Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Ukijua kazi ya idara hiyo huta rudia kuwalaumu tena shida sio mfumo wa ajira shida ni katiba kazi yao wana fanya ila nini baada ya hapo ndo shida ilipo
 
Idara ya Usalama wa Taifa iweke wazi Ofisi zake zilipo na iajiri kwa wazi kama CIA wanavyofanya. Sio mambo yote ya kufanyia gizani
Ofisi zao zimejificha hawataki watu wajue as if wanafanya maajabu gani sijui..

Hii mifumo ya kuficha ofisi za usalama ni tabia ya kisocialism tena kipindi kile cha cold war..

Nowdays ni mwendo wa technologies zaidi na sio mtindo tulionao..
Wanapaswa waajiri watu intelligent kwelikweli..na taasisi ya cha EGA kingekuwa chini ya idala hii..
 
Nahisi shida ni mfumo tayari ni mmbovu hawa usalama wa Taifa wao wanajua kazi Yao ni kulinda viongozi tu

Kwa mfano hizo gali zilizolipiwa alafu Hadi Leo hazijafika ilitakiwa usalama wa Taifa wawe wanajua kuhusu hilo jambo na kumtalifu Raisi kabla ya CAG in short hao usalama Taifa hawana faida yoyote katika nchi hii
 
Kwa demokrasia ya kuwaogopa na kuwaonea haya majizi ya pesa za umma hata miaka elfu wizi hautaisha sio miaka kumi tu ! Watu wasijifiche kwa kulaumu uongozi uliopita ! Upigaji wa namna hii ulikuwepo hata kabla ya Magufuli tena ulikuwepo karibu kila awamu !! Kinachotakiwa ni kaudikteta fulani hivi kuzilinda mali za Umma bila hivyo Nchi itaendelea kukopa mpaka itafilisika !! Mark my words !!
 
Nikweli kabisa aliefeli HAWEZI kumzika Alie faulu form4.
 
Mbona jpm alikuwa dictator lakini kila kitu kikaenda mlama. Atcl, ttcl, trc vyote vikawa ni majanga tu
 
Mbona jpm alikuwa dictator lakini kila kitu kikaenda mlama. Atcl, ttcl, trc vyote vikawa ni majanga tu
Pengine hakuwa kiongozi dikteta mzuri ! Lakini alionyesha kwa vitendo kukerwa na wizi wa mali za umma na alikuwa anachukua hatua papo hapo bila kuchelewa !!
 
Idara siyo tatizo, tatizo lipo kwa wanaoshauriwa na si tulikubaliana one man show ni udikteta?!

Tatizo lipo TAKUKURU ndio walipaswa kuchukua hatua na siyo TISS labda sheria ZA uundaji wa TISS zirudi bungeni kurekebishwa ili waweze kukamata, na kufungua kesi.

Naona watu wengi ni wagumu kuelewa IDARA haina meno ya kuwachukulia hatua wezi wa mali za umma.

Idara ipo chini ya rais siyo independent, kama rais ndiyo vile ameshikwa na kuzungukwa na marafiki walafi na mafisadi, idara itafanya nini?
 
Nenda kasome ACT ya TISS, sio kazi yao kujishughulisha na ubadhirifu, ufisadi au uhujumu uchumi.
Ni kazi yao kuhakikisha hakuna uhujumu uchumi ufisadi wala ubadhirifu wa mali za umma.

Kiutendaji TISS inatakiwa isimamie usalama wa nchi, uchumi na siasa za kitaifa.

Ila kwa huu mfumo mbovu hawatimizi majukumu yao.
 
Mimi huwa nashangaa vipi kuna vijana wa Usalama lkn majengo yanajengwa chini ya kiwango mpaka Mwenge waje wagundue.
 
Sasa wewe inerpol...
Mkuu, hii ni njama yako ya kufifisha hoja ya mleta mada. Mleta mada kaleta hoja yenye nguvu, ndiyo maana nimemuuliza swali la msingi kwa maoni yangu kama raia wa nchi hii.

Mkuu naomba umpe nafasi mleta mada afanye kazi yake ya kuleta majibu ya kulisaidia Taifa. Asante.
 
Mimi huwa nashangaa vipi kuna vijana wa Usalama lkn majengo yanajengwa chini ya kiwango mpaka Mwenge waje wagundue.
Ila mkuu samahani una elimu gani?unafahamu kazi ya tiss kisheria na kikatiba?
 
Mimi huwa nashangaa vipi kuna vijana wa Usalama lkn majengo yanajengwa chini ya kiwango mpaka Mwenge waje wagundue.
Ngoja nikusaidie kazi ya tiss ni kukusanya taarifa kuzichakata/kuzichambua na kuzipeleka kunakohusika na kushauri wenye mamlaka ya kuchukua hatua ni wale wanaopelewa taarifa na wanatimiza Sana majukumu ipasavyo.
 
Nenda kasome ACT ya TISS, sio kazi yao kujishughulisha na ubadhirifu, ufisadi au uhujumu uchumi.
Broo kajiridhishe! Utagundua kwamba TISS inawajibika kuishauri serikali juu ya mambo ya kiusalama, uchumi, siasa na kutoa mapendekezo stahiki ya kutatua changamoto zinazoendana na hizo.

Ndiyo maana JPM aliwabanaTISS wakawa wanajitahidi kuibua ubadhilifu na magendo mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…