooo! Hili la uvutaji bangi kwa wanafunzi na vurugu za hapa na pale ni kiasi kidogo mnoo ila kiuhalisia serikali yatakiwa kujifumua mifumo yake ijidhatiti kwenye elimu.
Kuna mdau kazungumza swala la usafiri, ninamuunga mkono kwa asilimia zote zitakiwazo, wanafunzi wa hii shule na ile ya Uhamiaji majirani zao utawakuta wako mtaani saa 2.30 asubuh au wanakula mihogo kwa wauza mihogo mazingira ya jirani na eneo la shule wakiwa wanategea muda wa break waingie darasani. Mara kadhaa nimekuwa nikizungumza nao hawa watoto kutaka kujua kinachowachelewesha, sababu zao zimekuwa ni moja, TAABU YA USAFIRI UNCLE. Ukiwa unaufahamu mtiti wa usafiri wa Mbagala na viunga vyake kwa asubuhi na jioni utanielewa, na kibaya zaidi wazazi wa wilaya ya Temeke huwa sio rahisi kugombelezea wanafunzi kwa makondakta wafike shule mapema tofauti na wazazi wa huu upande wa Kinondoni na Ilala