Unasemaje kuwa umefunga wakati kila jioni unakula?

Kadri unavyoendelea kuandika unadhihirisha namna hicho mnachoita kufunga kisivyo na manufaa.

Ukifunga vizuri unakuwa mpole, mtulivu na mnyenyekevu. Hapo sasa ibada inakuwa nzuri mbele za Mungu.

Jaribu siku saba ulete mrejesho.
Wewe unataka manufaa gani? Lengo la funga ya muislam unalijua?
Manufaa ya kidini yapo kwa mwenye imani yake.

Kwani wewe unapohubiri huo uponyaji na uzima una manufaa kwangu mimi?

Sisi sitajaribu hizo siku 7 wala 100 days....sababu sihitaji hayo manufaa ya kwako. Nahitaji manufaa ya kidini sio hayo unayotaka wewe.

Tusilazimishane.
 
Mada haikuwa imetaja dini yoyote. Naona waislamu wengi mmekuwa wakali hapa ingawa hata baadhi ya madhehebu ya kikristo yapo kwaresma na hawajalalamikia mada.

Unadhani ni kwanini waislamu ndio wamekuwa wakali?
Hizi mada huwa hamzileti ila mpaka msubiri Ramadhani muwabeze waislam. Mna shida sana mafarisayo.

Hivi mimi nikisema anayeamini utatu amekosea nitakuwa nimetaja dini ya mtu?
 
Hapana shida mkuu, mimi nimejaribu tu kuelimisha namna bora ya kufunga kwa manufaa mapana kiimani na kiafya.
 
Mimi sina tatizo na msimamo wala imani yako. Nimezungumzia namna bora ya kufunga.
Namna BORA kwa tafsiri ya kwako. Na ni kwanini ulazimishe hiyo yako ndio iwe bora?
Namna BORA kwa waislam ndio hiyo wanayoifanya.
 
Hizi mada huwa hamzileti ila mpaka msubiri Ramadhani muwabeze waislam. Mna shida sana mafarisayo.

Hivi mimi nikisema anayeamini utatu amekosea nitakuwa nimetaja dini ya mtu?
Mimi naheshimu dini za watu wote.

Kufunga kupo Imani nyingi lakini utatu mtakatifu upo kwenye madhehebu mengi ya kikristo na hivyo huo mjadala utakuwa maalumu kwa madhehebu hayo.
 
Hapana shida mkuu, mimi nimejaribu tu kuelimisha namna bora ya kufunga kwa manufaa mapana kiimani na kiafya.
Basi badilisha title ya story yako na utoe hayo maelekezo kuliko ulichoandika unaonesha dhahiri kile unacholenga kuwa watu wanakosea.

Hakuna anayekosea sababu ndivyo alivyoambiwa afanye.

Wewe fanya yako.
 
Namna BORA kwa tafsiri ya kwako. Na ni kwanini ulazimishe hiyo yako ndio iwe bora?
Namna BORA kwa waislam ndio hiyo wanayoifanya.
Ni namna bora kwa tafiti za kiafya.

Mimi sipingani na mafundisho ya imani yoyote.
 
Basi badilisha title ya story yako na utoe hayo maelekezo kuliko ulichoandika unaonesha dhahiri kile unacholenga kuwa watu wanakosea.

Hakuna anayekosea sababu ndivyo alivyoambiwa afanye.

Wewe fanya yako.
Title naiona iko sawa ila pengine hisia za kidini zinachangia kuiona bila objectivity.
 
Mimi naheshimu dini za watu wote.

Kufunga kupo Imani nyingi lakini utatu mtakatifu upo kwenye madhehebu mengi ya kikristo na hivyo huo mjadala utakuwa maalumu kwa madhehebu hayo.
Imani nyingi
Madhehebu mengi
Sasa we ni nani mpaka uhoji kifunga kwa watu
 
wanajishindisha njaa, au wanapiga pasi ndefu. Mimi nakumbuka nikiwa shule pesa zilikuwa hazitoshi nikawa natumia njia hiyo ya kula usiku tu ili kumudu masomo na nilifanikiwa kufanya hivyo muda mrefu sana, ilikuwa inaitwa KUPIGA PASI NDEFU, yaani kujishindisha njaa hadi usiku ili kutimiza malengo yangu
 
Mkuu wewe ndio umeleta mambo ya dini hapa.

Kufunga sio jambo la kiibada pekee. Ni suala la kiafya zaidi.
 
Mimi naheshimu dini za watu wote.

Kufunga kupo Imani nyingi lakini utatu mtakatifu upo kwenye madhehebu mengi ya kikristo na hivyo huo mjadala utakuwa maalumu kwa madhehebu hayo.
Kama mtu akitaja utatu atakuwa amewalenga watu fulani. Kwanini umewataja wanaosema wamefunga mchana na wanakula jioni? Hujui kwamba kuna watu wa dini fulani utakuwa umewagusa direct?

Bado narudia. Ficha upumbavu wako.
 
Ndio maana mimi nashangaa mtu akisema ati amefunga wakati kila usiku anakula.
 
Nakazia...
 
Wakristo pia wa madhehebu kadhaa wanafanya hiyo ya kushinda njaa mchana na kula usiku ambayo haiwezi kuitwa ni kufunga. Wanakuwa wamebadili ratiba ya kula.
 
Wakristo pia wa madhehebu kadhaa wanafanya hiyo ya kushinda njaa mchana na kula usiku ambayo haiwezi kuitwa ni kufunga. Wanakuwa wamebadili ratiba ya kula.
Kwanini isiitwe kufunga?
Tukubaliane kutokubaliana. Let us agree to disagree.
Kila mtu ana tafsiri yake ya kufunga.
Na hakuna kubeza wengine.

Hata wewe unayekunywa maji tu unakuwa umebadili ratiba ya kula. Na kwamba umeacha food intake umehamia water intake.
 
Ndio maana mimi nashangaa mtu akisema ati amefunga wakati kila usiku anakula.
Kuacha kula kabisa completely si katika maana ya kufunga kwa Waislam. Usiwapangie jina kuita ibada yao.

Mbona watu wanaenda Isreal na wanasema wameenda hija. Kuna muislam kawakataza wasiite hija kisa haifanani na ya kwao kule Macca?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…