Unajua stori ya mtu ambaye alipotea tu ghafla na hajulikani kama yuko hai au amekufa?

Ndio maana geita Iko tofauti kidogo na Kanda zingine kwenye uchimbaji Kama chunya maana Kanda ya ziwa lazima watu wa idara ya ukaguzi(inspectors) wapite kila duara na hata Kama wasipopita msimamizi wa duara lazima aandike orodha ya wanaoingia duarani kila siku na muhuri unapigwa na kwenye majina ya waponchaji Kuna taarifa za sehemu uliyotoka kuanzia Kijiji mpaka mkoa na namba za dharura ikitokea shida.

Sikufika chunya siku nyingi Ina Nina amini masuala ya idara ya ukaguzi yatakuja tu
 
aisee mimi niliacha chimbo sababu ya ushenzi wa maboss, duara linahitaji timba, boss hataki kutoa hela mpaka mawe yatoke yakasagwe,...wakati huo duara bovu,....ukiwashitaki kwenye mamlaka ,...kwanza wakaguzi wenyewe hawajii duarani na boss anakuja chimboni kibabe na shombo juu,....unaweza jikuta una kesi ya mauaji,.... kidogo unafuu ulikuwepo kipindi cha magu watu walikuwa na hofu,....pia duara alillofia mshikaji halikuwa rasmi,...
 
Kwa hali aliyokua nayo ukichanganya na elimu yake ndogo hawezi kuwa spy
Watu wengine ingawa tunawatazama Kwa nje tunawaona wazima ..but wengine Wana changamoto za afya ya akili.... kwahiyo kuna kitu kina wa trigger wakiwa na watu wanaowajua...wanataka kukaa mbali Sana na watu wanao wajua....wagonjwa tu
 
Umenikumbusha kuna mwaka jamaa flani aliletaga story za maisha ya machimbo na lugha za machimbo huo uzi ulinichekesha sana... kuna neno La Kugongomeja aisee 😅😅😅 sitolisahau
 
Duh!
 
Kanda ya ziwa fundi akitoka duarani inabidi akabidhi kazi yake kwa idara ya ukaguzi lasihivyo roller inashushwa chini hakuna kazi kuendelea mpaka waji ridhishe

ufungaji ni muhimu Sana unaweza kuua watu kimasihara kabisa
 
Umenikumbusha kuna mwaka jamaa flani aliletaga story za maisha ya machimbo na lugha za machimbo huo uzi ulinichekesha sana... kuna neno La Kugongomeja aisee [emoji28][emoji28][emoji28] sitolisahau
kujogomeja,kuchumira,kuporora,chabo,fonka,longo,sesa,ng'anda

Yani Kuna maneno uliongea sehemu nyingine hakuna atakaye kuelewa
 
Nina ndugu yangu ila niishie kusema No Reforms No Election
 
kujogomeja,kuchumira,kuporora,chabo,fonka,longo,sesa,ng'anda

Yani Kuna maneno uliongea sehemu nyingine hakuna atakaye kuelewa
Huyo jamaa ndo alikua anatupa tafsiri

Inamana machimbo yote lugha ndo hio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…