Unaichunguzaje Bandari nzima wakati CEO wake yupo kazini? Hii inakuwa ni zaidi ya siasa

Unaichunguzaje Bandari nzima wakati CEO wake yupo kazini? Hii inakuwa ni zaidi ya siasa

Kama ni Mimi Mhaya Kakoko ningeomba likizo Bila malipo kupisha uchunguzi huru uendelee kwenye Taaisisi.
 
Nimemsikia Waziri Mkuu Mh Majaliwa akiwaagiza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kufanya uchunguzi kwenye bandari zote nchini.

Bandari hizo ni Mwanza, Kyela, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam.

Agizo hili amelitoa kufuatia ripoti ya CAG kubaini ufisadi bandari ya Kigoma.

Ndio nauliza, uchunguzi huo unafanyikaje bila Mkurugenzi mkuu wa Bandari kuwekwa pembeni ili asiuingilie?

Kule Zanzibar Rais Mwinyi alishatoa angalizo penye uchunguzi wa kitaasisi Mkurugenzi Mkuu lazima akae pembeni kuachia mazingira huru ya kuchunguza, huku bara sijajua tunafeli wapi.

Maendeleo hayana vyama!
Kwa kawaida mitazamo yangu kwa Joni thepaptist ni tofauti na fikra zake hilo nalisema wazi, ila mbona naona wakati mwingine kile
kinachosemwaa kama hakitoki kwako?

Ama una agenda gani.
 
Wakati mwingine siyo hadi utenguliwe bali wewe mwenyewe unajiweka pembeni kwa muda!
Bwashee kirahisi rahisi tu ajiweke pembeni? ingekuwa wewe ungejiweka pembeni? ukifikiria una ghorofa lako mbweni halijaisha, una familia inakutegemea, una wazazi wanakutegemea n.k kiafrika issue ya uwajibikaji bado sana na itasubiri miaka trilion zilion
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimemsikia Waziri Mkuu Mh Majaliwa akiwaagiza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kufanya uchunguzi kwenye bandari zote nchini.

Bandari hizo ni Mwanza, Kyela, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam.

Agizo hili amelitoa kufuatia ripoti ya CAG kubaini ufisadi bandari ya Kigoma.

Ndio nauliza, uchunguzi huo unafanyikaje bila Mkurugenzi mkuu wa Bandari kuwekwa pembeni ili asiuingilie?

Kule Zanzibar Rais Mwinyi alishatoa angalizo penye uchunguzi wa kitaasisi Mkurugenzi Mkuu lazima akae pembeni kuachia mazingira huru ya kuchunguza, huku bara sijajua tunafeli wapi.

Maendeleo hayana vyama!
Wewe unashauri nini ili kutupatia muono wako na tupate nafasi nzuri ya kuchangia.
 
Wakati mwingine siyo hadi utenguliwe bali wewe mwenyewe unajiweka pembeni kwa muda!
Exactly, yaani ukimsikiliza CEO unaona kabisa na yeye kuna kitu, hajiamini. Haingii akilini mkurugenzi wa fedha apishe uchunguzi then wewe CEO ubaki kwa uozo huo huo. Dkt Magufuli ana kazi, kwa hawa wateule wasiokuwa na uzalendo.
 
Double standard tatizo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Wakati mwingine siyo hadi utenguliwe bali wewe mwenyewe unajiweka pembeni kwa muda!
Bwashee unaijua njaa lakini au unaisikia?! Afrika Njaa bado ni janga kubwa! Ndiyo maana hilo ulilolisema ni moja kati ya milioni mia moja kutokea Afrika!
 
Umeniohopesha sana.Kumbe hata mkulu ni fisadi!!!!????Looooooooo.

Majaliwa hawezi kumfanya lolote Kakoko, Board yenyewe ya TPA kaiweka mfukoni, hakuna anayefanya fyoko. Kakoko anareport moja kwa moja Chato.

Kakoko ni Core Member wa Syndicate ya TANROADS iliyokusanya hela kutoka miradi ya Ujenzi wa barabara kumwezesha Waziri wa Ujenzi wa wakati ule apate Urais, kwa hiyo Kakoko is Untouchable. Wengine ni Mfugale(DG Tanroads), John Kijazi (KMK) na CAG Kichere, hao wana ubia wa moja kwa moja na Urais wa Awamu hii, wanajua dili zote chafu zilizochezwa wakati ule.

If anything Majaliwa ndo anaweza kupoteza Uwaziri Mkuu wake maana yeye ni Outsider kwenye hilo kundi la TANROADS/Wizara ya Ujenzi ya wakati ule.

Tunza hii kama rejea baadaye
 
Hii haina tofauti na uchunguzi kwa wakufunzi 2 wa Chuo cha Ardhi Morogoro waliofanya ubadhirifu wa bil. 2 za wananchi kwenye mradi wa urasimishaji viwanja Morogoro! Maagizo ya Mabula ni kwamba hao walimu wachunguzwe, then anamwagiza mkuu wa chuo amsimamishe mkuu wa utawala ili achunguzwe!! Hivi hao walimu wangeweza kula hizo hela bila kumshirikisha huyo mkuu wa chuo? Na kwa uelewa wangu hela kama hizo huwa zinaingia kwenye akaunti ya chuo ambayo hao walimu hawana access nayo, anayeweza kuidhinisha ni mkuu wa chuo na mhasibu!! Ila mkuu wa chuo kaachwa!! Tz kuna vituko sana
 
Back
Top Bottom