[emoji817][emoji1666]
Kuna manzi alifall kwangu inshort wote wawili tulielewana kipindi hicho bado life langu si kivile lakini pesa ya maisha ya kawaida ipo.
Siku anagraduate wakatoka wanafunzi kadhaa na baadhi ya walimu wao wa chuo lengo wakafurahie sehemu na aliniambia mapema kuhusu hiyo ratiba
Akanipigia simu jioni niende kumchukua pale walipokuwa wameenda nikashtuka kidogo nikamuuliza kwa nini? Akasema wewe njoo kwanza maana kuna lecturer kanifukuza hapa
Nikachukua boda mpaka pale nikakutana naye nikamuuliza akasema kuna lecturer alimtaka kimapenzi alimwomba wakapumzike lodge fulani na jamaa alimuahidi zawadi.
Jamaa alitaka kutumia pesa yake ili ampate. Manzi alipokataa yule lecturer alikasirika akamwambia kama vipi aondoke kwa dharau akamuitia bolt yule manzi akaikataa
Nafika pale manzi kaniambia alifanya vile makusudi ili yule mwalimu ajue kwamba ana mtu wake. Nikiangalia jamaa wamepark ndinga zao na mimi nimekuja na boda! Nilifarijika sana ukizingatia kwa kipindi kile kama ukilinganisha life langu lilikuwa chini ukilinganisha na yule lecturer.
Nakubaliana na wewe si kila mwanamke atakuvilia pichu kwa sababu ya pesa japo ni wachache wenye msimamo huo