Mashudu tu kama ya Lucas Mwashambwa ,au ndiyo umekuja kivingine?
 
ephen_ bandiko kama la mlishikaji au kabadili ID?
 
Namuomba mwenyezi Mungu sana mjalie Rais wetu Dkt. Samia afya njema. Ampe macho ya kiroho anione popote nilipo, aniite mimi ili nikamuonyeshe fedha mahali zilipo za kukijenga na kukiimarisha chama ngazi za shina tawi kata na jimbo.

Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikunguruma kama simba baada ya kikao fulani cha chama kabla hakijaisha niliona wanassem mafukara wakipigana vikumbo kuwagombea viongozi walau wawaachie chochote.

Nikaumia sana moyoni hasa kwa kuzingatia mambo ya kufanya yapo ila waliopewa nyadhifa za kufanya maamuzi ni wakali wakali muda wote. Mikwara mingi na vitisho vya kufa mtu kinyume na viapo walivyoapa na kuahidi kuwa wanyenyekevu.

Mheshimiwa Daniel Godfrey Chongolo aliyekuwa Katibu mkuu CCM taifa nakumbuka tarehe 15/06/2022 katika baraza kuu la UWT huko Dodoma alisema sisi ni viongozi tuliopewa dhamana ya kusimamia katiba kanuni na miongozo halali ya chama chetu.

Mwisho wa kunukuu.

Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk 153 kifungu 04 ili kupata uhalali wa kwenda kusoma kanuni za fedha na mali za chama na jumuiya zake toleo 2018 uk 164-165 kwa mazingatio makubwa.

Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk 09-10 ibara 14(5) kwa msisitizo. Ilani ya CCM uk 01 ibara 04 na ibara 10 na 11. Nakumbuka tarehe 5/august/2021, Padre Dkt Faustine Kamugisha wa parokia ya Minziro jimbo la Bukoba alisema ukitaka kumsaidia mtu mwenye matatizo muache aongee sana. Na ili aongee msikilize na onyesha juhudi kwamba unamsikiliza.

Mwisho wa nakumbuka tarehe 13/07/2022. Comrade Shaka Hamdu Shaka akiwa katibu NEC itikadi siasa na uenezi CCM taifa akiwa ndani ya ZBC- zanzibar alisema Chama chetu ni chama cha kusikiliza watu. Mwisho wa kunukuu.

Nikitazama chama cha mapinduzi ngazi za chini huku machozi yananitoka. Hali ni mbaya sana. Wanachama wana maisha magumu. Hata ikitokea mwanachama kafariki hapati huduma stahiki anazo zistahili kama mwanachama wa chama tawala hasa kwa kuzingatia chama hiki kina mali nyingi zisizo wanufaisha wanaccm walio wengi.

Wanachama wakiwezeshwa ni wazi watawahudumia vyema wananchi wenye changamoto.

Wananchi walio wengi na wenye changamoto zilizo nyingi huishi huku ngazi za chini .

Huku ndiko kunako paswa kurekebishwa saana na kuboreshwa kuliko huko wilaya , mkoa na taifa.

Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar Katika baraza la eid el fitr nakumbuka tarehe 03/05/2022 alisema tumuombe mwenyezi Mungu (ili) atuongoze katika kufanya mambo mema na kuyakimbilia yale yote ya kheri ili tupate kufanikiwa hapa duniani na kesho mbele ya haki.

Mwisho wa kunukuu.

Kufanikiwa kwetu wana ssem ni kuwajali watu wanyonge miongoni mwetu kwani sio kheri kukimbilia nje kuwajali watu wa nje huku waliopambana kutuinua sisi wakiwa ni mafukara na hawana hata hope yeyote ya kufikiriwa kuinuliwa kimaisha.

Wanassem ni wananchi pia ambao wanatamani waboreshewe maeneo yao ili kazi zao za kusikiliza watu na kuisimamia serikali iweze kutekeleza ilani ya ccm.

Wanassem wamekuwa wakilia vilio vikubwa na machozi yao kupotelea baharini pasipo kusikilizwa wala kupewa hope.

Mheshimiwa Daniel Chongolo, Katibu mkuu wa zamani ccm taifa nakumbuka tarehe 01/06/2022 alisema hatuwezi kuwa tunafanya masihara kwenye mambo ya msingi.

