Uongozi wa UDSM watoa angalizo uwepo wa CHATU maeneo ya Shule ya Msingi Mlimani

Uongozi wa UDSM watoa angalizo uwepo wa CHATU maeneo ya Shule ya Msingi Mlimani

Kwa yale mapori ya UD pale na wanafunzi hupenda sana kujilaza kwenye vivuli vya miti mida ya mchana maana kuna hali ya hewa nzuri kuna siku atamwezwa mwanazuoni mmoja chatu anageuka lecturer wallah.
Na UD kuna mapori haswaa, khaaaah
 
Hahahahaa wale ngedere kama watu, wanaingia hadi vyumbani kuchukua vyakula mkiacha madirisha wazi.
Kuna siku moja tunakunywa chai kwenye vimbweta mikoba tumeweka pembeni ndegere mmoja akachukua walet ya mwenzetu akaondoka nayo. Yule dada alilia huku anamuomba " naomba nirudishie walet chukua hata maandazi haya"
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakurudisha alienda nayo mitini bahati nzuri akaiangusha anavyoruka. Ngedere wa UDSM wakorofi na wachokozi mno hawaoni shida kuja kuchukua chakula mezani unapokula.
Kwanza kwann ule msitu usiondolewe? Chuo kikubwa kuzungukwa na Wanyama wa Porini, Si upumbavu huu.

Miaka yote niliyokaa pale Main campus nilikua nashangaa sana
 
Wametoa tahadhari lakini hawajasema nini kimefanyika au kinakusudia kufanyika.. Nilitegemea Jeshi Usu la TAWA 'limejaa' UDSM kwa sasa kumtafuta mpaka apatikane pamoja na makazi yake na uzao wake na ahamishiwe sehemu nyingine.. kama waliweza kuondoa nyoka wote Chamwino, sidhani kama hili litawashinda..
 
Hao wachina waliojaa hapo udsm si ndio msosi wao huo wautafute.
 
Kwa yale mapori ya UD pale na wanafunzi hupenda sana kujilaza kwenye vivuli vya miti mida ya mchana maana kuna hali ya hewa nzuri kuna siku atamwezwa mwanazuoni mmoja chatu anageuka lecturer wallah.
Uliona wapi chatu kameza binadamu?
 
Mimi nilikuwa narandaranda maeneo hayo wakati huo hadi giza linaingia zaidi ya miaka 17 iliyopita kumbe ningeweza kumezwa na chatu, aiseeee!
Huyo chatu alikuwa hajazaliwa.
 
Back
Top Bottom