UPDATES: Elimu kwa umma ambayo ni jambo la msingi na endelevu
Nilisikika huko Ndotoni nikiunguruma Kama Simba katika Ulimwengu wa kiroho baada ya kujikuta Niko China nikapewa pombe yenye kimzizi ndani ya chupa Akili ikafa ganzi nikaanzaa kuropoka

Nakumbuka Tarehe 13/03/2022 Makamu wa Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isdor Nzabayanga Mpango Katika Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya huko Dodoma Alisema. Mjenge tabia ya kujiongezea maarifa kwa namna mbalimbali ikiwemo Matumizi ya Mitandao.

Internet Kuna maarifa huko Someni Vitabu Someni taarifa mbalimbali Mwisho wa kunukuu. Nakumbuka Tarehe 14/08/2023 Mchungaji Mwl Aliko wa Dorcas Mwalulili Wa huduma ya Uhuru wa Kristo kwa Mataifa yote wa huko Dodoma Akitoa mahubiri alisema

Ukiona unaota ndoto unaona , maana yake Mungu amekupa neema ya kujuwa. Unapoamka mshukuru Mungu
Ahsante (Mungu ) kwa kunipa kuota hii ndoto. Kwa sababu nimejuwa hila za adui. Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Jenerali Ulimwengu Ex Mbunge Katika hafla ya kumuenzi Hayati Seif Sharif Hamad
Nakumbuka Tarehe 27/112023 alisema (Kuna Mwanafalsafa aliwahi kusema)

Maneno wakati Mwingine lazima yawe kidogo Yana (Maudhi) Yaudhi kidogo Kwa sababu haya maneno wakati Mwingine inabidi yawe ni silaha za kuwafanya wasio fikiri, Wafikiri kidogo. Mwisho wa kunukuu.

Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 12(1)(2) , ibara 13(1)(4)(5) ibara 3(1) uk 13 paragraph ya Kwanza ikisomwa kwa Pamoja na ibara 09 a b f na h kwa msisitizo. Katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara5(8)(9)(11)(16) Ilani ya CCM uk 01 ibara 04 na uk 161-168 ikisomwa kwa Pamoja na ibara 10 na 11 kwa msisitizo.

Watanzania tulio wengi hasa Viongozi baadhi Tumetokea familia Duni ambazo zilikosa lishe. Madhara ya kukosa lishe yametupelekea kuwa na Mijitu baadhi ya hovyo kabisa ndani ya nchi yetu. Jitu limesoma Lina Elimu ya Chuo. Ila hata ujaribu kulielimisha Halielewi kabisa. Ukichunguza unagundua lilikosa lishe utotoni.

Chama Cha Mapinduzi kimeliona Tatizo hili Ndiyo maana chama kikaingia mkataba na Wananchi ili kipewe jukumu la kusumamia lishe ili Jamii iweze kuwa na watu wenye Tija ndani ya Taifa. Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania. Dkt Philip Isdor Nzabayanga Mpango Katika Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya huko Dodoma

Nakumbuka Tarehe 13/03/2022 Alisema (Watumishi wa Umma) mkumbuke kurejea (na kuvifanyia kazi) Ahadi zilizomo katika ilani ya Chama Tawala CCM. Mwisho wa kunukuu.

Tusome ilani ya CCM 2020 uk 298 ibara 251 Kisha tusome uk 04-05 ibara 07 ili kupata uhalali wa kwenda kusoma ilani ya CCM 2015 uk (i) ibara 01 ikisomwa kwa Pamoja na ibara 177 uk 230 ndipo tutoke turudi kwenye ilani ya CCM 2020 uk 139 ibara 85, uk 142 ibara 89 zote zikisomwa kwa Pamoja na uk 08 ibara 10 na 11.

