Uongo wa kutisha wafugaji hudanganyana kuhusu ufugaji wa kuku (3 itakuvunja mbavu)

Sio theory za ajabu, kama unahisi ni theory za ajabu, prove me wrong
Lakini ukubwa wa gharama na upatikanaji wa vifaranga vya layers huchangiwa kwa sababu kubwa ya kua vifaranga jike kuwapata ni 50-50 Chance , kuna sababu nyingine ila hio ndo kuu
Upo sahihi 100%. Inahitajika mtu uwe na utulivu wa akili na ufanye cost-benefit analysis na ndipo utaweza kuona kwamba kwenye Mradi kama lengo mahsusi ni kupata vifaranga-jike wa mayai(Layers) kwa ajili ya soko; halafu inatokea e.g. unatumia gharama kwa mayai 100, then vifaranga assuming vifaranga vitatotolewa kwa ratio ya 50:50 (vijike:vidume); Mwisho wa siku unajikuta unalazimika kuteketeza(discard) vifaranga 50 vidume ambavyo sio lengo lako.- Ni hasara. Hali inakuwa mbaya zaidi katika ngazi ya mfugaji mdogo ambaye hana utaalam wa kuvitofautisha vikiwa bado ni vidogo e.g. day old chicks - ataendelea kuvilisha kitu ambacho ni hasara kubwa zaidi.
 
Hicho chuo basi tu ni miyeyusho sana.
Wewe kimekusaidia Nini kama Kila kitu Cha maana hata ng'ombe wa maziwa tunatoa Kenya pale?
Hujajibu swali la mdau alokuuliza: Ulitaka mtaalam wa mifugo atoke wapi? Sema e.g. unataka atoke Kenya, Tengeru, VETA au .......
Usikiponde hicho chuo kutokana na kutokujua shughuli yake Kuu kwamba hiyo ni Taasisi ya kutoa Elimu na sio ya Uzalishaji wa mifugo.
 
Huo ni Uongo mkubwa kiwango cha 5G. na haitakaa itokee. Labda huko mbeleni baada ya technolojia kuongezeka.
Nakuona Spidernyoka umecheka. Vipi, ww una amini hilo au unashangaa jibu langu kuwa ni tofauti? Ikikupendeza, Niambie tafadhali.
 
Upo sahihi lakini hujatuambia ni katika mazingira na Maeneo gani. Huku vijijini, kwa mtindo wa ufugaji huria, kuku wa kienyeji ndo mahali pake. Usijaribu kufuga hao wenu wa kisasa - watakufa wote leo-leo.
Ni kweli ukuaji (Growth rate) wa vifaranga wa kuku wa kienyeji ni mdogo sana lakini tukubaliane kwamba kuku wa kienyeji kwenye kibiashara (market demand) anasoko zaidi ya hao wa kisasa.Hata mayai ya kuku wa kienyeji yanasoko zaidi ila shida ni yanayopatikana (Production)hayatoshelezi soko.
Sahihi japo kuna breed moja inaitwa Sasso, hao ni baaab kubwa. Unawafuga ndani week 8 tu, kama uko kijijin unawaacha nje ni kama wa kienyeji tu, na wanataga sanaa
 
Sasso wana umbile kubwa ndio, ni wachakuraji i.e. wabangaizaji wazuri lakini ni wadhaifu mno kwenye visumbufu e.g. viroboto, utitiri, minyoo n.k. Halafu Uatamiaji (sitting on eggs/Incubate)wao sio mzuri -wanalalia mayai muda mfupi then wanayatelekeza. Majogoo ni wavivu kupanda. (Huo ni uzoefu wangu kwa hao sasso - hata huku umasaini ndani ndani huku wapo).
 
Hujajibu swali la mdau alokuuliza: Ulitaka mtaalam wa mifugo atoke wapi? Sema e.g. unataka atoke Kenya, Tengeru, VETA au .......
Usikiponde hicho chuo kutokana na kutokujua shughuli yake Kuu kwamba hiyo ni Taasisi ya kutoa Elimu na sio ya Uzalishaji wa mifugo.
Atoke popote pale. SUA kimejishusha thamani chenyewe mtu anasoma pale miaka zaidi ya 3 mkijua alitoka kule aje awe msaada kwenu wakulima /wafugaji badala yake anakuwa hajui kitu na anaanza upya kujifunza kunyoa akishajua anafunga saloon yake.
 
Kwenye mayai yaliyochongoka nakupinga kwa 98%

Mimi nimewahi ku prove hii njia zaidi ya mara6 nilikuwa nikichagua mayai 10 yaliyochongoka ncha basi yakitotolewa yote nitapata vifaranga 7-8vijogoo tupu hii ni uhakika kama una bisha weka dau tuingie field
Kwanini haikuwa kumi vijogoo tupu ? 10 / 10 ? na umefanya mara 6 which means maya 60; na yale yaliyobaki yalikuwaje majike mangapi na madume mangapi ?
 
