Sio Ishu ya Tetesi ndugu, ndivyo ilivyo kwa uhalisia wake; Kila Idara, Mfumo wa utendaji unapoanzishwa basi lazima jamaa wawekwe.
Hii ilianza zamani toka enzi za nyerere, Kila taasisi ilipoanzishwa aliangalia Mfumo mzuri wa kupenyeza watu wa Usalama ili kuhakikisha Taasisi, Idara au Mfumo husika unafanya kazi Bila kuleta wasiwasi kwenye usalama wa Taifa.
Wakati wa kuanzishwa Mfumo wa Vyama vingi, Nyerere aliigomea hii kitu kabisa (Alikuwa hataki mfumo wa vyama vingi), Lakini ishu ilikuwa atawezaje kuhakiksha usalama wa Taifa kwenye Vyama hivyo (ndani katika utendaje wake), Ilimchukua muda tangu azimio la vyama vingi kutakiwa mpaka jamaa aliporuhusu. Ndipo akaweka Utaratibu kuwa Ukitaka upate usajili wa kudumu basi chama cha siasa basi lazima kipate wanachama japo 200 angalau katika mikoa kumi. Sasa hapa ndipo inakuwaga ndio pale Usalama wa nchi Yetu unaingiza watu wake japo 5, na mara nyingi si watu wa kawaida unakuta ni watu walio very smart kwenye uwezo wa kupambanua mambo, wana mtazamo chanya kabisa kabisa juu ya hicho chama, wanajenga hoja vizuri kiasi kwamba ni rahisi kupewa nyadhifa za juu katika chama, ila Core-business yake ni Undercover; (wako kazini kiusalama na si kichama), Achana na Usalama hawa vijana wa siku izi, anatoa kitambulisho, mara bastola; Usalama makini nawaambia huwezi kumtilia shaka ndugu yangu, Angali comment yangu nyingine hapo juu, kuna mtu nimefanya nae kazi serikali ya awamu ya 3 yotee, same Dept, Tukaenda kusoma ughaibuni tukarudi awamu ya Jk miaka 3+ tuko nae ofisini ila nikamuona amevaa Gwanda anapewa Mkono na Mheshimiwa Rais wa Awamu hii ya 5, Nilistaajabu sana; hawa jamaa mtu anafanya kazi yake kwa ueledi huku akifanya jitihada zote asiweke wasiwasi juu ya walio karibu nae; Katika Idara zote na Taasisi za Serikali Lazima kuwepo watu wa system (ni lazima) BOT, Taasisi za Elimu, Mashirika ya Umma yote, Mamlaka zotee( EWURA,TRA,TRL,TFDA,TPA,MSD,SUMMATRA yaani mamlaka zote) Tena Hao TISS wanakuaga wanapanda taratibu vyeo kutokana na Usmart wao (Refer Mkuu wa Idara ya Usalama wa sasa MK)
Most of high political Leaders hasa wale walionza toka Mfumo wa Vyama vingi umeingia nchini, Believe me ni Under cover, Wako kiusalama zaidi kuliko kichama.
NB: Usalama wa Taifa uko katika nyanja nyingi sana, Kiuchumi, Kijamii etc ndio maana watu wanawekwa kwenye hizo Idara, vyama vya siasa, mashirika ya kijamii na Mamlaka zote; Infact Usalama wa Nchi ndio unahakikisha unapata Raisi ambaye hana viashiria vya kuhatarisha Usalama wa Taifa letu (i hope mtanielewa) Huwa wanapropose na kuhakikisha wanatoa Support stahili.