Lishe Bora ni muhimu katika kuhakikisha Taifa linakuwa na Jamii yenye nguvu kazi imara na uwezo mkubwa wa kuelewa na kukabiliana na Mazingira yake. Shekhe Muharam Rashid Mziwanda. Akitoa Mawaidha Tarehe 20/11/2023 Alisema Watu wengine inawezekana mnapata nao taabu saana (kuwaelimisha) Mnahisi (labda) hawajasoma (Au mtu Mwingine) Hana adabu Hana Nini ...(lishe) Kumbe Hali Matunda. Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya 06 ya Mkataba wa lishe September 30 , 2022 Alisema (Hii Hali ya Kutokuzingatia lishe) maanake Nini !?
Maanake hatujielewi, Si Ndiyo !?

Wala hatujuwi thamani ya vitu ambavyo Mungu ametuumba navyo. Mwisho wa kunukuu
Tuzingatie lishe ili itutoe kwenye janga la kuwa na watu ambao wamedumaa akili na kupelekea kufanya Mambo ya hovyo hadharani bila kujali kuwa anayoyafanya Yana mdhalilisha mbele ya Jamii. Mfano
Tumeshuhudia Diwani katika Ulimwengu wa kiroho asiyekuwa na Elimu Mwenye changamoto ya Udumavu wa akili wa kata ya Nkiwanzeeezaa akijihusisha na Mambo ya hovyo kiasi kwamba unaweza kudhani hakuapishwa kuilinda kuihifadhi na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005.

Kisha huko huko katika Ulimwengu wa kiroho tukaliona lisomi lenye historia ya kujihusisha na Mapenzi ya jinsia moja likiwa ndilo limama , lipenda vyeo. Na jitu la kukisusa Chama likisimama kumtetea Diwani huko Nkiwanzeeezaa ambaye ananuka kiasi kwamba Diwani Huyo anaogopa hata kuitisha Mkutano wa hadhara kwa hofu ya kuzomewa au kupigwa mawe kabisa.

Udumavu wa akili unaaibisha Unaweza liona lijitu limevaa suti Limeweka poozi Ukiliuliza kitu linaonekana Kama Lina dharau, Au Lina jeuri Au unaweza kujuwa halitaki kuongea na wewe kumbe limekosa lishe
Unalielimisha halielewi. Hata Kama limeapa utaona jitu lenye Udumavu wa afya ya akili linafanya Mambo hadharani yaliyo Kinyume kabisa na viapo lilivyo viapa.

Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya 06 ya Mkataba wa lishe September 30, 2022. Alisema Ndiyo Yale aliyoyasema nadhani Waziri Ummy, Tunagombana huko TAMISEMI
Huko Chini Hata huku juu Serikalini. Unamueleza mtu kitu (chenye manufaa kwa Taifa) Mara nne
Mara tano Hata hakimuingii Unauliza , Dharau? Jeuri!? (Au)hutaki?

Kumbe Masikini hujuwi historia yake (huko siku za nyuma). Historia yake imefichwa na suti na Tai aliyoivaa.
Inawezekana kabisa. Maanake unasema (Kisha unajisemesha wewe mwenyewe) Ahaa, Mbona Mi naona hapa Kuna tatizo!? Naona (Matatizo) moja, mbili, tatu. Hivi inakuwaje!? Huyu niliyemuamini hapa (hivi kweli yeye haoni?) Haoni!? Haiwezekani. Kumbe Kuna hayo (ya kukosa lishe na uelewa mdogo) Tuna watu lakini sio Raslimali watu.

Maandiko ni mengi, Ni mazuri Lakini hatufanyi vile tunavyo andika na kufanya. Mwisho wa kunukuu
Yaliyotokea yametokea. Bado tunayo nafasi ya kuangalia wale wote wanao semeka vibaya ndani ya Jamii tuwatoe. Tuondoe Muhali wa kubebana kwa historia za Koo fulani.