Mtu umepewa dhamana lazima uwajibike kwa dhamana uliyopewa. Unatakiwa kutumikia wananchi lazima utumikie wananchi. Wananchi hawawezi wakawa wana kilio (ambacho) hakifiki mwisho. Wamelalamika leo. Wamelalamika kesho. Wamelalamika jana. Sisi (viongozi wenye dhamana) tupo (tu). Tumekaa kwenye ofisi. Mwisho wa kunukuu

Diwani Manyama. Diwani wa kata ya wazo dar es salaam, nakumbuka tarehe 19/06/2022 alisema Uongozi tunapopewa ni utumishi kama utumishi mwingine, Twende tukatumie nafasi tulizopewa kutatua kero za wananchi. Mwisho wa kunukuu.

Mazingira mazuri ya kufanyia kazi husaidia watu wanaoitumikia jamii kufanya kazi kwa tija. Mfano katiba ya ccm inamtaka balozi atunze kumbukumbu. Atazitunzia wapi. Je matawi yasiyo na ofisi yanatunzaje kumbukumbu za chama!? Je utunzaji wao hao wasio na ofisi uko kisheria?

Tusome ilani ya ccm uk 01 ibara 04. Nakumbuka tarehe 05/08/2022, Mheshimiwa Rais Dkt Samia Katika uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa mbeya alisema Utafiti unaonyesha kwamba mwaadamu akifanya kazi kwenye mazingira mazuri. Basi kama ni haki (anaitoa ) anakuwa ametulia anatoa haki ipasavyo. Kama ni huduma anatulia anatoa huduma ipasavyo. Mwisho wa kunukuu

Saa nyingine tunawalaumu saana wanaccm huku ngazi za chini ila mazingira ya kazi zao ni magumu kiasi kwamba hata haki hazitekelezeki inavyo stahili .

Ni jukumu letu makada kuyaona haya kwani haya ni aibu kwetu wote wazalendo ndani ya ccm. Mheshimiwa Wanu Hafidh Ameir. Mwenyekiti wa mwanamke initiative foundation Zanzibar

Binti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nakumbuka tarehe 19/06/2022, alisema Changamoto za kijamii ni nyingi na zinahitaji nguvu ya pamoja (ili) kuzitatua. Mwisho wa kunukuu

Wanaccm hatuna ofisi za kutosha ngazi za chini. Hakuna kumbi za mikutano, hakuna vyoo, hakuna maji.

Na sisi ndiyo tunatakiwa kuwa na vitu hivyo vya msingi ili tutakapo kuwa tunaieleza jamii kuwa tutaiondolea umaskini ione tunamaanisha hivyo.

Pastor Sunbella Kyando wa the reality of christ church nakumbuka tarehe 17/11/2020 alisema (mwenyezi mungu) kama kakuita kwenye siasa, yanayotokea kwenye siasa yatakuwa yanakutesa sana.

Unaweza ukaona kila mtu anafurahia hilo eneo.

Lakini kila wakati ukiangalia kwenye hiyo sekta moyo wako unatoka machozi. Ukiona vinavyotokea kwenye siasa havikuumizi(ujuwe) wewe sio mwanasiasa. Mwisho wa kunukuu

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara huko dodoma, nakumbuka tarehe 14/08/2022 alisema Kipaumbele (chetu) cha kwanza ni wananchi kule chini. Mwisho wa kunukuu

Tusome katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania 1977 toleo 2005 ibara 08 yote. Ibara 26 yote bila kuiacha ibara 9(a)(b)(f)(h)

Mheshimiwa rais Dkt. Samia Suluhu Hassan August 2022 Katika hafla ya kuwaapisha wakuu wa mikoa alisema na (katiba ) iliyoko mezani kwangu ni katiba (ya )1977 toleo 2005.

Dkt. Dotto Mashaka Biteko, Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati akimuwakilisha mheshimiwa rais dkt samia suluhu hassan katika shughuli maalumu za waumini wa kikatoliki huko tabora Alisema Tupambane kuwaondoa watanzania kwenye umaskini na kuwaletea nafuu kubwa ya maisha. Mwisho wa kunukuu

Kauli hii inawezekana tu pale baadhi ya viongozi watakapoamua kubadili mitazamo yao juu ya watanzania wanajitokeza wakiwa na ubunifu wakiomba kusaidiwa walau kuidhinishiwa mambo fulani ili wayafanye wazalishe ajira kwa wenzao wasio wabunifu.

Sisi wabunifu hatupati msaada kabisa huku ngazi za chini. Watu hawatusaidii. Wanaamini kuwa tukiwasaidia maskini wao wasiopenda kuwasaidia watapoteza vyeo vyao ndiyo maana hawako tayari kutusaidia.

