Unaichunguzaje Bandari nzima wakati CEO wake yupo kazini? Hii inakuwa ni zaidi ya siasa

Unaichunguzaje Bandari nzima wakati CEO wake yupo kazini? Hii inakuwa ni zaidi ya siasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimemsikia Waziri Mkuu Mh Majaliwa akiwaagiza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kufanya uchunguzi kwenye bandari zote nchini.

Bandari hizo ni Mwanza, Kyela, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam.

Agizo hili amelitoa kufuatia ripoti ya CAG kubaini ufisadi bandari ya Kigoma.

Ndio nauliza, uchunguzi huo unafanyikaje bila Mkurugenzi mkuu wa Bandari kuwekwa pembeni ili asiuingilie?

Kule Zanzibar Rais Mwinyi alishatoa angalizo penye uchunguzi wa kitaasisi Mkurugenzi Mkuu lazima akae pembeni kuachia mazingira huru ya kuchunguza, huku bara sijajua tunafeli wapi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Aliyemteua ndio mwenye mamlaka na hilo la kumuweka pembeni au kumtumbua.

Yeye hajaona shida yeyote
 
Majaliwa hawezi kumfanya lolote Kakoko, Board yenyewe ya TPA kaiweka mfukoni, hakuna anayefanya fyoko. Kakoko anareport moja kwa moja Chato.

Kakoko ni Core Member wa Syndicate ya TANROADS iliyokusanya hela kutoka miradi ya Ujenzi wa barabara kumwezesha Waziri wa Ujenzi wa wakati ule apate Urais, kwa hiyo Kakoko is Untouchable. Wengine ni Mfugale(DG Tanroads), John Kijazi (KMK) na CAG Kichere, hao wana ubia wa moja kwa moja na Urais wa Awamu hii, wanajua dili zote chafu zilizochezwa wakati ule.

If anything Majaliwa ndo anaweza kupoteza Uwaziri Mkuu wake maana yeye ni Outsider kwenye hilo kundi la TANROADS/Wizara ya Ujenzi ya wakati ule.

Tunza hii kama rejea baadaye
 
Lazima Waziri mkuu awe makini anaweza kumgusa Mkurugenzi mkuu akajikuta yeye ndio anafukuzwa badala ya huyo Mkurugenzi mkuu.
Kwani mkurugenzi wa TAKUKURU hawezi kumgusa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umma yaani SU?
 
Majaliwa hawezi kumfanya lolote Kakoko, Board yenyewe ya TPA kaiweka mfukunoni, hakuna anayefanya fyoko...Kakoko anareport moja kwa moja Chato

Kakoko ni Core Member wa TANROADS Syndicate iliyokusanya hela huku na huku kumwezesha Waziri wa Ujenzi wa wakati ule apate Urais, kwa hiyo Kakoko is Untouchable...wengine ni Mfugale, na CAG Kichere, hao wana ubia wa moja moja kwenye Awamu hii ya Urais.

If anything Majaliwa ndo anaweza kupoteza Uwaziri Mkuu wake maana yeye ni Outsider kwenye hilo kundi la TANROADS

Tunza hii kama rejea baadaye
Umeongea kisiasa zaidi siyo kikatiba!
 
Ndio nauliza, uchunguzi huo unafanyikaje bila Mkurugenzi mkuu wa Bandari kuwekwa pembeni ili asiuingilie?


Kule Zanzibar Rais Mwinyi alishatoa angalizo penye uchunguzi wa kitaasisi Mkurugenzi Mkuu lazima akae pembeni kuachia mazingira huru ya kuchunguza, huku bara sijajua tunafeli wapi.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu Yohane Mbatizaji, johnthebaptist , wewe nawe!, yaani unataka kumtilia mchanga, kitumbua chake?, hajui yeye na naniliu, walikutana wapi?, hawakukutana barabarani!. Hata hivyo Zanzibar ni Zanzibar na Tanzania Bara ni Tanzania Bara!.

Ila hata katika viongozi, wote hawafanani!, kuna Wakurugenzi na 'wakurugenzi', hawalingani!.

Hata katika Utumbuaji,
P
 
Back
Top Bottom