Brayan_Jk
JF-Expert Member
- Mar 28, 2025
- 210
- 250
1.Kuku wa nyama (broilers) ni GMO🧬 au wamechomwa homoni!💉:
Wengi wanadhani kuku wa nyama (Broiler) wametengenezwa maabara au wanachomwa hormone zinazowafanya waongezeke uzito ndani ya muda mfupi lakini SI KWELI ! Ukuaji wao wa haraka unatokana na uchaguzi wa vizazi bora (selective breeding) kwa miongo kadhaa ambapo walichaguliwa kuku wa asili wenye ukuaji mkubwa wakapanadishia (cross) mpaka kupata broiler na pia lishe bora na yenye protini kubwa ni moja wapo wa sababu
2.Mayai 🥚 yaliyochongeka hutotoa jogoo
SIO KWELI ! Hakuna utafiti wa kisayansi ulioonyesha uhusiano kati ya umbo la yai na jinsia ya kifaranga.Tafiti zimeonyesha kuwa mayai yanapoanguliwa, uwiano wa vifaranga wa kiume na wa kike hubaki karibu na 50:50, bila kujali kama mayai yalikuwa na ncha kali au duara.Umbo la yai huathiriwa na aina ya kuku, umri wake, na fiziolojia yake binafsi, sio jinsia ya kifaranga aliye ndani.
Kama wewe unatamani kuanza ufugaji wa kuku na hujui gharama za kuanzia au unataka kujua kuku aina gani ana faida zaidi tembelea tovuti ya www.primaxtz.com kisha bonyeza fanya makadirio hapa

3.Mitetea 🐔 anahitaji jogoo 🐓ili aweze kutaga mayai!🥚
Uwezo wa kuku jike kutaga mayai unategemea mzunguko wake wa kibaolojia na mwanga wa jua, si uwepo wa jogoo.Kama vile wanawake wanavyopata hedhi bila kushika mimba, kuku jike hutaga mayai hata bila kupandwa na jogoo, jogoo anahitajika Tu kwa Urutubishaji Katika mashamba makubwa ya mayai, kuku jike hutunzwa bila jogoo, lakini bado hutaga mayai mara kwa mara.