Kila tukiwaomba hawataki na ushahidi wa barua nilizo waandikia ninao ila wanakaa kimya tu.

Nakuomba sasa mheshimiwa rais uingilie kati , uniite mheshimiwa rais huku nikiamini kukuona wewe itakuwa ni mwanzo wa kufanya maamuzi magumu .

Nakumbuka august 2022, Mheshimiwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan alisema Mwamuzi wa mwisho ni mimi kama rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania na amiri jeshi mkuu. Ni mimi. Mwisho wa kunukuu.

Kwa kulijuwa hili mheshimiwa rais nakuomba mheshimiwa unitizame kwa jicho la kipekee ili nami niweze kufanya jambo lisilo na bla bla la kuacha alama ndani ya chama ingawaje sisi wabeba maono tunakuwa na vita vikubwa ili kuzuiwa tusitimize maono hayo.

Pastor sunbella kyando wa the reality of christ church, Nakumbuka tarehe 18/03/2022 alisema Kuna mawazo (ambayo) mungu ameyaongea ndani yako na unayadharau Unayaona ni ya kawaida. Lakini hayo mawazo yamebeba hatma za watu Hayo mawazo yamebeba miisho ya watu

Hayo mawazo yamebeba destiny za watu na hao watu hawatakufa kama utakubali kutengeneza hilyo safina. Mwisho wa kunukuu

Naamini kwa usikivu na upendo wa rais wetu alio nao kwa ccm naamini ataniita ili afanye maamuzi ili niweze kufanya kazi kuacha alama ndani ya ccm.

Meja Charles Mbuge akiwa mkuu wa mkoa wa Kagera Nakumbuka tarehe 10/06/2022 alisema (Dkt. samia suluhu hassan) ni rais mwenye maono, Rais mwenye upendo, Rais msikivu wa awamu ya sita. Mwisho wa kunukuu

Kwa usikivu wa mheshimiwa rais dkt samia,

Naendelea kufunga na kufanya maombi ili mwenyezi mungu amguse mheshimiwa rais dkt samia katika hali ya kipekee kabisa amguse ili aweze kuniona na kuielewa nia yangu thabiti iliyopo ndani yangu ya kuweka alama kubwa ndani ya ccm itakayokumbukwa vizazi hata vizazi.

Mheshimiwa rais dkt samia suluhu hassan, Nakumbuka tarehe 10/06/2022 Katika hafla ya ufunguzi wa msikiti wa jami'ul istiqaama huko bukoba kagera Alisema Mwenyezi mungu ametuambia kwenye vitabu vyake (vitakatifu na vitukufu)

Quran inasema Mwenyezi mungu ametuambia niombeni (nami ) nitawajibu. Twende tukaombe na mwenyezi mungu si mchache wa kujibu. Atatujibu, Pia kwenye biblia kuna aya inayosema;

Ombeni mtapewa.
Bisheni hodi mtafunguliwa.
Kwa hiyo nasi (twendeni) tukaombe ( mbele ya mwenyezi mungu).
Tumuombe mwenyezi mungu atushushie neema na baraka zake.
Hivyo basi kila mmoja wetu kwa imani yake

Hatuna budi kumuomba mwenyezi mungu mara kwa mara na kwa unyenyekevu mkubwa usiku na mchana ili (mwenyezi mungu) aweze kutukidhia haja zetu mbali mbali na kutuepusha na majanga ya dunia. Mwisho wa kunukuu

Nimezuiliwa saana. Nimepuuzwa sana. Naamini sasa kwa dua hizi naona mbigu zikimimina baraka nakwenda kuitwa ikulu ili kuongea na mheshimiwa rais dkt samia kuhusu kukiimarisha chama ngazi za huku chini.

Apostle deonis mutalemwa bushir wa kanisa la ACG nakumbuka tarehe 28/09/2021 akitoa mahubiri alisema (wagalatia 1:20) na hayo niliyo waandikia, angalieni Mbele za mungu Sisemi uongo. Mwisho wa kunukuu

Nikashtuka kutoka ndotoni nilipokuwa naota huku nikiwa nimeikunja miguu huku nikisema huu ndiyo wakati muafaka wa kukiimarisha chama ngani za huku chini kabisa kwa vitendo.

Kidumu chama cha mapinduzi.

Mathias Mugerwa Kahinga
 
Mkishatumia hivyo vilevi vyenu visivyokuwa na viwango mnasumbua sana humu jamvini, JF imeingiliwa kweli na viwavi jeshi.
 
ephen_ vipi jamaa amekuja kivingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…