Unafanyaje kukusanya kodi nyumba iliyo mbali? Nishachoka

Unafanyaje kukusanya kodi nyumba iliyo mbali? Nishachoka

Nyumba nzuri waga ni gesti au fremu, kupangisha watu lazima uwe mvumilivu.
Kuna nyumba moja ni kama nilishamuweka mtu aiangalie. 😁
Mkali yule, ikifika kulipa kodi ananiwahi na excuse. Atalipa hapo kwa muda anaotaka yeye.
Ila uzuri waga analipa, nahisi ni life tuu inamsumbua.
Bora huyo
 
Niliwahi kuwa na mama mwenye nyumba anayeishi mbali na hakumbushii kodi🙆‍♂️🙆‍♂️ inabidi ujiongeze mwenyewe ulipie.

Yaani nikijisahau nae anasahau. Siku namlipa hata hajui ni ya muda gani🤣
Mizi wewe shindii
 
Wanawake wengi wana huruma sana hawawezi kushurutisha mpangaji.
Wife anawaulizaga wapangaji wake "mna uhakika mtapata kodi mapema? Kama hakuna uhakika mniambie mapema..."
Nikimuuliza ndivyo utaratibu wa kudai ulivyo? Anajibu kirahisi tu "una watoto wamepanga na wenyewe huko,ukiwanyanyasa hawa na wenyewe watanyanyasika huko"...
Imebidi tu kila mtu adai wapangaji wake sasa
😀😀😀
 
Kama una wapangaji wengi ni shida lakini mpangaji mmoja ni rahisi. Binafsi huwa namkumbusha mwezi mmoja kabla ya muda wa kodi kwisha lkn wakati mwingine anatuma tu mwenyewe hata bila kumkumbusha
Mmoja juzi mdada nimemuambia Kodi ijayo nataka ya miezi sita, kaninunia! Wapangaji ni mtihani sana!
 
weka system ya ku lock milango kwa kuhesabu siku, na pia luku system inayo ruhusu kuweka wewe tu.
Kwenye Lodge mnafanya nini kudhibiti wafanyakazi wasio waaminifu wanauza vyumba halafu haweki rekodi kwenye daftari?
Milango ya kufungua kwa kadi inaweza kusaidia ?
Upo uwezekano wa kufungua milango kwa Code ambayo inakuwa inasomq na kwa mmiliki pale mteja anapoingia.?
 
Back
Top Bottom