Uongozi wa UDSM watoa angalizo uwepo wa CHATU maeneo ya Shule ya Msingi Mlimani

Yeah. Ni sawa na wale wasemao "Ukinipiga umenionea, ukiniacha umeniogopa".
AfanaAlek! Bora........ kuliko watu waendelee kuishi kwa hofu. Kama mnyama huyo ana njaa lazima awinde chakula chake. Je, hapo maeneo ya chuo kunapatikana chakula chake? au atawinda binadamu e.g. watoto hata watu wazima au wanyama wafugwao majumbani mbuzi,kuku,bata n.k. Tutafakari. Chatu akishiba vizuri anaweza kukaa hata wiki 1-2 bila kuhitaji tena kuwinda au Kula.
 
Kwa kawaida ni nadra sana Afrika chatu kumeza mtu, kwa sababu binadamu hayupo kwenye menu yake, ila ukijichanganya utamezwa tu...
Pia chatu wa Afrika siyo wakubwa kivile.

African rock python ni wa tatu kwa ukubwa katika aina ya chatu.

Chatu ambao mpaka sasa wamekuwa documented kumeza watu ni wale wanaopatikana kusini mashariki mwa Asia. Na hao wanaitwa reticulated pythons ambao ndo chatu wakubwa kabisa katika jamii ya chatu.
 
Wakidhuru mtu ndipo utasikia waziri husika anajitokeza kutoa tamko
 
Ndio uko sawa mkuu. Lakini mbona wanasema Simba akiishiwa hula majani? Chatu ni mwindaji mzuri sana wa wanyama wadogo wadogo kama digidigi, ngedere, Tumbili(Nyani) mbwa, n.k. Sasa Kama mahali hapo hawapatikani hao wanyama chatu atakuwa hana jinsi- inambidi chatu ajiongeze na hukamata watoto/binadamu dhaifu. Mnyama huyu hufanya mawindo yake kwa kuvizia na endapo itamlazimu ataingia kwenye makazi ya watu kusaka chakula. Je ni nani atakuwa wa kwanza kuathirika kama sio binadamu?
 
Hataweza Kumla Ila Atamsababishia Madhara
 
Ndiyo, chatu akipata windo lolote lile anakula tu. Ila kwa hawa chatu wa Afrika, kumla mtu inabidi mtu huyo awe na mwili mdogo.

Hata wale reticulated pythons wa kule Indonesia ambao wamekuwa documented kumeza watu, ni wakubwa sana. Wanaanza futi 19 mpaka 23 hivi.

YouTube kuna video nyingi tu zinazoonyesha chatu [Burmese pythons] wakijaribu kumeza mawindo ambayo ni makubwa na mwisho wake wanaishia kuacha na kukimbia.

Ila chatu hata kama si mkubwa sana, bado anauwezo wa kukuua ukiingia kwenye 18 zake.

Akishajivingirisha kama huna wa kukusaidia, hapo ni kifo tu.
 
Mimi nilikuwa narandaranda maeneo hayo wakati huo hadi giza linaingia zaidi ya miaka 17 iliyopita kumbe ningeweza kumezwa na chatu, aiseeee!
Aaah Mkuu, kwani huyo chatu alikuwepo hapo miaka 17 iliyopita? Kipindi hicho Wewe hukujua na pengine ulikuwa mtoto/kijana. Huyo chatu mbona ni wa juzi tuu?
Exactly yes. Akishajiviringisha, kitendo ambacho ni cha haraka sana, yan chap' na kama atashindwa kukumeza kutokana na ukubwa wa mwili wako, lakini si atakuwa amekwisha kukuua? Mbwa ndo anakuwaga mwathirika mkubwa kwani mbwa hujipeleka mwenyewe kwa chatu kutokana na ile tabia yake ya kutaka kushambulia/kung'ata.
 
Nachukulia kama chatu anapatikana hapo mjini leo pengine miaka 17 iliyopita walikuwepo wengi zaidi manake hata hiyo Mlimani City ilikuwa pori tupu wakati nafanya jogging zangu usiku usiku.
 
W Wewe acha lawama za kipumbavu,,

UDSM kutoa tangazo huoni Kam inasaidia watu kufahamu kuwa maeneo tajwa ni hatar hivyo hakuna atakayesogea eneo Hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…