Ndiyo, chatu akipata windo lolote lile anakula tu. Ila kwa hawa chatu wa Afrika, kumla mtu inabidi mtu huyo awe na mwili mdogo.
Hata wale reticulated pythons wa kule Indonesia ambao wamekuwa documented kumeza watu, ni wakubwa sana. Wanaanza futi 19 mpaka 23 hivi.
YouTube kuna video nyingi tu zinazoonyesha chatu [Burmese pythons] wakijaribu kumeza mawindo ambayo ni makubwa na mwisho wake wanaishia kuacha na kukimbia.
Ila chatu hata kama si mkubwa sana, bado anauwezo wa kukuua ukiingia kwenye 18 zake.
Akishajivingirisha kama huna wa kukusaidia, hapo ni kifo tu.