Unatabiri nini mwisho wa vita hii Iran vs Israel

Unatabiri nini mwisho wa vita hii Iran vs Israel

Nchi za Kiislamu hazina mshikamano na kibaya zaidi tawala zilizopo madarakani zipo kwa maslahi ya Marekani na crew yake.

Fikiria nchi kama Jordan inazuia na kudungua makombora ya Iran yasipite kuelekea Israel, lakini wakati huohuo Inaruhusu anga lake kutumika na Israel ili kumshambulia Iran.

Yote kwa yote Iran anapambana pamoja na kuwa jesshi la mtu mmoja asiye na msaada kutoka nje bado amekuwa tishio kwa Israel anayeungwa mkono na kusaidiwa kila kitu (fedha, makombora, mifumo ya ulinzi na bado tu anasumbuliwa na Iran.

Je, Iran angepata huo uungwaji mkono kama Israel, unadhani angefanya nini pale mashariki ya kati?
Ukiona husaidiwi hilo ni kosa lako si la jirani kusaidiwa
 
Wanapigana vita KWA njia moja tu ambayo ikikomeshwa tu hana namna zaid ya KUSUBIRI kupigwa popote patakatakiwa kupigwa.
Asubuhi hii mtaa mmoja kiongozi mwingine kalipuliwa kwenye apartment yake.

Hakuna covert operations na subortage yoyote kutoka Iran KWA israel ndani ya Israel.

Hakuna Cyber warfare yoyote.

Israel anahujumu kutokea moyoni mwa nchi ya Iran. Asubuhi Lowbed kama nne zikiwa zimebeba Ballistic missiles kuelekea launching site zimepigwa drone humohumo na kulipuka zikiwa njiani. Kimsingi nchi ya Iran Iko uchi mbele ya Israel.

Walisema Nuclear site inayotegemewa Iko chini dagger haziwezi kuichimbua. Ndge zaidi ya irishirini zimerusha makombora bunkerboosters KWA mfuatano kama mtu anayechimba shimbo aggregate ni kuichimbua na kuharibu kabisa hiyo Underground site. Leo Rais wao anasema hata kama wakiibomoa tutajenga tena wakati kabla alidai haziwezi kulipuliwa maana Iko chini sana.

Hadi Sasa lengo la Israel limetimia. Anaweza kupitia washirika wake kuitisha marithiano vita ikaisha ila yeye amefuta viongozi wote wa kijeshi, kairudisha nyuma mikakati ya kinyuklia zaidi ya miaka 40 na wakianza ataanza kuwafuatilia kimyakimya.
Yaani Iran hana mkakati wa kivita dhidi ya Israeli hilo tuwe wazi
 
Ukiona husaidiwi hilo ni kosa lako si la jirani kusaidiwa
Pia hajaomba msaada popote, Israel anaomba msaada KWA rafiki zake na wanaopendana. Yeye rafiki zake wanaogopa kumsaidia KWA wazi.

Israel ni sawa na mtu MWENYE marafiki wa kushibana. Iran amezungukwa na marafiki wanafiki wenye maslahi binafsi na ya kishabiki. Russia, China, Pakistan na NK
 
Yaani Iran hana mkakati wa kivita dhidi ya Israeli hilo tuwe wazi
Pia Yuko too slow, wakati mwenzake ni advanced yaani akipiga ngumi mia yeye ndio anajikongoja na kamoja tena kanaonekania mbali kabisa
 
Iran siyo waarabu ni wa Persia ambao walivamiwa na wajinga wa kiarabu kuwafanya waongozwe kiislamu wakati hawataki

Ndo maana hata leo Iran walikuwa wanawashangilia Israel wakisema piga huyo khamenei

Na target za israel ilikuwa kwenye maeneo muhimu

Britanicca

Hapa mbele umeweka chai wairan walikusanyika kwnye uwanja kulaani shambulio la israel na pia kumtaka kiongozi wao awapige na wao.. Ndio maana walikuwa wanashangia walipokuwa wanapata taarifa kuwa tel aviv inapigwa.. Video ipo CNN, IRNA, REUTERS..
Usipotoshe.
 
Ukiona husaidiwi hilo ni kosa lako si la jirani kusaidiwa

Tawala nyingi zinazomzunguka Israeli zote, nyingi ni vibaraka wa marekani na wanafanya kile Marekani anachokitaka.

