Unatabiri nini mwisho wa vita hii Iran vs Israel

Unatabiri nini mwisho wa vita hii Iran vs Israel

Nchi za Kiislamu hazina mshikamano na kibaya zaidi tawala zilizopo madarakani zipo kwa maslahi ya Marekani na crew yake.

Fikiria nchi kama Jordan inazuia na kudungua makombora ya Iran yasipite kuelekea Israel, lakini wakati huohuo Inaruhusu anga lake kutumika na Israel ili kumshambulia Iran.

Yote kwa yote Iran anapambana pamoja na kuwa jesshi la mtu mmoja asiye na msaada kutoka nje bado amekuwa tishio kwa Israel anayeungwa mkono na kusaidiwa kila kitu (fedha, makombora, mifumo ya ulinzi na bado tu anasumbuliwa na Iran.

Je, Iran angepata huo uungwaji mkono kama Israel, unadhani angefanya nini pale mashariki ya kati?
Sasa nani amuunge mkono Iran mwenye agenda ya kipuuzi
 
Hatma ya vita hii ni VITA KUU YA TATU YA DUNIA(Mark my word).

Ndio maana samia anaringa tu, inawezekana akadumu jumba jeupe kwa muda mrefu sana(endapo atashinda uchaguzi), na wala si kwa mabavu, katiba tu inaeza kumzuia asitoke madarakani mpaka vita viishe.
 
Iran, Iraq, Syria, Jordan and Lebanoni kwa asili sio Waarabu; wameingizwa kwenye Arab league tu kwasababu ya DINI ya Uislam but these guys walikuwepo duniani kama Mwarabu hajaingia duniani. Mwarabu ni product ya mu Iraq na Mmisri, Misri ya weusi.
Mafafanuzi tafathali bwashee kwamba mwarabu ni mchanganyiko wa mbantu wa misri na Muiraq?
 
Siku Iran ikija kulusha kombora zake pale USA ndiyo Nita sema iran wamekuwa Sasa

Lakini kujiandaa kupigana na Israel ni upotezaji wa nguvu kazi ya wa Irani

Israel inatakiwa waachiwe vijana Kisha yeye adeal na USA
 
Pia hajaomba msaada popote, Israel anaomba msaada KWA rafiki zake na wanaopendana. Yeye rafiki zake wanaogopa kumsaidia KWA wazi.

Israel ni sawa na mtu MWENYE marafiki wa kushibana. Iran amezungukwa na marafiki wanafiki wenye maslahi binafsi na ya kishabiki. Russia, China, Pakistan na NK
Mkuu urafiki na ushirikiano wa kinchi UNATENGENEZWA hauji tu kwa bahati mbaya

Israel kupitia washirika wake ndio wame injinia mpango mzima
Kuanzia kuhakikisha pale mashariki ya kati anawagombanisha wao kwa wao na kuforce urafiki wa kimkakati kumzunguka adui yao mkuu Iran

Katika hao ulio wataja India kawezeshwa awe anamuweka Pakstan roho juu juu
Russia saa hii kapewa Ukraine anahangaika naye
China uzuri wake sio mtu wa vita vita sana, vita yake anapambanishwa kibiashara

Mkuu wenzetu wanakaa chini na kuchora plan nzima jinsi ya kuthibiti maeneo duniani kimkakati
Si maanishi kwamba wanafanikiwa kila mara kwa 100% lakini wanajitahidi sana
 
Mafafanuzi tafathali bwashee kwamba mwarabu ni mchanganyiko wa mbantu wa misri na Muiraq?
Wanaposemaga Uislam, Ukristo na Judaism kwamba ni Abrahamic religions ni hivi, babu wa Mu Israel, Lebanoni na Mwarabu ni mmoja, anaitwa Ibrahim, Ibrahim ni raia wa Iraq, yeye na mkewe, waliishi kwenye ndoa miaka mingi sana bila kujaaliwa kupata mtoto; baada ya uvumilivu kwisha, Ibrahim akapita na beki 3 wake. Huyu beki 3 alikua mtoto wa Kimisri; remember Misri ilikua ni ardhi ya weusi from the history. Walibahatika kupata mtoto, huyu ndio baba wa Waarabu wote unao wajua wewe, yaani Saudia, Kuwait, Abudhabi (Oman, UAE/Dubai ) kule kwa Houthis nk and baada ya kama miaka 12 tokea dogo azaliwe, Ibrahim na mkewe nao wakapata mtoto mwingine, huyu sasa ndio alikuja kutengeneza kizazi cha Kiisrael na Lebanoni. Tuishie hapa kwa leo
 
Shida vyombo vya habari vya kimagharib vinapotosha watu.. Hiyo vita mpaka sasa bado 50 kwa 50 .. Kila mtu amepgwa miundombinu yake.. Ila kwa kupoteza watu iran kapoteza watu 78 waliofariki na idadi inaweza ongezeka, huku israel mpaka sasa wamepoteza watu wawili kwa maana wamefariki na majeruh 41.

Hizi habari usizifuatilie BBC , nenda fars, mehre, CNN kidogo, IRNA na Al jazeera kidogo hawapiki sana takwimu.
Israel huwa haisemagi ukweli juu ya vifo mkuu.
Ila naamini Israel wamekufa wengi sana kuliko Iran.
Na CBS news inasema majeruhi Israel wamepita 80 asubuhi ya leo.
 
Back
Top Bottom