Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza
Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye eneo la mwisho ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika, kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.
Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini je tumeangalia nini athari yake?
Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza hayo majukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?
NAULIZA TU.
Kama uliingia TISS kwa kutoa rushwa au kutumia cheti cha mtu, basi tayari umefanya kosa kubwa sana kwani umevunja miiko inayopaswa kufuatwa wakti wa kuteua makuruta.
Sasa linapokuja suala la uhakiki ambalo linafanyika sasa, wengi wa vijana ambao waliingia kwa kuhonga au kwa kutumia majina makubwa wanapewa muda wa kujitafakari kisha kuondoka ndani ya idara hiyo bila kulipwa chochote.
Hivyo kama uliondolewa kwa sababu hizo hapo juu, basi negative side effects zitakuwa more devastating kuliko positive side effects.
Kuna mdada mmoja nilikuwa namfahamu kwa miaka mingi lakini sikudhani kama alikuwa akifanya kazi huko, ila hivi karibuni alikuja kwangu huku akilia sana.
Nilimuuliza kulikoni bibie, akasema ameambiwa kwamba aweza kustaafu kazi lakini hakutakuwa na malipo yoyote stahiki kama kiinua mgongo wala fedha za kusafiria kwasababu yeye alitumia vyeti vya mtu mwingine.
Fikiria mtu amepiga kazi miaka zaidi ya 30 kazini kwa cheti bandia yaani hakukuwa na uchunguzi mahiri kubaini mtumishi mtarajiwa yaani Vetting na matokeo yake huyu dada yangu ametumbukia shimoni.
Hivyo basi side effects zaweza kukupata ukiwa katika mazingiza hayo au mazingira mengine kama kustaafu ukiwa hukujenga nyumba, au ulikuwa unahanja na vimwana na hukuwa na akili ya future.
Lakini Positive side effects zingine zipo na ukipata nafasi tembelea eneo la Mbweni uone nyumba za maana zilizojengwa na wastaafu na hata wale ambao ndo umri wasogea.