Pili tujikite Sasa katika kuwapatia lishe Bora wanetu ili kulipunguzia Taifa mzigo wa kuwa na watu wengi Walio na Udumavu kiakili wenye kuapa viapo na Kisha kuishi Kinyume na viapo vyenyewe wakiwa wanabebana na kupendeleana mchana kweupe huku Chuki binafsi zao wakizielekeza kwa Watumishi wa Umma na Mafukara kuwahukumu kisheria na kuwalinda watu wenye vinasaba nao Kama vile Diwani wa Nkiwanzeeezaa Mwenye tabia chafu aliyechokwa na raia wote huku alitumia jitu somi kumtetea na somi lenyewe la huko Nkiwanzeeezaa katiba Ulimwengu wa kiroho likiwa na kashfa za kujihusisha na Mapenzi ya jinsia moja na lenyewe likiwa limama kwenye mahusiano hayo Kama tunavyoona katika Ulimwengu wa kiroho.

Sisi tulio katika Ulimwengu wa kiroho tunayafyekelea kule majitu Kama haya yaliyokosa lishe na kuanza kuwadhuru Mafukara. Mchungaji Jonas Singo Wa Mahubiri TV Anasema katika Mahubiri yake Tunazungumza katika Ulimwengu wa kiroho Na katika Vita ya kiroho ni Vita isiyoonekana. Ni Ulimwengu usio shikika ingawaje matkeo yake yanaweza yakashikika. Yanaweza yakaonekana. Mwisho wa kunukuu

Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 19 (1)(2) ibara 18(a) na ibara 8(d) kwa mazingatio ya ibara 9 a,b,f,h. Tupambane na Udumavu wa afya ya akili. Tukishikamana tunaweza.
Tuanze na wanetu Sasa ili wasidumae akili wakaja nao kuwa wanaapa na Kisha kuishi Kinyume na Matakwa ya viapo. Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Katika Uzinduzi wa Report ya utafiti wa afya ya uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya Mwaka 2022 Mheshimiwa Rais alisema Suala la Udumavu lichukuliwe kwa uzito mkubwa.

Hili ni suala la Ustawi wa Jamii Na ni suala la Usalama wa nchi. Miongoni mwa athari za muda mrefu za Udumavu ni kupunguza uwezo wa watoto kujifunza. Kuongeza hatari za kupata changamoto za kiafya ukubwani na hivyo kuathiri nguvu kazi ya Taifa letu. Ndiyo maana ninasisitiza umakini kwenye lishe ya Watoto.

(Tusipopambana na Udumavu) tutakuja kukuta Taifa hapa robo, thelusi nzima ya watu hawaeleweki eleweki
Udumavu unazuilika.

Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka kutoka katika Ulimwengu wa kiroho huko Ndotoni nifoka foka watoeni Viongozi wenye viashiria vya Udumavu wa afya ya akili na wenye viashiria vya kujihusisha na mapenzi ya jisia moja.
Wanaliletea Taifa letu laana.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Mathias Mugerwa Kahinga

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🔨🔨💪🏿💪🏿💪🏿
Kipenzi chetu Imam Hussein aliuwawa kikatili sana Karbala ili kulinda na kuutetea uislamu. Nasi Allah katupa Tawfiq. Lakini cha kuhuzunisha Sunni hawamuenzi Imam wetu wanamdhihaki kumtukana nakutudhihaki.

Allah mwenyez Mungu mwingi wa rehma ampe qaul thabeet kipenzi chetu Imam.
 
POLISI KATA WASHIRIKI KILA KIKAO NDANI YA KATA PASIFANYIKE VIKAO BILA UWEPO WA POLICE KATA HAWA NDIYO WASIMAMIZI WA HAKI ZA MAFUKARA

Nilisikika hivi hivi tu katika Ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikiwa natokwa povuNikaanzaWanyonge walio wengi wanaweka imani zao kwa MadiwaniIla Baadhi ya Madiwani sio watu wazuriNi wabinafsiWenye kutanguliza Maslahi binafsi mbele.

