Ungepata nafasi ya kurudi chuo ungesoma nini na kwanini? Unawashauri nini vijana wanaoingia chuo mwaka huu?

Kweli kabisa mtu akimiliki hekari 10 akaweka miundombinu ya kisasa akalima mwaka mzima ameaga njaa huyo.
Kwa kweli, ukiangalia mifumo ya kilimo katika nchi zilizoendelea, utaona jambo moja kilimo cha kisasa si mchezo wa kila mtu.

Nenda India, Israel, Marekani, Netherlands, Ukraine au hata Russia sehemu kubwa ya uzalishaji wa kibiashara inaendeshwa na wakulima na kampuni zenye mtaji, teknolojia, mashine, data, irrigation, improved seeds, automation na masoko ya uhakika.

Hawa ndio wanaozalisha kwa kiwango kikubwa, kulisha mamilioni ya watu na pia kupeleka mazao kwenye masoko ya nje.

Kwa hiyo, kilimo cha kesho hakihitaji tu ardhi kubwa kinahitaji capital + technology + knowledge + scale + market.

Kilimo si cha kila mtu kwa maana ya kufanya kwa mazoea.

Ni cha wale wanaoweza ku-adopt new technologies, kuongeza tija kwa kila acre na kuendesha shamba kama biashara.

Future ya kilimo kwa Afrika ni agribusiness si kulima tu kienyeji!
 
Ningesoma kwani CCM sii Wazalendo na hawana utu😭
 
Umeongea vitu vizuri kwahiyo bado kilimo /agribussiness sio course ya kujiajiri tena kwasababu ulichoongea hapo capital ni kubwa sana. Kwa graduate sio rahisi
 
Bado ningesoma hii Bachelor yangu ya Agronomy..maana imenifungulia fursa nyingi sana,nafurahia kupitia taaluma yangu #we feed the world#
 
elemi unaweza kuipata hata kama hujaingia darasani inalielewa hilo?

tena nyie wasomi uchwara ambao sio mainjinia nina vijana wangu wamejifunza elimu ya mtaani wamewaacha mbali sana kimaendeleo na nyanja zote kiujumla.

mumebaki na ujuaji usio na faida
 
kwamwezi nakula zaidi ya 7.5 milioni
Unaona sasa, ndio maana hata sikutaka kujua unalipwa kiasi gani. Sasa hiyo pesa ndio unapigia watu kelele hapa?

Siwezi kusema nalipwa kiasi gani lakini kwa vile una makelele sana, nalipwa zaidi ya hiyo pesa kwa mwezi.

Ila kwa sababu bado nimeajiriwa, hata kwa upande wangu namheshimu sana mtu aliyejiajiri au anaefanya mambo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…