Uongo wa kutisha wafugaji hudanganyana kuhusu ufugaji wa kuku (3 itakuvunja mbavu)

1.Kuku wa nyama (broilers) ni GMO🧬 au wamechomwa homoni!💉:
Wengi wanadhani kuku wa nyama (Broiler) wametengenezwa maabara au wanachomwa hormone zinazowafanya waongezeke uzito ndani ya muda mfupi lakini SI KWELI ! Ukuaji wao wa haraka unatokana na uchaguzi wa vizazi bora (selective breeding) kwa miongo kadhaa ambapo walichaguliwa kuku wa asili wenye ukuaji mkubwa wakapanadishia (cross) mpaka kupata broiler na pia lishe bora na yenye protini kubwa ni moja wapo wa sababu

View attachment 3289114

2.Mayai 🥚 yaliyochongeka hutotoa jogoo
SIO KWELI !
Hakuna utafiti wa kisayansi ulioonyesha uhusiano kati ya umbo la yai na jinsia ya kifaranga.Tafiti zimeonyesha kuwa mayai yanapoanguliwa, uwiano wa vifaranga wa kiume na wa kike hubaki karibu na 50:50, bila kujali kama mayai yalikuwa na ncha kali au duara.Umbo la yai huathiriwa na aina ya kuku, umri wake, na fiziolojia yake binafsi, sio jinsia ya kifaranga aliye ndani.
View attachment 3290009

Kama wewe unatamani kuanza ufugaji wa kuku na hujui gharama za kuanzia au unataka kujua kuku aina gani ana faida zaidi tembelea tovuti ya www.primaxtz.com kisha bonyeza fanya makadirio hapa
View attachment 3290054

3.Mitetea 🐔 anahitaji jogoo 🐓ili aweze kutaga mayai!🥚
Uwezo wa kuku jike kutaga mayai unategemea mzunguko wake wa kibaolojia na mwanga wa jua, si uwepo wa jogoo.Kama vile wanawake wanavyopata hedhi bila kushika mimba, kuku jike hutaga mayai hata bila kupandwa na jogoo, jogoo anahitajika Tu kwa Urutubishaji Katika mashamba makubwa ya mayai, kuku jike hutunzwa bila jogoo, lakini bado hutaga mayai mara kwa mara.
View attachment 3290038
Wanaodanganyana ni wafugaji au wasio wafugaji?
 
Inawezekana vipi kuku jike atage tu bila kupandwa na jogoo..??
 
Mmmh, kazi kweli kweli! Kuna mahali uliambiwa kwamba shahawa za kuku zinahusika na utengenezaji wa yai? Jogoo anahitajika tu pale unapotaka yai la kutotolesha vifaranga!
 
Niliposoma mwanzo tu nilijua mwandishi mtoa post ni mjinga na hana uelewa na kitu alichoandika
 
Ila wewe jamaa una theories za hovyo kabisa! Kwa hiyo gharama inatokana na ugumu wa kupata vifaranga jike? Wala huwazi kama inatokana na gharama za uzalishaji? Unafikri kumlisha layer ni mchezo eeeh? Umuhimu wa layers wenyewe kwenye soko hauwezi kuongeza bei?
Sio theory za ajabu, kama unahisi ni theory za ajabu, prove me wrong
Lakini ukubwa wa gharama na upatikanaji wa vifaranga vya layers huchangiwa kwa sababu kubwa ya kua vifaranga jike kuwapata ni 50-50 Chance , kuna sababu nyingine ila hio ndo kuu
 
1.Kuku wa nyama (broilers) ni GMO🧬 au wamechomwa homoni!💉:
Wengi wanadhani kuku wa nyama (Broiler) wametengenezwa maabara au wanachomwa hormone zinazowafanya waongezeke uzito ndani ya muda mfupi lakini SI KWELI ! Ukuaji wao wa haraka unatokana na uchaguzi wa vizazi bora (selective breeding) kwa miongo kadhaa ambapo walichaguliwa kuku wa asili wenye ukuaji mkubwa wakapanadishia (cross) mpaka kupata broiler na pia lishe bora na yenye protini kubwa ni moja wapo wa sababu

View attachment 3289114

2.Mayai 🥚 yaliyochongeka hutotoa jogoo
SIO KWELI !
Hakuna utafiti wa kisayansi ulioonyesha uhusiano kati ya umbo la yai na jinsia ya kifaranga.Tafiti zimeonyesha kuwa mayai yanapoanguliwa, uwiano wa vifaranga wa kiume na wa kike hubaki karibu na 50:50, bila kujali kama mayai yalikuwa na ncha kali au duara.Umbo la yai huathiriwa na aina ya kuku, umri wake, na fiziolojia yake binafsi, sio jinsia ya kifaranga aliye ndani.
View attachment 3290009

Kama wewe unatamani kuanza ufugaji wa kuku na hujui gharama za kuanzia au unataka kujua kuku aina gani ana faida zaidi tembelea tovuti ya www.primaxtz.com kisha bonyeza fanya makadirio hapa
View attachment 3290054

3.Mitetea 🐔 anahitaji jogoo 🐓ili aweze kutaga mayai!🥚
Uwezo wa kuku jike kutaga mayai unategemea mzunguko wake wa kibaolojia na mwanga wa jua, si uwepo wa jogoo.Kama vile wanawake wanavyopata hedhi bila kushika mimba, kuku jike hutaga mayai hata bila kupandwa na jogoo, jogoo anahitajika Tu kwa Urutubishaji Katika mashamba makubwa ya mayai, kuku jike hutunzwa bila jogoo, lakini bado hutaga mayai mara kwa mara.
View attachment 3290038
Hii namba 3 imezagaa sana na wengi wanaamini huo ujinga. Wanasema "kuku wa kisasa hawana baba".
Nimekutana nao wengi nikawaelimisha
 
Yote kwa yote, ufugaji wa kuku wa kienyeji ni changamoto mnooo hasa katika kuwaongeza. Rate ya ukuaji wa vifaranga wa kienyeji ni very slow halaf. Kwakifupi hawafai kwa ufugaji wa kibiashara😂
Upo sahihi lakini hujatuambia ni katika mazingira na Maeneo gani. Huku vijijini, kwa mtindo wa ufugaji huria, kuku wa kienyeji ndo mahali pake. Usijaribu kufuga hao wenu wa kisasa - watakufa wote leo-leo.
Ni kweli ukuaji (Growth rate) wa vifaranga wa kuku wa kienyeji ni mdogo sana lakini tukubaliane kwamba kuku wa kienyeji kwenye kibiashara (market demand) anasoko zaidi ya hao wa kisasa.Hata mayai ya kuku wa kienyeji yanasoko zaidi ila shida ni yanayopatikana (Production)hayatoshelezi soko.
 
Back
Top Bottom