Kwa kuzingatia ya kuwa Mheshimiwa Rais ndiye Amiri Jeshi MkuuNa kwa kuzingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatukataza Ubaguzi wa Aina yeyote ibara 13(5) NI vema Sasa kutambuwa uwepo wa Police kata ndani ya kata ili asaidie kuthibiti Kodi za Mafukara ziache kuhujumiwa na Baadhi ya Viongozi walafi wenye Matumbo pakacha yasiyo jaa majiNampongeza Mwl Mkuu na Uongozi wote kwa Ujumla wa shule ya Olyimpio Primary schoolNilihudhuria Mkutano pale Niliona Maafisa wa Police wakipewa heshima ndani ya kata ile.

Nikaangangalia kata yangu Sidhani Kama Police kata Kama kapewa hata walau Ofisi kwa kuzingatia umuhimu wake katika Jamii.

Kwa kuzingatia nchi yetu inafuata Utawala Bora na Police wanalo jukumu la kusimamia Sheria na Usalama wa watu , nilitamani kila Mkutano nione Police Kata akiheshimiwa na kupewa Dakika zake kuinyoosha kata .

Nilitamani Police kata awe Mtu huru anayesoma Mifumo na kuifanyia kazi pasipo Maelekezo mengine pengine yaliyo nje ya Mifumo ya nchi

Nilitamani Police kata awe Mdau kwenye Kamati ya Maendeleo ya kata kikao kinapoanza mpaka mwisho na sio kufikia maeneno ya fedha labda aambiwe atoke ili watu wapange ubadhilifu.

Watumishi wa Vyombo vya Usalama Rais wetu ndiyo Amiri Jeshi Mkuu wao .

Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 35(1)Ni Watumishi wa Umma .

Tunaomba wasitengwe kikao chochote Cha Maendeleo ndani ya kata kwani watasaidia kulinda fedha za Mafukara. Sheria za kusafurahisha Madiwani za hovyo zisiwepo.

Nikashtuka katika Ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikiwa kimya

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Mathias Mugerwa Kahinga
🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Wakishiriki vikao ndio pona yenu hiyo, lakini hivihivi kuna siku mtakuja kupigwa na raia wenye hasira kali.
 
KIONGOZI MCHA MUNGU ANA USO WA AIBU WA KUSIMAMA HADHARANI
KUFANYA MATENDO YA HOVYO YALIYO KINYUME NA VIAPO VYAKE KWA UMMA
NI KIONGOZI WA KIIBILISI TU NDIYE ASIYE NA AIBU WALA HAYA.

