Wapo Baadhi ya Viongozi Walio Wengi Wasio Stahili Kuwa na Vyeo
Wapo baadhi ya viongozi wengi wasio stahili kuwa na vyeo. Ndio walio vikalia vyeo vya kumuinua fukara. Itakuwa miujiza kwa fukara kuwa na maisha bora.
Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho nikiunguruma kama simba kuwapinga wale wote wenye vyeo walioapa kuihifadhi, kuilinda, na kutetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 2005, ikiwa ni pamoja na sheria zingine ndani ya nchi.
Watu wanatoa rushwa na inakuwa ni dhahiri, lakini watoa rushwa hao kununua vyeo wanalindwa kwa nguvu zote. Tumesahau kwamba tuliapa kutokuwa wabaguzi wala wapendeleaji. Watu wanapeana vyeo kiswahiba na sio kiuwezo wa kutenda kazi. Wanakula vinono na wao ndio wenye hasira kali kuliko mtu yule mwenye maisha ya dhiki tangu uhuru.
Tunatamka kulisaidia bara la Afrika huku tukiwa tu sisi tunao ongea lugha moja hatujasaidiana. Ubunifu tunao lakini watu hawatusaidii kwa hofu ya kwamba tukifanya vizuri wao watapoteza vyeo wavipendavyo kwa ajili ya kuvifanyia matanuzi. Hawana huruma kabisa.
Mfano miongoni mwetu, watu wamepata vyeo kutokana na wanavosema mafukara, ila kwa sasa wamewatema hao mafukara hadi nyakati za uchaguzi ndio watawaona tena kuwa na maana na sio sasa.
Nakumbuka kuna nyakati Pastor Sunbella Kyando wa The Reality of Christ Church alisema, "Saa nyingine mtu unaangalia kwenye eneo la siasa, machozi yanakutoka. Kuna wakati mwingine kuna vitu hatukutakiwa kuomba, kwa sababu tunaomba kwa sababu kuna watu walitakiwa wakae kwenye hayo maeneo (ya siasa) na hawajakaa, na inatugharimu kuanza kumuomba Mungu rehema. Lakini laiti tunge simamisha watu ambao wamekaa kwenye ufalme (watu hao) wangefanya vinavyotakiwa kufanyika."
Mwisho wa kunukuu.
Utaona baadhi ya viongozi wakijinasibu kama watu wanaomjuwa Mwenyezi, lakini matendo yao yako kinyume kabisa. Ni kama wamevaa ngozi ya mwanakondoo huku wao wakiwa ni mbwa mwitu. Hawana msaada hata kwa mawazo mema yanayoweza kuinua hali za wanavosema mafukara.
Nimebuni miradi tele. Nimehangaika huu ni mwaka wa 15. Nina kiu ya kuacha alama ndani ya jamii. Mimi sisikilizwi, ila machawa wakiongelea mambo yasiyo ya maana wanapongezwa na kuitwa wakale kwenye mahoteli makubwa.
Tumefika mahali ambapo mtu akitamka neno Mwenyezi Mungu tu, basi anaonekana kama ni mcha Mungu kumbe ni mnyambilisi. Hana msaada wowote kwa mafukara zaidi ya kuwatumia kwa maslahi yake binafsi.
Mheshimiwa Philipo Isdor Nzabayanga Mpango, Makamu wa Rais wa Tanzania, nakumbuka tarehe 29/06/2021 katika mkutano wa BAKWATA ufanyikao kila baada ya miaka mitano alisema, "Mimi naamini kwa dhati kabisa, kama watu wakishika mafundisho ya dini zao vizuri (naamini) maovu mengi yatapungua sana. Na ndio maana napenda kurejea ombi langu ninalolitoa mara kwa mara (pale) ninapokutana na viongozi wa dini zote kwamba muisaidie serikali kujenga jamii yenye maadili mema."
Mwisho wa kunukuu.
Uadilifu wa viongozi kwa jamii uko ndani ya viapo vyao na ndani ya miiko ya uongozi. Katika uongozi umchao Mwenyezi Mungu, huwa na masikio makubwa kusikiliza vilio vya watu mafukara, na kiongozi anayelalamikiwa na mafukara kwa kutotenda haki hutolewa.
Sasa hivi kuna vyeo visivyogusika. Mfano, M/kiti wa mtaa, diwani, mbunge. Utakuta watu maeneo baadhi katika ulimwengu wa kiroho mafukara wamewachoka watu fulani na katiba inakataza kubebana ila waovu wanabebwa na kulipwa posho.
Kwa mazingira haya, viongozi wa dini watakuwa hawana la kuamua bali kusubiri huruma za wenye viapo kuchukua hatua.
Padre Dkt Faustine Kamugisha wa Kanisa Kuu la Bukoba, Jimbo la Bukoba, nakumbuka tarehe 27/05/2022 alisema, "Shetani ni mpiga maneno. Anaitwa baba wa uongo. Lakini Yesu anafanya vitu vinaonekana."
Mwisho wa kunukuu.
Watu wamekuwa wabaya. Wanajisikia kumuumiza fukara na mtumishi wa umma huku watu wenye vinasaba nao wakiwa wanalalamikiwa na mafukara na hakuna hatua zinazochukuliwa.
