Mwanao, mwenza wako au yeyote wa karibu nawe amepata dharula au tatizo kama ajali, kuibiwa simu, kuugua nk kisha ameomba simu kwa mtu Ili akufahamishe wakati wewe unadhani kupokea simu ngeni ni tatizo.Ukipiga once na kuona mtu hapokei si utume sms?
Hivi hata matumizi ya sms watu hatuyajui kweli?? Unakuta 10 missed calls, huyo mpigaji anajitambua kweli?
Wakati mwingine jamaa yako amelazwa hospitali au kapigwa dawa za kulevya au amepelekwa kituo cha polisi au shida nyingine.
Huyu amejitokeza kukupigia akiwa ""Msamaria mwema" kisha wewe unabakia na msimamo huo wa kutopokea simu.
Huenda mwisho wa yote hasata itakuwa kwa aliyehoma kupokea simu.
Hata hivyo mwisho wa yote uamuzi wa mhusika [hata kama una utata] uheshimiwe.