Una maoni gani kwa matokeo haya ya kidato cha pili Shule ya Diplomasia inayopatikana Dar?

Kwa matokeo haya una maoni gani?

Shule ipo Jijini Dar es Salam na siyo Nachingwea.

View attachment 2869779
Matokeo ni direction tu, hakuna cha ziada. Kila mtahiniwa hapo anapaswa kutafakari uelekeo wa nini afanye kulingana na Matokeo yake.

Hizo zero ni chache sana ukilinganisha na idadi ya ambao hawafika hata sekondari, na werevu wameshachagua uelekeo sahihi WANAJENGA TAIFA.
 
Shule za serikali ni ajili ya kusogeza umri tuu
 
Daslam kusoma day ni changamoto sana maana naona watoto wanapata tabu sana katika usafiri,

Shuguli za utafutaji zinafanya wazazi wanashindwa kuwajibika vizuri katika kusimamia watoto wao....

Tatu waalimu wapo busy na mishe msihe ili waweze kuendana na hali halisi ya maisha dar es salam

wingi wa viburudisho na sehemu za starehe kuongeza vishawishi kwa wanafunzi

Etc....
Umemaliza kila kitu.
Dar haiko sahihi kwa upande wa Elimu hasa shule za Day.
 
Shule inaitwa Diplomasia?

Labda tatizo limeanzia hapo! Inawezekana waliendekeza sana Diplomasia wakasahau kuwa wakati mwingine "kakiboko" humsaidia mtoto kukaa kwenye njia sahihi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
sasa hili ndio chanzo kikubwa cha mimba haswa kwa jinsia KE.

bodaboda na bajaji ndio wanageuza hao watoto kuwa wake zao,
Tena sio uongo, unakuta boda au bajaj anazurura na mwanafunzi kutwa nzima.

Kuna siku nlikua natoka home naenda sehem, ilikua mchana, sasa niko njian natembea bajaj ikasimama nkapanda,

Nkamkuta mwanafunz wa kike ndan, punde anaanza kulalama "wee fulan unachukua abiria kwan tulikubalianaje?, we c ulisema leo tunashinda wote?" Jamaa akadakia "huyu namjua hana noma ndo maan nimemchukua namdrop had hapo mbelee"

Nilimuangalia yule mwanafunzi kwa jicho bayaa, uvumilivu ulinishinda nlianza kumsema yule mwanafunzi kwa ustaarabu, eti na yeye akajifanya kuanza kupanick n kunichamba, nkasema hunijuii wee nilimchambaa na kumchambua had akabaki anainama chini kwa aibu,

Na hatonisahau, baadae nkamuambia yule jamaa Leo unamchezea akipata mimba unamkana humjui ila unashinda nae kutwa nzima.

Yule jamaa akajibu, "sio mimi yeye ndo anataka, muda wa kuwa shule anataka kuwa na mimi, nifanyeje."
Nilichokaa.
 
Kuhusu changamoto za usafiri sio sababu za MTU kupata four au zero
Umeamua tu kukataa ila hii ni sababu tena changamoto.
Watoto mpka saa3 asubuhi hakuna gari inayotaka kuwabeba anafika shule kachoka muda umeenda.
Anarudi home saa1 usiku anafika anakutana na kazi akimaliza kula kulala.
Kuna namna serikali inabidi kuangalia kutatua suala zima la usafiri hasa watoto wanaotumia daladala kidogo kwenye treni wana afadhali maana wapo na mabehewa special.

Kinachofanyika baada ya mwanafunzi kuona usafiri mgumu ndio hutokea vijana haswa bodaboda au tu kijana atampa pesa ya kupanda usafiri siku zikienda tu mtoto wa kike anajiingiza kwenye mapenzi na mimba zisizotarajiwa.
 
Hiyo shule 70% ya wanafunzi wanaishi maeneo Karibu na shule.
 
Unafahamu unachokiongea au wafurahisha genge tu hapa?

Hiyo shule asilimia 98/9 ya wanafunzi wa pale wanaishi nje ya Kurasini. Hawa anzia kwa Aziz Ali ambao bado ni wachache mno wanaoishi hapo, kuendelea mpaka Kisemvule.

Hii shule kimsingi, mazingira ya ile shule ni magumu mno kuanzia kwa walimu wenyewe mpaka wanafunzi. Shule hii unakuta wana mikondo mpaka 7 au 8 na kila darasa unakuta lina wanafunzi 100+ na walimu ni wachache mnooo! Hili la uvutaji bangi kwa wanafunzi na vurugu za hapa na pale ni kiasi kidogo mnoo ila kiuhalisia serikali yatakiwa kujifumua mifumo yake ijidhatiti kwenye elimu.

Kuna mdau kazungumza swala la usafiri, ninamuunga mkono kwa asilimia zote zitakiwazo, wanafunzi wa hii shule na ile ya Uhamiaji majirani zao utawakuta wako mtaani saa 2.30 asubuh au wanakula mihogo kwa wauza mihogo mazingira ya jirani na eneo la shule wakiwa wanategea muda wa break waingie darasani. Mara kadhaa nimekuwa nikizungumza nao hawa watoto kutaka kujua kinachowachelewesha, sababu zao zimekuwa ni moja, TAABU YA USAFIRI UNCLE. Ukiwa unaufahamu mtiti wa usafiri wa Mbagala na viunga vyake kwa asubuhi na jioni utanielewa, na kibaya zaidi wazazi wa wilaya ya Temeke huwa sio rahisi kugombelezea wanafunzi kwa makondakta wafike shule mapema tofauti na wazazi wa huu upande wa Kinondoni na Ilala
 
Upo sahihi🙌🏽🙌🏽
 
Back
Top Bottom