DOKEZO Uongozi wa IAA, tafadhali chukueni kwa uzito suala la weledi, maadili ya ufundishaji na usimamizi wa mitihani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna malalamiko yanayojirudia kutoka kwa wanafunzi, hasa katika ngazi ya Master’s, kuhusu namna baadhi ya mambo yanavyosimamiwa chuoni. Hili si suala la mwanafunzi mmoja; ni jambo ambalo wanafunzi wengi wamekuwa wakilizungumzia na kujaribu kulifuatilia bila kupata majibu au suluhisho la kuridhisha.

Moja ya mambo yanayolalamikiwa ni mwalimu kumtaka mwanafunzi anunue kitabu chake kwa bei kubwa, huku mwanafunzi asiyenunua kitabu hicho akidaiwa kupata matokeo mabaya au hata kufeli mtihani wa somo husika. Ikiwa madai haya ni ya kweli, hii ni changamoto kubwa ya kimaadili na kitaaluma ambayo inahitaji kuchunguzwa kwa umakini.

Pia kuna malalamiko kuhusu usimamizi na uchakataji wa mitihani na matokeo. Wanafunzi wengine wameripoti kukuta marks zao hazijaakisi walichofanya kwenye mitihani, huku wengine wakidaiwa kuandikiwa kuwa hawakufanya mtihani, licha ya kuwepo kwenye mtihani na kusaini attendance sheet.

Swali ni: utaratibu wa kuhakiki na kuthibitisha matokeo kabla hayajawasilishwa au kupakiwa ukoje? Je, kuna mfumo madhubuti wa internal moderation, examiners’ board au chombo kingine kinachopitia na kuhakiki matokeo kabla hayajatangazwa?

Kinachokatisha tamaa zaidi ni pale mwanafunzi anapojaribu kufuatilia suala kama hili lakini hakuna hatua inayoonekana kuchukuliwa au majibu yanayotolewa kwa wakati na kwa uwazi.

Tafadhali, tusisahau kwamba nyuma ya kila mwanafunzi kuna muda, fedha, nguvu, sacrifices na malengo ya maisha. Mwanafunzi anayesoma Master’s hajafika hapo kwa bahati. Amewekeza katika elimu yake na anastahili kuhudumiwa katika mazingira yenye haki, weledi, uwajibikaji na maadili.

Hili si ombi la kuwabeba wanafunzi au kuwapa marks ambazo hawastahili. Ni ombi la kuhakikisha kila mwanafunzi anapata alama kulingana na kazi na performance yake halisi, na kwamba malalamiko ya kitaaluma yanashughulikiwa kwa utaratibu unaoeleweka, usio na upendeleo na unaoweza kukaguliwa.

Uongozi wa IAA, tafadhali chukueni malalamiko haya kwa uzito. Chunguzeni madai haya, boresheni mifumo ya usimamizi wa mitihani na results, na hakikisheni wahadhiri wote wanafuata viwango vya weledi na maadili ya taaluma.

Pia soma:
~ Changamoto kubwa kwa Wanafunzi wa Masters IAA: Matokeo, Appeals na Dissertation
~ Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) boresheni huduma zenu za online, zinatukwaza Wanafunzi
~ Serikali ya wanafunzi chuo Cha uhasibu Arusha (IAA) main campus - Arusha umefanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi
~
Chuo cha uhasibu Arusha kinawalazimisha waombaji wajiunge chuoni hapo,hakuna option ya kuahirisha maombi,na wanachagua kozi ambazo hawajaomba
 
Nimeona uzi mwingine wanalalamikia hili pia. Hope watafanyia kazi.
 
Asee hii inaumiza sanaa, inabidi uongozo iliangalie kwa undani zaidi watu wanapoteza haki zao.😢
 
ni vyema mambo yakiwekwa sawa
 
Back
Top Bottom