Nilisikika katika Ulimwengu wa kiroho nikitema cheche huko ndotoni kukemea tabia za Baadhi ya Viongozi kuwafanya Mazamwamwa watu walio waamini na kuwapa ridhaa ya kuwaongoza kwa kuwaapisha
Nikaanza
Nakumbuka Tarehe 01/08/2024
Rev Dkt Eliona Kimaro
Wa Kanisa la KKKT Kijitonyama
Akitoa mahubiri
Alisema
Ana kheri Mtu yule anayekuambia juu ya neno kuliko anayekupa fedha
Anayekupa fedha amekufanya Mtumwa
Amesababisha mawazo yako yasipanuke
Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Majengo ya Kampasi Chuo Cha Mzumbe huko Maekani
Nakumbuka Tarehe 04/08/2024
Alisema
Nimekuja na zawadi ya maneno
Lakini nataka muyaamini Maneno yangu .
Mwisho wa kunukuu
Watanzania tunayaamini Maneno yako Mheshimiwa Rais Dkt Samia ila huku chini Kuna watu wametengeneza ngome ya kulindana katika maovu
Tueleze tu Mheshimiwa Rais
Nakumbuka Tarehe 15/09/2021
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Siku ya Maadhimisho ya Demokrasia Duniani
Alisema
Nchi yetu pia inaongozwa kwa Mujibu wa Sheria ambapo hakuna mtu aliye juu ya Sheria.
Kila mtu ana haki sawa mbele ya Sheria
Ukivunja Sheria
Basi utashughulikiwa Kama Sheria zinavyosema
Haichagui ni Nani
Yeyote yule
Mwisho wa kunukuu
Naye Comrade Daniel Godfrey Chongolo
Akiwa Katibu Mkuu CCM Taifa
Katika kilele Cha Matembezi ya Uvccm Paje huko Zanzibar
Alisema neno
Tutafuata Sheria , Taratibu na Miongozo yote iliyowekwa na Serikali
Eneo hili ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020-2025
Kwani tumeahidi kuhakikisha haki za Raia wetu zinalindwa.
Na asitokee mtu (Mwingine) kumuonea mtu Mwingine.
Mwisho wa kunukuu
Ndani ya nchi maeneo Fulani watu tunalalamika
Kuwalalamikia Baadhi ya Viongozi lakini hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa
Watu wanachukulia Uelewa Mdogo wa Watanzania walio wengi Kama kisa Cha kuwadhulmu haki zao za Msingi huku wakificha Ukweli wa kuwahimiza watu kusoma ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu ili kuweza kujuwa haki zao.
Tunaposema Mtanzania asimame kwa ajili ya nchi yake maana yake Mtanzania hapaswi kucheka cheka na Kiongozi Yeyote anayekiuka kiapo na Taratibu ndani ya nchi
Na Huu ndiyo ucha Mungu wa kuipigania nchi.
Kuacha baadhi ya Viongozi waendelee kuwa kwenye vyeo huku wakiwa wamekiuka Mifumo ya nchi ni ushetani uliofichwa kwenye Hali ya kuchekeana chekeana na kuonyeshana Meno meupe huku Roho zikiwa hazimmanishi kuchekeana kule na tabasamu zile.
Tubadilike
Tuwe Waadilifu
Na tuwe waaminifu wenye kujawa hofu ya Mwenyezi Mungu ndani ya mioyo yetu.
Tusome ilani ya CCM 2020 -2025 uk 161-168 na uk 08 ibara 10 na 11
Nakumbuka Tarehe 04/08/2024
Kwa Mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 13(4)(5) na 09 a,b,f na h nasema nikiongozwa na ibara 18(a) na 19(1) kwa Maana ya Uhuru wa mawazo
Bila kuiacha katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 5(8) na ilani ya CCM 2020-2025 ibara 110(c) na ibara 10 na 11 uk 08
Wakili Jasiri na Msomi
Boniface Mwabukusi
Rais wa TLS
Akifanya Mahojiano na Mizani ya Kisiasa
Alisema
Hii tabia ya kukosa Uwajibikaji .
Na Uwajibikaji unakosekana kwa sababu Wanaanchi tumechagua nafasi ya kuwa watumwa na tukawageuza Viongozi wetu ( wa Umma) kuwa Wafalme.
Na Mfalme hafanyi Makosa
Kila anachofanya Mfalme ni hewala
Sahihi
Mwisho wa kunukuu