Hata hiyo Iran ilikuwa na kibaraka wao Shah akafurushwa na hapo ndipo chuki kuu ya Marekani ilipoanzia kwa utawala mpya wa Iran uliopo madarakani hadi sasa.
 
Iran,wawe ni waarabu au ni binadamu tu,yote kheri ila swali la msingi kwenye uzi lijibiwe.
Shida vyombo vya habari vya kimagharib vinapotosha watu.. Hiyo vita mpaka sasa bado 50 kwa 50 .. Kila mtu amepgwa miundombinu yake.. Ila kwa kupoteza watu iran kapoteza watu 78 waliofariki na idadi inaweza ongezeka, huku israel mpaka sasa wamepoteza watu wawili kwa maana wamefariki na majeruh 41.

Hizi habari usizifuatilie BBC , nenda fars, mehre, CNN kidogo, IRNA na Al jazeera kidogo hawapiki sana takwimu.
 
Moja ya kiumbe mwepesi kumuangusha katika vita ni mwarabu. Kwa sababu ni Rais kumnunua na kumtumia KUWA Adui wa NDUGU zake. Hii ndio maana maagents wa mossad walikuwa kwenye kazi maalumu KWA miaka mingi kufanikisha HIKI kinachofanyika ndani ya Iran.

Iran itapigwa kirahisi sana kisha itafuatia anguko la Serikali hii ya hayatollah, watakuja wadau wengine ambao watakuwa na msimamo wa kawaida kama wale kabla ya wakina hayatollah hawajachukua nchi.


Nini unadhani itakuwa hatma ya vita hii.
Mataifa mengine yataingilia kati kusimamisha vita maana madhara ya kibiashara na kiuchumi duniani ni makubwa sana ,kuanzia mafuta, usafiri wa anga na baharini, na stocks ambazo hadi leo zimeshuka kwenye kiwango hakijawahi kutokea hasa kwa israelv
 
Hapa mbele umeweka chai wairan walikusanyika kwnye uwanja kulaani shambulio la israel na pia kumtaka kiongozi wao awapige na wao.. Ndio maana walikuwa wanashangia walipokuwa wanapata taarifa kuwa tel aviv inapigwa.. Video ipo CNN, IRNA, REUTERS..
Usipotoshe.
Haobwanaoshangilia kupigwa Iran nao wapo. Kwanza Hao wakina Ayatollah wakiingia madarakani na kuifanya nchi iendeshwe kiislam na kutangaza audio na Israel ila kabla ya hapo Iran alikuwa rafiki mkubwa wa Israel. Hata project nyingi za majengo ikiwemo Airport nadhani zilijengwa na wayahudi. Sio wairan wote wanaunga mkono Serikali iliyopo ndio maana Mossad wapo Kila Kona Iran na wanajifanyia wanalotaka.

Rais Mstaafu Ahmanejad aliunda kikosi cha kuwatafuta mossad agents nchini Iran cha ajabu alikuja kugundua mwishoni kamati yote akiwemo kiongozi wa misheni hiyo alikuwa walikuwa ni mamossad zaidi ya 20. Hii amesema hivi karibuni akiwa mstaafu wakati anahojiwa.

Ndio ujue kuiangisha au kuifarakanisha Iran ni jambo jepesi sana KWA West hata KWA kutumia propaganda tu kuivuruga nchi hiyo Israel hawashindwi
 
Moja ya kiumbe mwepesi kumuangusha katika vita ni mwarabu. Kwa sababu ni Rais kumnunua na kumtumia KUWA Adui wa NDUGU zake. Hii ndio maana maagents wa mossad walikuwa kwenye kazi maalumu KWA miaka mingi kufanikisha HIKI kinachofanyika ndani ya Iran.

Iran itapigwa kirahisi sana kisha itafuatia anguko la Serikali hii ya hayatollah, watakuja wadau wengine ambao watakuwa na msimamo wa kawaida kama wale kabla ya wakina hayatollah hawajachukua nchi.


Nini unadhani itakuwa hatma ya vita hii.
IRAN sio waarabu wale ndgu, au we yyte mweupe aliemuislamu na akatoka middle east kwako ni mwarabu et[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Kafanye homework zako tena
 
Back
Top Bottom