Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Yote ya yote shukrani kwa wake kwa waume ambao kupitia jasho lao, hekima, busara na kazi za mikono yao, taifa letu limeendelea kuwa na uhuru, amani na utulivu. Ahsanteni kwa kuendelea kuidumisha sifa ya nchi yetu ya kisiwa cha amani.
Mlipopungukiwa ni ubinadamu sote si wakamilifu, jiinueni na kujirekebisha ili kuendelea kutimiza wajibu wenu kwa weredi na uzalendo
 
Tungetambua ni kiasi gani hao watu wa TISS wanavyotoil kuhakikisha taifa liko salama, tungefunga na kuwaombea mema kila siku

Hii amani tunayoiona hapa kwetu huku majirani zetu Congo, Burundi na Kenya wakichinjana haipo tu kwa bahati mbaya. Kuna watu wanavuja jasho na damu kuilinda!
 
Tungetambua ni kiasi gani hao watu wa TISS wanavyotoil kuhakikisha taifa liko salama, tungefunga na kuwaombea mema kila siku

Hii amani tunayoiona hapa kwetu huku majirani zetu Congo, Burundi na Kenya wakichinjana haipo tu kwa bahati mbaya. Kuna watu wanavuja jasho na damu kuilinda!
Labda niulize tu Kongo, Burundi na Kenya Kuna tatizo gani katika
idara zao za Usalama?
 
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza

Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye eneo la mwisho ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika, kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.

Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini je tumeangalia nini athari yake?

Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza hayo majukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?

NAULIZA TU.
Vipi wamekurekodi lini mkuu?? Mbona maneno mengi lakini mwisho ni mapovu ya kurekodiwa!! Pole mkuu!
 
Unaweza tumwa Ukafanye misheni flani Kubwa sanaa ambayo Inabdi iwee siriii... Unaweza maliza kiroho safii lakini akatumwa mtu ajee Kukumaliza na wew lakini hata ambiwa sababu ya kukua wew... NA HUWA HAWAJUANII WENGI WAOOOO...!!
 
Back
Top Bottom