N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Kwa kweli, ukiangalia mifumo ya kilimo katika nchi zilizoendelea, utaona jambo moja kilimo cha kisasa si mchezo wa kila mtu.Kweli kabisa mtu akimiliki hekari 10 akaweka miundombinu ya kisasa akalima mwaka mzima ameaga njaa huyo.
Nenda India, Israel, Marekani, Netherlands, Ukraine au hata Russia sehemu kubwa ya uzalishaji wa kibiashara inaendeshwa na wakulima na kampuni zenye mtaji, teknolojia, mashine, data, irrigation, improved seeds, automation na masoko ya uhakika.
Hawa ndio wanaozalisha kwa kiwango kikubwa, kulisha mamilioni ya watu na pia kupeleka mazao kwenye masoko ya nje.
Kwa hiyo, kilimo cha kesho hakihitaji tu ardhi kubwa kinahitaji capital + technology + knowledge + scale + market.
Kilimo si cha kila mtu kwa maana ya kufanya kwa mazoea.
Ni cha wale wanaoweza ku-adopt new technologies, kuongeza tija kwa kila acre na kuendesha shamba kama biashara.
Future ya kilimo kwa Afrika ni agribusiness si kulima tu kienyeji!