Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Personal attack

Huwezi kujadili hoja unamjadili mtu.
 
Hii mijadala ya kumchokono chokonoa Mwenyezi Mungu iishe sasa. Dhana ya Uwepo wa Mungu ipo kiimani zaidi. Mambo ya kusema eti nani alimuumba Mungu ni ujinga na ukosefu wa kuelewa mambo mengine.

Yai na kuku kipi kilitangulia. Tuanzie hapo kwanza. Maana hii hapiop kiimani.
 
Mimi kama sijui chanzo changu ni kipi kunafanya jibu liwe Mungu?
 
Kwanini kuhoji dhana yenye utata kuhusu mungu iwe ujinga,?

Ujinga ni nini?
 
Kwasababu hojayako ilijielekeza kwa Mungu na mwanadamu so siwezi kuuliza kwa kutumia "nini" ila ukitaka naweza kukuuliza pia
Nini kilitengeneza au kiliweka hizo mechanisms?
Mimi sijaleta hoja yoyote mezani, wala sijasema Mungu hayupo....simply mimi nimesema tu hivyo vitu ulivyokuwa unasema kama jinsi jicho linaweza kuona rangi,sijui utumbo kula ugali, mechanisms zake zinajulikana na ni vitu biological kabisa.

Sasa ukauliza tena nani kaiweka hiyo mechanism
Hata kama nikisema Sijui ni nani kaweka hiyo mechanism haitamaanisha ni Mungu ndiyo kaweka...

Wewe unayesema ni Mungu kaweka, unatakiwa uthibitishe. na ukithibitisha beyond doubt, Mimi nitaamini na kumuabudu.

Lakini kama ukishindwa kuthibitisha, Tusiseme ni Mungu bali tuseme ni hizo mechanisms.
 
Unadhani uwepo wa nyota utapingana vipi na madai yangu hapo juu?
Dogo usitafute sifa kupitia MUUMBA wako, kama nilivyokushauri hapo juu uvitazame na utafakari ni namna gani vingeweza kuwepo bila nguvu ya uumbaji na haujatilia maanani.

Kama tu ambavyo huwezi kuyageuza macho yako na kukitazama kisogo chako tambua pia fikra na akili zako zina ukomo, hivyo utakuwa sahihi sana kuamini uwepo wa MUNGU.
 
Kama sijui hizo nyota zilitokea vipi hakufanyi jibu liwe ni mungu...kitendo cha kukimbilia kusema ni mungu ni uvivu wa kufikiri hivyo unaamua kutafuta jibu jepesi " mungu kaumba"
 
Unajikanyaga si umesema Mungu kaandika kitabu? Ebu rudia kusoma Uzi wako.
Nimekuuliza swali hujajibu.

Una uthibitisho gani kuwa hayo maneno kwenye Quran ni ya mungu na si mtu tu aliyeyatunga?
 
Bora umwamini tu, hata kama kweli hayupo haudhuriki, kuliko kutomwamini na ukamkuta kwenye kiti cha hukumu!
 
Hakuna vitisho hapo mkuu...utatishika vipi na kitu cha kufikirika?
Sawa mkuu mimi pia nafatilia comment za watu.

Bahati mbaya mpaka thread ya 4 hii sijaona comment iliyonishawishi kutoka kwa waumini wa dini. Ni jazba, vitisho na kuuliza maswali yasiyokua na uhusiano kimantiki kuhusu dhana ya uwepo wa Mungu. Hii dhana ya uwepo wa Mungu hata mimi pia ilianza kugoma kuingia kichwani tangu nikiwa o-level nilijiuliza maswali mengi sana, kwanini vitabu vya Mungu vina mkanganyiko, kwa maelfu ya miaka Mungu alishindwa kujidhiirsha yeye mwenyewe afrika mpaka akasubiri atambulishwe na wakoloni?, mababu zetu waliokufa kabla ya ujio wa hizi dini je saiv wapo motoni?

Tangu kuletwa kwa hizi dini takribani miaka 500 sasa hivi je sala na maombi vimesaidia kumaliza tatizo gani hapa afrika? Yaani maswali ni mengi sana bahati mbaya sijawahi kupewa majibu ya kuniridhisha kwaiyo naishi kwa kuongozwa na ubinadamu.

Dini naichukulia kama namna fulani tu ya kujumuika na jamii ila sio muongozo wa maisha
 
Unao ufahamu kuhusu ulimwengu wa ROHO yaani usioonekana
 
Kama kuna makosa ya uandishi umeyalinganisha na yepi sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…