Atoke popote pale. SUA kimejishusha thamani chenyewe mtu anasoma pale miaka zaidi ya 3 mkijua alitoka kule aje awe msaada kwenu wakulima /wafugaji badala yake anakuwa hajui kitu na anaanza upya kujifunza kunyoa akishajua anafunga saloon yake.
Yeah. Ni kweli mkuu. Kuna baadhi ya ex-SUA performance i.e. service delivery yao huku maofisini ni ya viwango vya chini mno hadi inashangaza i.e. ni very poor performance.
Kuna wakati inafikia hadi mtu unajiuliza- Hivi huyu kweli kamaliza au katokea SUA kweli au alinunua cheti on line?
Ukienda naye field ndo hapo sasa utashangaa na kujiuliza maswali mengi.
 
Sasso wana umbile kubwa ndio, ni wachakuraji i.e. wabangaizaji wazuri lakini ni wadhaifu mno kwenye visumbufu e.g. viroboto, utitiri, minyoo n.k. Halafu Uatamiaji (sitting on eggs/Incubate)wao sio mzuri -wanalalia mayai muda mfupi then wanayatelekeza. Majogoo ni wavivu kupanda. (Huo ni uzoefu wangu kwa hao sasso - hata huku umasaini ndani ndani huku wapo).
Hawalalii kabisaaa kwa nijuavyo. Wao wanataga tu, na tena ukiwatoa nje, wanataga hovyo hovyoo unaweza hata usijue leo katagia wapi. Ila ni watagaji wazuri
 
Atoke popote pale. SUA kimejishusha thamani chenyewe mtu anasoma pale miaka zaidi ya 3 mkijua alitoka kule aje awe msaada kwenu wakulima /wafugaji badala yake anakuwa hajui kitu na anaanza upya kujifunza kunyoa akishajua anafunga saloon yake.
SUA ilikuwa zamani. Lakini sio SUA tu vyuo vyote tz unakutana na mhitimu unatamani kumnasa vibao, na wanaambiwa waende veta ha ha. Tunakoenda giza nene
 
Hawalalii kabisaaa kwa nijuavyo. Wao wanataga tu, na tena ukiwatoa nje, wanataga hovyo hovyoo unaweza hata usijue leo katagia wapi. Ila ni watagaji wazuri
IMG_20220822_134144_299.jpg

Mimi wangu Huwa wanataga mahali palepale ukweli ni kwamba hawalalii kabisa akilalia siku2 akinyanyuka hapo ni mazima harudi hapo Tena.

Jogoo hayapandi Kwa sababu ya uzito mkuu Huwa hayawezi kukimbia nilishapa kesi2 majogoo kuteguka mifupa likikimbiza mtetea.

Lakini jogoo la sasso ukilifuga bila kuwa chakula chochote kile hata pumba asipewe Huwa ni wepesi sana na hufukuzia vzr tu

Hili ni jogoo la sasso miazi 5 kasoro ukiangalia tu haliwezi kimbiza mtetea
IMG_20220905_073813_914.jpg
 
SUA ilikuwa zamani.
Kweli kabisa. Nadhani wale maprofesa competent hawapo tena. Enzi hizo ukutane na prof. Mtenga, Dr. Katule, Dr.Sharma (yule Mhindi) n.k., hukatizi kimasikhara hata kidogo.
Lakini sio SUA tu vyuo vyote tz unakutana na mhitimu unatamani kumnasa vibao, na wanaambiwa waende veta ha ha. Tunakoenda giza nene
Yeah. Hiki ni kizazi cha Kidigitali zaidi; manake Google imewalemaza sana.
 
Upo sahihi 100%. Inahitajika mtu uwe na utulivu wa akili na ufanye cost-benefit analysis na ndipo utaweza kuona kwamba kwenye Mradi kama lengo mahsusi ni kupata vifaranga-jike wa mayai(Layers) kwa ajili ya soko; halafu inatokea e.g. unatumia gharama kwa mayai 100, then vifaranga assuming vifaranga vitatotolewa kwa ratio ya 50:50 (vijike:vidume); Mwisho wa siku unajikuta unalazimika kuteketeza(discard) vifaranga 50 vidume ambavyo sio lengo lako.- Ni hasara. Hali inakuwa mbaya zaidi katika ngazi ya mfugaji mdogo ambaye hana utaalam wa kuvitofautisha vikiwa bado ni vidogo e.g. day old chicks - ataendelea kuvilisha kitu ambacho ni hasara kubwa zaidi.
Sikuwahi kuiangalia kwa angle hii kwa mfugaji mdogo anaetotolesha mwenyewe, Nashukuru sana kwa Maarifa Palesho
 
Back
Top Bottom