Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Hapana mkuu...kumuua mtu bila uthibitisho sio fair...Pia kumbuka kuna watoto wadogo wasiojitambua wanatumiwa.
Hata kukiwa na uthibisho hakuna Sheria inayosema akibainika apigwe risasi hapohapo, tunafika huku kwa sababu ya malezi mabovu, haya matukio hapa dar hayajaanza Leo na zipo familia zinabariki matukio haya kwa kula na watoto wao, zipo familia hata baada kuambiwa mwanao anajishughulisha na haya mambo hata hawaangaiki, Kuna vikundi mtaani mpaka vimejipa utawala na vinaogopeka mtaani na ni vitoto vidogo tu . Watoto shule hawafiki kutwa wanashinda machimbo, kwenye vijiwe na mzazi hajishughulishi kumfatilia mtoto sasa nani unategemea akusaidie kulea
 
Kwanza mwandishi ulivyoandika kwa hisia na kujihamii inaanza kututia shaka....
1. UNATOA MALALAMIKO YA JUMLA
2. UNAJIHAMI KUWA WEWE SIYO MHALIFU NA HUNA NDUGU MHALIFU [NDUGU ZAKO WOOOOTE]
3. MALALAMIKO YAKO NI YA JUMLA NA HUJATOA HATA MFANO WA TUKIO AU MTU ALIYEUAWA BILA HATIA NA MAZINGIRA YA KUUAWA KWAKE....

KWANZA NAOMBA KUSEMA WAZI KUWA SIUNGI MKONO MAUAJI YA HOLELA YASIYOFUATA SHERIA...

LAKINI NINA HAYA YA KUSEMA KUHUSU BANDIKO LAKO HILI:-
1. Kutokana na uandishi wako ni either unataka huruma juu ya kile kinachoendelea na unahitaji kisimame mara moja ili upate nafuu.. Je wewe ni mnufaika kwa namna moja au nyingine juu ya hiki kilichokuwa kinafanywa na panya road?

2. Ni kipi kinawapa vijana jeuri ya kuendelea makundi hasa maeneo hatarishi na nyakati hatarishi kama hawa majukumu ya kufanya kwa nini wasikae majumbani ili kutoa nafasi kwa walinda USALAMA kufanya kazi zao?

3. Operation nyingi za polisi kwenye zoezi hili wanapata info kutoka kwa raia wanaochoshwa na vitendo vya hawa panya road ambao mara nyingi ndugu na jamaa huwakingia kifua wanapofanya uhalifu na kuumiza wengine...



USHAURI TUSHIKIANE NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUKOMESHA VITENDO HIVI...

KWA RAIA WALIOATHIRIKA NA VITENDO VYA PANYA ROAD WANAOA KUNA TIJA MAANA PANYA ROAD WAMEPOTEA MITAANI NA AMANI INAREJEA!!!!!
 
Unyama unyama wametaka wenyewe,ujawahi kuvamiwa na wezi??nakumbuka 2011 nilipo maliza form 4 nikazama mtaani huku nikisubiri matokeo ya advance,nikaanza kujishikisha kwenye vikazi vya saidia fundi nilikusanya pesa yangu safi tu,wezi walinivamia wakachukua pesa zangu zote,nguo zangu zote na. Kuku wangu niliyofuga walikuwa wanakata vichwa na kuwaweka kwenye viroba takribani kuku 50 waliondoka nao alafu ni majogoo wakubwa,niliwahesabu walikuwa wezi zaidi ya 15,wakanipiga sana sitaka nisahau siku ile,basi sasa nimekuwa sina huruma tena nikishajua wewe mwizi nanikajiridhisha kukupiga na vitofali siwazii
 
Unaambiwa mtume muhammed alikua hawachekei kima wa namna iyo ya panya road ilishawahi tokea kisa kuna wahuni waliingia madina wakajifanya wema na walikua wanaumwa ugonjwa flani dawa yake ilikua ni maziwa ya ngamia wale wahuni wakatibiwa vizuri kuna siku wameenda machungoni na mwenyeji wao wakamamuua wakaiba ngamia taarifa zilipomfikia mtume akatuma msako wahuni wakadakwa
Alichawafanya sasa

Walikatwa mguu mmoja mmoja kila muhuni akabaki na single leg wakatobolewa macho alafu wakaachwa juani wafe mdogo mdogo[emoji16] usichukulie poa jua la jangwani.. alafu akawaambia hii ndo hukumu ya jambazi

Kwaiyo mtoa mada acha huruma huruma maamuzi magumu yakiume yanatolewa muda mwingine kulinda watu wenye roho nyepesi kama zenu ndo maana leo huwezi sikia vigenge vya kiarifu kweny nchi kama saudi arabia waliweza kukomesha vitabia vya kishenzi kama vya panya road ukiona mtu kakamatwa na polisi ujue kuna tatizo pahala kaa kwakutulia dawa iingie
 
