Unaye mtu wa kukusikiliza? Kuna muda unapitia hali unapitia unatamani kumweleza mtu mmoja upate ahueni lakini hayupo

Unaye mtu wa kukusikiliza? Kuna muda unapitia hali unapitia unatamani kumweleza mtu mmoja upate ahueni lakini hayupo

Kwanza jifundishe kujipenda mwenyewe, huu upendo wa kutaka upendwe na wengine mara nyingi ndio utakuumiza zaidi..!!
Ukiwa na magumu sana omba Mungu na sali ili kukuondolea ule uchungu uliokuwa nao au yale yanayokusibu..!! Hii tabia ya kumwambia mtu vitu vyako kuna wengine hawana vifua utayakuta nje na itakuumiza zaidi.

Bora mara mia zaidi yakikushinda uyalete JF huku utakuta wa kukushauri vizuri, bila kusahau ndugu zangu wa backbenchers hao wanajibu kile kinachowajia muda huo. Lkn hautokosa cha kukufariji na kukuponya majeraha.
 
Kwakweli nashukuru marafiki wananisnich sana kwakweli,mashost hapana
Ila ninao wa kunisikiliza
 
Simama kwenye hoja ya kukosa wa kukusikiliza.

Mana kuhusu familia wengine tumezaliwa full house na hakuna wakukusikiliza mpaka unajuta
 
Mi ni kama wewe, yakinizidi Huwa natafuta chemba, peke yangu naongea na Mungu asiyeonekana Tena kwa kujiamini as if tuko wawili, note siyo kwamba nasali, ila nazungumza a way you can to a friend,
Huongei na Mungu ila unaongea peke yako kwa kuunda dhana ya kufikirika kichwani mwako unayoitumia kujiuliza na kujijibu..

Huna tofauti na mlevi anaye amini anaongea na watu kumbe anazungumza mwenyewe bila kujitambua..
 
Kuna vipindi unapitia kama binaadamu lakin unataman kumueleza mtu m,moja atakae kusikiliza lakini hayupo.

Basi napiga magoti na kumueleza Mungu
Hata huyo Mungu unayedai una mueleza matatizo yako hayupo..

Unajifariji tu kwa kuunda dhana ya kufikirika kichwani mwako unayoitumia kujiuliza, kujijibu na kujifariji mwenyewe.

Ni sawa na mlevi anayekunywa pombe kisha akishalewa ana amini na kujifariji matatizo yake yamekwisha.

Ila pombe zikiisha matatizo yanaendelea kumwandama katika maisha yake ya kila siku.
 
Sawa
 
Kwanza jifundishe kujipenda mwenyewe, huu upendo wa kutaka upendwe na wengine mara nyingi ndio utakuumiza zaidi..!!
Ukiwa na magumu sana omba Mungu na sali ili kukuondolea ule uchungu uliokuwa nao au yale yanayokusibu..!! Hii tabia ya kumwambia mtu vitu vyako kuna wengine hawana vifua utayakuta nje na itakuumiza zaidi.

Bora mara mia zaidi yakikushinda uyalete JF huku utakuta wa kukushauri vizuri, bila kusahau ndugu zangu wa backbenchers hao wanajibu kile kinachowajia muda huo. Lkn hautokosa cha kukufariji na kukuponya majeraha.
Sawa mamii
 
Huongei na Mungu ila unaongea peke yako kwa kuunda dhana ya kufikirika kichwani mwako unayoitumia kujiuliza na kujijibu..

Huna tofauti na mlevi anaye amini anaongea na watu kumbe anazungumza mwenyewe bila kujitambua..
Hata hivo kuamini ni kulewa,Mimi ni mlevi kwa kuamini kuhusu Mungu, na niseme tu nimemshuhudia huko, huwezi nielewa coz haupo ktk viwango vyangu vya ulevi,otherwise unywe ninachokunywa tulewe wote hapo tutaelewana
 
Mimi Sina mtu wa kumweleza,Sina mtu wa kunisikiliza,

Kuna wakati unapitia hali flani una wish angekuwepo mtu M,Moja na akusikilize tu...
Kua na familia unayoitamani ni jambo zuri sana na Mungu akusaidie ulitimize achana na usingle mother, lakini kwa wakati huu lisikupe shida sana kuna watu ni ndugu wa baba na mama mmoja na wamekua nyumba moja lakini hawaongei wala kusikilizana.

USHAURI
Kuongea sio lazima awe ndugu yako, unaweza ukatafuta rafiki mzuri mwenye imani sawa na yako na mwenye misingi mizuri. (tatizo liko hapa kwenye kuwapata 😂 )

Kama ni mtu wa imani tia bidii katika kusali, unaweza pia ukaongea mwenyewe mbele ya kioo chako 😎
 
Kwanza jifundishe kujipenda mwenyewe, huu upendo wa kutaka upendwe na wengine mara nyingi ndio utakuumiza zaidi..!!
Ukiwa na magumu sana omba Mungu na sali ili kukuondolea ule uchungu uliokuwa nao au yale yanayokusibu...
Hapo Tanga kunani hamjambo?
 
Mimi Sina mtu wa kumweleza,Sina mtu wa kunisikiliza,

Kuna wakati unapitia hali flani una wish angekuwepo mtu M,Moja na akusikilize tu...
Historical background ends at 30! Baada ya hapo wewe ni background! Acha kulaumu wazazi! Cha kukushauri! Mtu wa kumpelekea shida zako ni Mungu! Kuna wakati huwezi pata msaada kwa Mwanadamu hata kama ni mama yako
 
ukiona huna wazazi,tengeneza watu wa pemben kua marafiki ila sio ndugu🙌🏾🙌🏾(namshukuru Mungu wazazi ninao),nje na apo sina wa kufunguka matatzo yangu.
 
Nimepitia hali hiyo,naelewa kitu gani unapitia hasa kwa wew binti,ila amini kuwa kesho haitakuwa sawa na leo:JOSHUA 1;9
 
Usiilaumu familia katika maisha yako kwa kuwa ni jamii uliyojikuta ndani yake tayari, huna jinsi.

Je wewe maisha yako umeyajenga vipi? Kwanini umeshindwa kutengeneza watu/mtu wa kumuamini ambaye utaweza kuongea nao/naye chochote ukapata amani?

Binafsi katika familia yetu siwezi kuwa huru kuongea kila kitu, ila Mungu amenijalia mwenza anayenisikiliza kwa vyote na kuniongoza vyema.
Najivunia sana hilo

Umeshasema wewe Mungu amekujalia. Sio wote waliojaliwa au watakaojaliwa kupata upendo
 
Back
Top Bottom