Mheshimiwa Mwanaidi Ally Khamis, akiwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalumu, nakumbuka tarehe 27/05/2022 alisema, "Tatizo letu tumekuwa waoga wananchi. Hata sijui tunatishwa na kitu gani ambacho kinatupa hofu tusiweze kuyaeleza yale mambo ambayo yanatokea katika mitaa yetu."
Mwisho wa kunukuu.
Ujasiri wa kusema tunao na wala sisi sio waoga ila kama unasema halafu hakuna hatua zinazochukuliwa, maana yake sisi wasemaji tunafitinishwa na hao tuwasemao wasiochukuliwa hatua.
Mfano tu huko Nkiwanzeeezaa kuna diwani wananchi wanamlalamikia kwa kuwabaka mabinti wa shule za msingi na sekondari katika ulimwengu wa kiroho, kuwabaka mabinti na kuwaonyesha wapambe zake katika ulimwengu wa kiroho, kuuza madawa ya kulevya katika ulimwengu wa kiroho, kutembea hovyo hovyo kama kuku wa mdondo na wake za watu katika ulimwengu wa kiroho, kuwadhulumu mayatima nyumba katika ulimwengu wa kiroho, kudanganya chama kwa kutoa taarifa za uongo ili apate cheo, kupata udiwani kinyume na matakwa ya katiba ya chama katika ulimwengu wa kiroho, na mengine mengi lukuki ya hovyo ikiwa na kutokusoma mapato na matumizi maeneo yote aliyowahi kuwa kiongozi tokea kuzaliwa kwake katika ulimwengu wa kiroho.
Ajabu na kweli, bado diwani huyu yuko madarakani. Kwa hali hii, watu wasemeje katika ulimwengu wa kiroho?
Diwani amefika mahala anaogopa. Hawezi tena kuitisha mkutano wa hadhara kwa hofu ya kuzomewa na kudhalilika kwa jinsi alivyochokwa na wananchi.
Mheshimiwa Albert John Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar, nakumbuka tarehe 21/11/2023 alisema, "Sisi viongozi aliotuteuwa (Mheshimiwa Rais kumsaidia kazi), tukifanya vitu vya hovyo na watumishi wenzetu, (tujuwe) wananchi wanamchukia Rais aliyetuteuwa sisi. Tukifanya matendo mema, matendo ya huruma, matendo yanayogusa watu (inakuwa) ni sifa kwa Rais wetu."
Mwisho wa kunukuu.
Tuonyeshe sifa njema kwa Rais kwa kuchukua hatua kwa mujibu wa viapo vyetu na kwa kuizingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, toleo la 2005, ibara 34(4), ibara 35(1), ibara 26 yote, na ibara 9 a, b, f, h.
Shekhe Walid Alhad Kawambwa, Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akitoa mawaidha tarehe 13/03/2023 alisema, "Vyeo hivi vinaharibu watu hasa ikiwa ulikuwa unavitaka tangu zamani. Kuna watu wamepagawa kwa mazoea mazoea tu kisha Mungu akawaonja, akawapa madaraka. Wao wenyewe hawakujua kama ule ni mtihani. Wakapiga mbizi katika bahari ya kujitahidi, lakini wakatoka katika bahari hiyo hawakulowa hata tone moja."
Maneno haya yanataka darsa ndefu wakati hatuna. Mwisho wa kunukuu.
Nakumbuka tarehe 21/11/2023, Mheshimiwa Albert John Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema, "Wananchi na ninyi iko siku pia mtanielewa vizuri, kwamba Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Mkoa wa aina gani. Kwanza napenda uwazi, halafu nachukia ubabaishaji, na ninaweza nikakukurupukia hadharani bila hata haya kwa umri wako, kwa umbile lako, na kwa umbo lako. Kwa hiyo nikisikia mahali kuna ubabaishaji, kuna rushwa zisizoangalia haki za watu, hakuna commitment, watu wanakuwa hawana huruma, inakuwa ni mbaya. Mimi kwenye mazingira kama hayo
Tumuunge Mkono Mheshimiwa Rais kwenye Vita vya Kupambana na:
Hasa ujinga, tukiuchekea utatuangamiza. Tumeishajua ujinga ni adui, tusiuchekee chekee.
Mheshimiwa sana, kiongozi mstaafu, mkuu wa majeshi mstaafu, mwenye hofu ya Mungu kwa vitendo, mcha Mungu wa kweli, Mheshimiwa Venance Salvatory Mabeyo, akifanya mahojiano katika eneo la Itega - Dodoma alisema:
"Adui huwezi kumchekea. Si ndiyo? Basi, adui ukimchekea chekea atakumaliza wewe kabla hujammaliza."
Mwisho wa kunukuu.
Tuache kuwachekea maadui. Wanatumaliza kifikra mpaka baadhi yetu hatuonyeshi heshima kwa katiba, kanuni, miongozo na taratibu.
Naye Shekhe Walid Alhad Kawambwa, Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akitoa mawaidha tarehe 13/03/2023 alisema:
"Basi nimeona nimalize kwa maneno hayo."
Mwisho wa kunukuu.
Nikashtuka kutoka ndotoni nilipokuwa naota, nikiwa mwili umeishiwa nguvu huku nikisema blabla hazifai. Kila kiongozi anaposema asimamie kauli zake zifanyike kwa vitendo, ikiwemo kuchukua hatua kwa vitendo.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mathias Mugerwa Kahinga