Unatambua polisi mmoja anahitaji kuhudumia raia wangapi? Kodi unayolipa ili kila raia aweze kulindwa na polisi ni kiasi gani? Nabaki na msimamo wangu hawa ni wa kupunguza tu hizo sheria zinachelewesha maamuzi, hizo sheria ndo zimewaachia hao wanaorudi kuja kuua, hizo sheria ndo zimeachia kwa dhamana hao wanaorudi kuja kuua. Kwangu the only remain solution is by ELIMNINATION. Na tamani kuona hata OPORD na SMEAC hazitumiki bali polisi wajikite kwenye Elimination mpaka hapo baadae. Kuwachekea chekea ndo maana wajiona vidume.
 
Mwenzetu unaishi Jf siyo?

Haujawajua vizuri hao jamaa.
 
Watu wanakwapua mipesa ya umma na kujinunulia ma harrier , nako mtaani huwapa heshima kuwa ni ma fighter kumbe ni wauaji maana pesa zilizokwapuliwa zingeboresha huduma za afya na kupkoa uhai
Kikubwa elimu maana wanaua sekta ya elimu ambapo msomi anaweza hata kujiajiri.

Sasa hawa tunaowaona mitaani hata ukiwapa mitaji hawafiki nayobali.

Panya road ni zao la watawala
 
mkuu mwambie kijana wako aachane na makundi
 
Polisi sio wapumbavu kama unavyodhani.
Wao wanajua pia kuna watu hawana hatia.Wanajua kazi yao kuliko unavyotaka kuwafundisha.
Najua watu mnaowatengeneza hawa watoto kuwa magaidi mmepaniki sana.
Ila usidhani viongozi ni makatili na wewe ndio mwenye roho nzuri.
Kwanza inabidi mtuambie mna lengo gani kuwafundisha watoto ugaidi?
 
Tunarudi pale pale, je mahakama zifungwe Ili mamlaka ya kuua yakaimishwe Kwa POLISI?

Au tuwawezeshe POLISI mafunzo na vitendea KAZI kuhakikisha POLISI wetu hawadhuriki na wahalifu??
Kuna kesi za kubaka, Wizi, Utapeli zitaendelea mahakamani Ila Kwa hili la panya road tunaomba tuwapunguzie mahakama KAZI ni mwendo WA Shaba!

Jichanganye na wewe tukulie timing

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
mkuu mwambie kijana wako aachane na makundi
Sina kijana yoyote ila kama mwananchi mpenda haki inabidi nitetea vijana wote wa Dar. Shida yako naona unadhani kuwa (kama walivyo watanzania wengi) tatizo mpaka likupate wewe au mtu wako wa karibu ndiyo inabidi upige kelele. Ndiyo maana umeshafikia conclusion kuwa nina ''kijana wangu'' amekuwa victim. Mimi naumia sana kuona binadamu wenzangu wanateseka na kuuawa kwa bila kufuata sheria. Pengine wewe unadhani uko mbali sana na huu mfumo mbovu wa utawala, lakini nakuhakikishia hauko mbali. Kuna siku utakumbuka maneno yangu kwa sababu siyo lazima uathiriwe na hii ua ua au kamata kamata ya panya road tu, kuna mengi mengine unaweza kuja kuwa victim au mtu wako wa karibu.
 
Kwa hii stori ni kwamba panya road wanafahamika ila raia wema wanaogopa kuwataja kwa kuhofia usalama wao kwa hao hao panya road.
Kama ndio hivyo hao raia wema wafunguliwe mashtaka kwa kuwa wanashirikiana na wahalifu kwa kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Ikifanyika hivi ushirikiano watatoa na wahalifu halisi watapatikana na adhabu stahiki wapate badala ya kuzoa zoa na kusomba watu ambao wengine pengine wala hawahusiki.

Polisi wanashindwa kujiongeza tu. Wakiamua kuwawekea mtego hao panya road ni rahisi tu. Sidhani kama hawayajui maeneo yao ya kujidai.
 
Pole sana wezi wanaudhi sana na wanarudisha maendeleo ya watu nyuma. Yaani ukiibiwa unajisikia kuchanganyikiwa unakitafuta kitu kwenye mfuko wa shati au suruali wakati kitu chenyewe ni kikubwa kwa akili za kawaida hakiwezi kuingia.

Hao ni wezi bado mziki wa majambazi na magaidi, siyo poa kabisa. Polisi fanyeni kazi yenu hamuonei mtu ,apandaye bangi atavuna bangi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…