Unamiliki iPhone ya macho matatu wakati hata kiwanja huna, wewe ni bure tu

Unamiliki iPhone ya macho matatu wakati hata kiwanja huna, wewe ni bure tu

Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure

Kwa umri ulio nao Ndio kama hivyo,ukizeeka utakua mchawi amini yani
 
Kumiliki viwanja imekua kama fasheni...unamiliki ila hujengi miaka nenda..utasikia mtu anakuja na hoja ni mtaji...
Hata hivyo kiwanja bado ni asset inayopanda thamani kila siku tofaut na kununua hiyo macho matatu ambayo huwez kuja kuuza kwa bei uliyo nunulia
Bado kiwanja ni Bora kuliko macho 3 hata kama haukiendelezi
 
Mtu kua na simu ya gharama si makosa,pengine umaridadi wake ndio unaoficha hali mbaya aliyokua nayo.
Basi ukimuona anasimu janja mtu kama wewe unapagawa
Mkuu usipangawe kwa vitu ambavyo hata Mimi naweza nikakutunuku.
IMG_0364.png

NB:- wengi unao waona wana simu za iPhone wanakua na ndgu zao nchi za nje kwaiyo mtu kuimilik inakua rahis.
 
Naombeni mwenye picha ya IPhone macho matatu aweke hapa please
 
Daaah, umenikumbusha kuna mzungu mmoja aliwahi tembelea Afrika nafikiri West africa. Basi alivyorudi huku siku moja tukawa tunapiga nae stories vitu alivyoviona huko West Africa. Alinambia waafrica sio maskini kama tunavyojitangaza ila ni akili zetu kidogo zina mushkeli, aliongea kama wewe ulivyosema hapo, huko alikutana na watu wanamiliki simu mbili mbili zote za bei mbaya lakini ukienda makwao maisha wanayoishi ni duni sana kitu ambacho wao wazungu hawafanyi. Na hizo simu mbili unakuta watu wanamiliki kwa show off hamna lolote la maana wanafanya nazo.
Huyo mzungu alikupanga mkuu, wao hawatumii tecno wala itel. Wanatumia IPHONE tu.
 
kijana
...Ana milki simu ya bei ya kiwanja kule mkoani
...anamiliki laini zaid4 na zote zna madeni
..Anamiliki nguo za gharama ukiunganisha zote kabatini unapata zaid ya milion1
....anawachanganya madem kama dj wa kisingeli, yan anawacontrol watu 10 bila wao kujijua
....ana marafiki wasap,fb, insta na bado uko normal text na mitaani&mikoani
....Kamaliza chuo
.....alpata mkopo by100%
....hataki kuondoka dar/mjini
.....hatak kazi ngumu
kijana kama huyu unamuwzesha vip? hafai hata kuaminiwa kupewa mkopo wa ujasiliamar maana tayar alivyo navyo ni mtaji tosha hawa ndyo wanaorudsha nyuma maendeleo ya hii nchi, na ndio hawa hawa wamejazana uko insta wakiuza vinguo online na kuuza sura zao wakishindana kujipost picha za location, hawa simu zao hazikos bando japokuwa hawana sources za kupata izo pesa za mabando

watu kama hawa wapo kila sehemu, na humu wapo pia hata comments zao utazitambua jinsi walivyo comment negative na hii thread, hawa hata nyuzi zao pendwa ni zile za hovyo hovyo zle senseless , hawa hawafai kuwepo JF maana wanaidharirisha maana ya great thinkers.
 
Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure
Acha kuwapangia watu vipaumbele vya maisha, tumetofautiana preference vipaumbele na vionjo.. Wewe unawaza kiwanja kama ndiyo top notch ya mafanikio katika maisha, Mwingine hawazi unavyo waza wewe. Mwingine mafanikio katika maisha yake ni kukaa Kidimbwi na kunywa moet chamdor na hennesy za laki na nusu.. mwingine mafanikio yake ni kushika amri kumi za mungu...
Unatumia simu gani wewe..?
 
Mkuu kweli una akili hata kidogo ama unazo sema unazitumia vibaya

Yaani wewe unafikiri matumizi ya simu ni kupiga,kupokea & kutembelea social networks

Unafikiri maisha ni viwanja tena wakati huu wa digital assets
 
Unakuta kijana anamiliki Iphone ya macho 3 wakati hata kiwanja hana mjini hii ni aibu nyingine na janga la hatari sana.

Unakuta wengine ni mtu nzima kabisa anamiliki Iphone ya macho 3 halafu analala kwa shemeji yake na kula mikate na watoto asubuhi wakati wanapata kifungua kinywa ili wapandishwe kwenye school bus.

Mimi nawaangalia watu wa aina hiyo najiuliza wana akili kweli? Unamiliki vipi iphone ya macho matatu au simu ya milioni moja na nusu wakati hata kiwanja huna?

Halafu umekaa ukila bure bure tu vya wazazi unategemea wazazi tu hapa hujui kusaka kwa jasho lako.

Ni aibu na fedheha kumiliki simu ya mamilioni wakati hata kiwanja cha laki 5 kule kisemvule huna unatakiwa ukaombewe au ukapimwe akili maana ni aibu.

Unanunua iphone ya macho 3 wakati hata godoro huna hata kitanda hujawahi nunua unalalia vya watu na vya shemeji zako utakua ni mgonjwa sio bure
huku ni kupangiana maisha...kila mtu na kupao mbele chake!

Sent from my PACM00 using JamiiForums mobile app
 
Leo hujaongea kiajem Leo umegusa kwenye uhalisia wa vijana wengi ku fake life
 
Back
Top Bottom