Big alichokuwa anaweza ni kuruka ruka na kutingisha kichwa tu basi, au kidogo kuimba kuhusu maisha yake binafsi hakuna kingine.
Tofauti na Pac ambae aligusia political, ubaguzi wa rangi, aliimba nyimbo ya kuwaasa wazungu na mablack wawe kitu kimoja, wasibaguane maana mbele ya Mungu hakuna rangi iliyokuwa bora isipokuwa ni matendo yako tu ndo yatakuokoa, nyimbo hiyo ni CHANGE. Ameimba dear mama ambayo imekuwa kama kioo cha ulimwengu kwa mama zetu wote waliohai na waliokufa mpaka kupelekea kina Christian Bella, Banana Zoro, Mr Nice, GK na wengineo nao kuona umuhimu wa kuimba nyimbo za kuwasifu mama zao (zetu) Pac aliimba my unborn child ambapo ujumbe wake unatumiwa na wazazi wengi kwa watoto wao kule Marekani maana alitoa usia wa maana sana. Pac aliimba ain't mad cha pia ni ujumbe mzuri sana kwa vijana mabaru baru kutulia na kuweka akili chini ili kujenga maisha yao upya yalioharibiwa na madawa, wizi nk.
Ki ukweli ukona mtu anasema Big ni zaidi ya Pac basi ujue huyo sio mfuatiliaji au mjuaji wa maana ya miziki inayoimbwa na wasanii hao.