Unajua stori ya mtu ambaye alipotea tu ghafla na hajulikani kama yuko hai au amekufa?

Hapo Cromwell Street nimefika kuna jamaa zangu walikuwa wanaishi huo mji.

Nakumbuka vizuri sana matukio hayo
Jamaa alikuwa mkatili sana na mke wake pia

Nafikiri Rose west bado anatumikia kifungo
Yeah nafikiri the whole community ilikua traumatized.
Yeah Mrs. West bado anatumikia kifungo na hatoki mpaka afe.
 
Kimbukumbu zangu za mwisho kumuona baba yangu mzazi ni siku aliponichukua na kuniandikisha standard 1. Baada ya hapo sikumuona tena ni miaka 21 imepita hajulikani halipo.
Daah pole sana 😔 💔
 
Daahhhhhhh 💔
 
Kweli kabisa tukumbuke kuwa na moyo wa shukrani.

Kuna vitu vingi kama upendo na maelewano na familia ambavyo tunavichukulia kwa wepesi na watu vingine wanavikosa na wanaishi kwa maumivu.

Pole yake sana huyo kijana, ndugu huwa wazingua sana kwenye mali.
 
Poleni sana jamani, bibi akashindwa kumzika mwanae 💔
 
Kuna kijana mmoja jirani yetu kipindi alipomaliza darasa la 7 alienda mjini kujitafuta, tangu 2005 hadi 2014 nikakutana nae barabarani Arusha sehemu inaitwa kona Nairobi akiwa mchafu sana, manywele mengi huku meno yameoza hatari na ananuka uchafu.
Cha kushangaza alikua anaongea vizuri tu na alikua na simu... Nikahojiana nae kuhusu maisha yake na namna ndugu zake wanavyomkumbuka nyumbani, akasema yeye ni dereva wa kenta na amejenga mtaa wa mbauda, suala la kwenda nyumbani akaniambia ataenda wiki ijayo. Tukabadilishana namba tukaagana, mimi nikampigia mdogo wake niliyesoma nae nikampa taarifa na namba akafurahi kweli.
Baada ya siku 2 toka nikutane nae akaenda nyumbani wakamfanyia na sherehe kabisa ila tangu alipoondoka tena nyumbani wiki ileile hajawahi kurudi tena na zile namba zake zilipotea hewani mwezi uleule.
Najiuliza alienda wapi sababu nipo Arusha tangu kipindi hicho mbona sikutani nae? Kwanini alipotea hewani baada ya kuondoka nyumbani?
Pia aliponipeleka alipopaki kenta lake alionekana kufahamika na madereva wengine waliokua pale ila niliporudi pale kuulizia walionesha hawamjui mtu wa aina hiyo.

Kwa sasa mdogo wake anafanya kazi ya bodaboda mtaa huo mwaka wa 5 na hajawahi kukutana nae

Binti wa zamani nisamehe jana nilicomment hapa nikiwa nimelewa 😇
 
Inawezekana ni spy so amehamishiwa kazi kituo kingine...kwa sbb hataki ajulikane hasa na watu wa karibu...au kuna matukio ya kutisha ameyafanya hivyo hataki familia yake iwe involved...
 
Babu mzaa baba wa mama yangu alihamia machame akaoa mwanamke akazaa watoto , mwisho wa siku kazi iliyo mleta ipo isha akaondoka zake mpaka leo hajulikani alipo na alitokea nchi gani
Hujui alitokea nchi gani na wewe ujiujaje alikuwa ni Babu mzaa Baba wa Mama yako?

Ubinadamu ni kazi/The humanity and then.
 
nikiwa chimbo, kuna jamaa mgeni aliingia pale chimboni, akaomba connection akapewa,...akapiga kazi kama siku tatu,..akapata mpunga kiasi akaenda chunya mjini akala bata na jioni akarudi pale chimbo,...

Kwenye mastori ya hapa na pale, akatuambia,..yeye ni mwenyeji wa ARUSHA, ameoa na ana watoto wawili, pia mama na wadogo zake wanamtegemea,
mke na watoto wake wamehamia mbeya mjini kama mwezi mmoja umepita wakiwa wametokea machimbo ya kahama, wakafikia mbeya alipoiacha familia yake na yuko kwenye mchakato wa kuihamishia familia yake chunya mjini,...na alipoenda mjini aliwatumia pesa ya matumizi , maana wife bado hana mishe na watoto wanafanyiwa mchakato wa shule,...jamaa alikuwa na simu, aliiuza hukohuko chunya mjini maana alisema pesa haikutosha, so akabakiwa na laini tu,.....siku kama ,mbili mbele jama alienda kwenye migodi fulani kuchimba na washikaji wengine, aisee shimo likatitia jamaa akiwa bado shimoni wenzake wakapona lakini jamaa alifia mulemule na kumtoa ilishindikana kutokana na ulefu wa mgodi ule....

hakuna aliyekuwa anamjua jina lake kamili wala kufahamu inapoishi familia yake.....

huwa kila nikiwaza familia yake sipati picha🥲🥲😔😭
 
Nawaza maumivu yaliyobaki kwa familia mpaka muda huu 😒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…