nikiwa chimbo, kuna jamaa mgeni aliingia pale chimboni, akaomba connection akapewa,...akapiga kazi kama siku tatu,..akapata mpunga kiasi akaenda chunya mjini akala bata na jioni akarudi pale chimbo,...
Kwenye mastori ya hapa na pale, akatuambia,..yeye ni mwenyeji wa ARUSHA, ameoa na ana watoto wawili, pia mama na wadogo zake wanamtegemea,
mke na watoto wake wamehamia mbeya mjini kama mwezi mmoja umepita wakiwa wametokea machimbo ya kahama, wakafikia mbeya alipoiacha familia yake na yuko kwenye mchakato wa kuihamishia familia yake chunya mjini,...na alipoenda mjini aliwatumia pesa ya matumizi , maana wife bado hana mishe na watoto wanafanyiwa mchakato wa shule,...jamaa alikuwa na simu, aliiuza hukohuko chunya mjini maana alisema pesa haikutosha, so akabakiwa na laini tu,.....siku kama ,mbili mbele jama alienda kwenye migodi fulani kuchimba na washikaji wengine, aisee shimo likatitia jamaa akiwa bado shimoni wenzake wakapona lakini jamaa alifia mulemule na kumtoa ilishindikana kutokana na ulefu wa mgodi ule....
hakuna aliyekuwa anamjua jina lake kamili wala kufahamu inapoishi familia yake.....
huwa kila nikiwaza familia yake sipati picha🥲🥲😔😭