Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Mimi hata upige unakufa na no ngen sipokei ng'o
Ndg kijijin kutaka misaada/ maden/ michepuko
Aisee tuma msg kama ni mtu wa muhim nitakupigia hapo hapo kama sio wa muhim NO
 
Mimi mwenywe nawashangaa Sana wenyemsimamo huu Sasa vipi mtu kama kapata dharula ,

Mimi binafsi nikikuta mamba ngeni napokea naongea nae kama kakosea namba namwambia sio Mimi unaye mtafuta,nikikuta missed call napiga kujua nani kanitafuta.
 
Kweli mkuu...Maana kwangu mimi wanachofanya ni Illogical
Mimi pia sipokei namba ngeni. Na hakuna chochote illogical hapo. Kwa sababu simu yangu, muda wangu, uamuzi wangu, na nina sababu nzuri sana ya kufanya hivyo.

Kama kitu muhimu sana mtu atatuma SMS au kuacha voicemail.

Kuna matapeli, kuna ma recruiters wanaopoteza muda, kuna telemarketers wanaotaka kukiuzia maji kisima, kuna ghasia za kila aina unazozijua na usizozijua dunia hii.

Na mimi sitaki ghasia.

Sasa, kutotaka ghasia kunakuwaje illogical?
 
Haijanitokea kwa mtu mmoja au wawili. Ni watu wengi sana. Wengine ni watu wangu wa karibu. Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni.

Mwingine labda ni mtu ambae hamjawahi kuwasiliana na ndiyo kwa mara ya kwanza labda umepata namba yake. Nayeye hana namba yako na una shida ungependa kuongea nae. Unapiga simu hapokei. Baadae atakuja kukwambia namba ngeni hapokei.

Nini siri ya kutopokea namba ngeni? Faida zake ni zipi au hata nyinyi mnafanya bila kujua faida na hasara zake?
Kwanini upige kwa namba ngeni??

Na kama kweli una nia ya kumtafuta mtu no bora ukamtumia ujumbe kumfahamisha wewe ni fulani kama hajapokea simu yako.

Mimi mwenyewe namba ngeni sipokei.
 
Kwa uzoefu wangu,katika kupokea namba ngeni nimekutana na mengi haya;

1. Mtu anaomba Hela.

2. Anasalimia.

3. Amekosea namba.

4. Anakuliza wewe ni nani (wakati kapiga yeye).

5. Ukipokea haongei ila anasikiliza sauti.

Faida ya namba ngeni ni kupigiwa na watu wazito. Mara nyingi watu wa kwenye mfumo hutumia namba ngeni kwenye mambo yasiyo ya ofisi.
3,4&5 kweli kabisa
Mtu anapiga anaanza kuuliza wewe ni nani!
Kupotezeana muda tu.
 
Mimi mwenywe nawashangaa Sana wenyemsimamo huu Sasa vipi mtu kama kapata dharula ,

Mimi binafsi nikikuta mamba ngeni napokea naongea nae kama kakosea namba namwambia sio Mimi unaye mtafuta,nikikuta missed call napiga kujua nani kanitafuta.
Kwamba hujui kitufe cha msg??
Utakuwa huna shida wewe.
 
Wengi hatujui matumiz ya sms,jitambulishe kwanza Kwa sms baada ya kupiga cmu Ili mtu aweze kujua ww n nan,
Unakuta mtu anapiga cmu hachoki tu ,ikikata anapiga Tena ,ikikata anapiga Tena, mwishowe inakuwa usumbufu.
Kutopokea simu kisa namba ngeni ni utoto, kutojiamini, kiburi, jeuri, ushamba na kuwa na chembechembe za uhalifu.
 
Haijanitokea kwa mtu mmoja au wawili. Ni watu wengi sana. Wengine ni watu wangu wa karibu. Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni.

Mwingine labda ni mtu ambae hamjawahi kuwasiliana na ndiyo kwa mara ya kwanza labda umepata namba yake. Nayeye hana namba yako na una shida ungependa kuongea nae. Unapiga simu hapokei. Baadae atakuja kukwambia namba ngeni hapokei.

Nini siri ya kutopokea namba ngeni? Faida zake ni zipi au hata nyinyi mnafanya bila kujua faida na hasara zake?
Anapokwambia hapokei namba ngeni unakuwa umepigia Kwa namba ipi ikiwa awali ulipiga Kwa ngeni hakupokea hayo maelezo alikupa Kwa BARUA au mlikutana USO Kwa USO !!??
 
Mimi mwenywe nawashangaa Sana wenyemsimamo huu Sasa vipi mtu kama kapata dharula ,

Mimi binafsi nikikuta mamba ngeni napokea naongea nae kama kakosea namba namwambia sio Mimi unaye mtafuta,nikikuta missed call napiga kujua nani kanitafuta.
Ushawahi kupigiwa na recruiters/ telemarketers 30 kwa siku?

Hapo ukitumia dakika mbili tu kwa kila simu, na ukishapokea simu unatakiwa kuwasikiliza, unakuwa ushapoteza saa moja.

Who has time for that?
 
Madeni ndyo yanafanya watu waogope kupokea namba ngeni. Mfano wewe ni mfanyabiasha sidhani kama unaweza kuacha kupokea namba ngeni, mfano wewe ni boss eneo fulani sidhani kama unaweza usipokee namba ngeni kwasababu unahudumia watu wengi kwahiyo sio kila anaetaka huduma yako ume save namba yake. Mfano kama una familia huwezi kuacha kupokea cm je kama mtoto au mke/mume amepata ajali huko? Watu wanafuata mkumbo tu wa kutokupokea namba ngeni kwasababu alishamsikia mtu fulani hapokeagi namba ngeni. Ukiona mdada anakuambia hapokei namba ngeni achana nae huyo ni mambo mengi (Malaya). Pia mtu ambae hapokei namba ngeni ni mshamba na limbukeni wa maisha. Full stop!
 
Haijanitokea kwa mtu mmoja au wawili. Ni watu wengi sana. Wengine ni watu wangu wa karibu. Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni.

Mwingine labda ni mtu ambae hamjawahi kuwasiliana na ndiyo kwa mara ya kwanza labda umepata namba yake. Nayeye hana namba yako na una shida ungependa kuongea nae. Unapiga simu hapokei. Baadae atakuja kukwambia namba ngeni hapokei.

Nini siri ya kutopokea namba ngeni? Faida zake ni zipi au hata nyinyi mnafanya bila kujua faida na hasara zake?
Asilimia kubwa ya watu hao ukichunguza utakuja kukuta wanadaiwa na nimadeni ya muda mrefu yanayowapa aibu na kujificha sasa jwa sababu anayemdai anamoigia mara kwa mara na hapokei anaamini anaweza kuwa amebadilisha namba...na anampigia ili amdai...kwa hyo hata hiyo nayo hapokei
 
Back
Top Bottom