Unajua kwanini 90% ya wana-hiphop huamini kuwa 2pac ni king wao?

NI kama Bob Marley kwenye Reggae Kuna waimba Reggae wengi lakini Bob alikuwa wa Tofauti ukija kwenye Hip-hop kuna marapa wengi wakali lakini PAC alikuwa na kitu cha kipekee ambacho mpaka leo ameacha Legacy
Hakika wewe unaongea ukweli na uhalisia wa kile tunachojadili hapa.

Wengi hawajui kuwa Pac ndio nembo ya mziki wa Hip Hop kama ilivyo kwa Mohammed Ali masumbwi, Michael Jordan basketball na wengine wengi wa aina hiyo.
 
Huwa nashindwaga kuuelewa u bora wa BIG over 2pac..nimejaribu nimeshindwa
Big alichokuwa anaweza ni kuruka ruka na kutingisha kichwa tu basi, au kidogo kuimba kuhusu maisha yake binafsi hakuna kingine.

Tofauti na Pac ambae aligusia political, ubaguzi wa rangi, aliimba nyimbo ya kuwaasa wazungu na mablack wawe kitu kimoja, wasibaguane maana mbele ya Mungu hakuna rangi iliyokuwa bora isipokuwa ni matendo yako tu ndo yatakuokoa, nyimbo hiyo ni 'CHANGE'.
Ameimba 'Dear mama' ambayo imekuwa kama kioo cha ulimwengu kwa mama zetu wote waliohai na waliokufa mpaka kupelekea kina Christian Bella, Banana Zoro, Mr Nice, GK na wengineo nao kuona umuhimu wa kuimba nyimbo za kuwasifu mama zao (zetu)

Pac aliimba my unborn child ambapo ujumbe wake unatumiwa na wazazi wengi kwa watoto wao kule Marekani maana alitoa usia wa maana sana. Pac aliimba ain't mad cha pia ni ujumbe mzuri sana kwa vijana mabaru baru kutulia na kuweka akili chini ili kujenga maisha yao upya yalioharibiwa na madawa, wizi nk.

Ki ukweli ukona mtu anasema Big ni zaidi ya Pac basi ujue huyo sio mfuatiliaji au mjuaji wa maana ya miziki inayoimbwa na wasanii hao.
 
Tupac alikuwa na beats zake? Beat karibu zote za hip hop huwa wana-sample toka aina nyingine za muziki so obviously hakuna aliyeiba beat za Tupac.

Tupac alikuwa mkali na kinachomtofautisha na rappers wengi ni passion aliyokuwa nayo. Lyrical deliveries zake ziko very emotional na zinagusa. Pia Pac alikuwa multitalented, that doesn't hurt either. Kwangu mimi Pac ni mkali kuliko Biggie. Is he among the greats? Yes. Is he the GOAT? Lyrically no. In my opinion Nas, Jay, Jadakiss, Mos Def and Rakim wako juu kuliko Pac kwa mashairi.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hakwepeshi
Pac hakuwahi kukwepesha. Sikiliza 'Out On Bail' uone au usikie alivyowachana chana polisi, jaji na wanasheria wa serikali tena anawataja live bila kuogopa wala kumung'unya maneno.

Ile ngoma yake ya You wonder why i call you bit..ch alikitolea kimama kimoja cha serikali tena ni kiblack chenzake ambacho kilikuwa kinahamasisha watu na studio za mziki Marekani wasipige nyimbo za 2pac redioni au majumbani.

2pac akamshukia na huo wimbo kibibi kikafunga domo lake, maana alikichana chana vibaya.

Pia kuna ule 'we can't stop' alioimba na kundi lake la outlawz (watoto wa mbwa) akamchana tena yule bibi na makamu wa raisi wa wakati huo, tena kwa kuwataja majina live bila kuogopa system wala mamlaka.
 
Ukiachana na maisha ya u Niga, u hustler na Dis hits jamaa alikua na ma songi ya makali makali sana.

Yan nyimbo ya mapenz ambayo wewe kama mgumu huoni tabu kuisikiliza mbele za watu.
"LITTLE DO YOU KNOW"


Ukweli ni kwamba Marekani nzima bado hajapatikana msanii kama 2pac.
 
Nas namkubali pia mkuu. Kwangu mimi nampa nafasi ya pili after Pac, japo kuna watoto wadogo watakuja kukwambia kuwa Nas anashindwa hata na Eminem, Wayne nk.
 
Ni kweli kabisa kuwa 2PAC ATABAKI KUWA MSANII BORA DUNIANI AKIWA NAMBA MBILI NYUMA YA THE NOTORIOUS B.I.G(biggie small)
 
Uongoooooooo......
 
Tupa qumerr tu..Msikilize notorius B.I.G
Tupa alibamba kwasababu ya lifestyle yake, ila kimziki yani punch to punch, mistari mikali, biti kali, style kali...tupa hamgusi BIG hata kwa mbali
Nikumbushe hv ameuza record ngapi vile huyo notorious BIG na jumla ana nyimbo ngapi...movie je anazo ngp vile nikumbushe tu....Tuzo je? Vp kuhusu ile museum ya Tupac Wake me when I'm free na vp kuhusu ile siku inayoazimishwa ya 2pac
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…