Ngazi za Matawi, Kata , Jimbo na Wilaya Baadhi Tumekuwa wa Viongozi wenye vinasaba za kifalme wasio sikiliza kauli za Viongozi wakuu wa kitaifa na Matokeo ya wao kuto kuchukuliwa hatua yamepelekea kuwa na Viongozi Baadhi wenye kuiamini Rushwa na kuisujudia Kama Mlinzi wao Mwenye nguvu kiasi kwamba hata wakisigina vipi Kanuni Miongozo na Taratibu zote , kwa kutumia Rushwa hubaki salama kana kwamba watu wanao waongoza ni Watu waliofariki huku wakiwa na mionekano Kama wako hai ila wamepoteza Uelewa .
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe
Mheshimiwa Nicodemus Maganga
Akiwa kwenye Baraza la Madiwani huko Mbogwe
Alisema
Mimi Sio Mnafiki
Lazima hapa niwe Mkweli
Mwisho wa kunukuu
Kubebana
Na kuinjiniana kupeana vyeo
Kwa kuangalia Koo za watu
Uswahiba
Urafiki
Na Muhali ni Ujinga Bobevu ambao upo Kinyume na Viapo vya Viongozi
Taabu ya Watanzania
Tulio wengi
Tumezingirwa na hofu ya kuhoji
Huku tukijipa hope ya kuwa Mtoto wa Simba ni Simba
Kumbe Kuna nyakati Kuna Mapepo na Mitoto itokanayo na Dawa za kishirikina za Waganga wa kienyeji hujitwalia vyeo ili kuwatesa watu Wa Mwenyezi Mungu walio wengi .
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka Tarehe 03/01/2023
Akiongea na Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa huko Ikulu Dar es salaam
Alisema
Tunajenga upya Taifa letu lisimame liwe Taifa la Watanzania
Taifa la Watanzania
Watanzania wenye kuamini kwenye Mambo Yao.
Watanzania wenye kujuwa kwamba hii nchi NI yetu ( sote)
Na wenye kusimama kwa ajili ya nchi Yao.
Popote pale Duniani.
Akisimama Kama Mtanzania , atasimama kwa ajili ya nchi yake.
Na hatasimama kwa ajili ya chochote kile.
Bali nchi yake.
Huko ndiko Mwenyezi Mungu amenielekeza ( waja wake) tuelekee
Na ni imani yangu kwamba wenzangu mtaniunga mkono( ili) tuendelee huko
Mwisho wa kunukuu
Tunapoteza muda kushabikia mipira huku tukiwa hatuna muda wa kusoma maandiko Matakatifu kwa imani zetu ili yatuongoze kusa Majasiri wa kukataa tabia za kijinga pale zinapoibuka .
Kila Uongozi Wa Umma una Miiko yake ya kikanuni
Twawezaje Kujenga hoja kwa miiko tuyoijuwa !?!?
Ni lazima tujisomee ili tuweze kuchukuwa hatua pale tunapobaini Mifumo inapindwa kwa sababu za Maslahi binafsi
Tunao Baadhi ya Viongozi Makafir wasiotii viapo na Taratibu zetu , tumewachekea wametufikisha hapa tulipo tulio wengi tukiwa Omba omba na Wala hawana hata Ndoto za kutuinua Zaidi ya kupanga safu za Uongozi huku wakila na kunywa vizuri wao na vibararaka na. Vijijibwa vyao huku tulio wengi tuhaha walau kupata makombo tule tuishi.
Huu ni ukafir mkubwa wa kutangaza kusikiliza watu huku tukiwa hatuna Nia hiyo.
Huu sio ucha Mungu
Ni Ukafiri uliozingirwa na uoga wa kuisema kweli Kama ilivyo
Shekhe Hillali Kipozeo
Akitoa Mawaidha
Nakumbuka Tarehe 15/09/2013
Alisema
Makafir ni (watu ) wale wanaompinga kumpinga Mwenyezi Mungu na kuwapinga Manabii wa Mwenyezi Mungu
Hao ndiyo wanaitwa Makafir
Hao ndiyo Makafir Shekhe
Usiwatafute
( Ukawa unajisemea) hao Makafir hao wa Ukoo gani !?
Watu gani hao !?
Ni hao
Usiwatafute Makafir wako wapi Shekhe
Makafir tunao
Tena wengine Marafiki zetu bhana.
Maana ya Ukafiri ni kupinga tu
Mwisho wa kunukuu
Mnaopinga ilani , katiba ya nchi, katiba ya CCM , Kanuni mnazipinda , Miongozo mnaipinda,
Hamna Nidhamu kwa kauli za Viongozi wetu Wakuu wa nchi
Mnao yafanya hayo Ninyi ndiyo Makafiri wenyewe mliokula kiapo kumtii Mwenyezi Mungu kumbe mkiwa mmevaa ngozi ya Mwanakondoo huku mkiwa. mbwa mwitu .
Tusome Mwongozo wa CCM 1981 uk 104 ibara 110 uk 138-139 ibara 159
uk 46 ibara 59 kwa msisitizo
Ilani ya CCM 2020 ibara 04 uk 01 na uk 08 ibara 10 na 11
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Akizindua Kampeni ya Tupendane
Akiwa Mnvomero Mkoani Morogoro
Nakumbuka Tarehe 03/08/2024
Alisema
Sheria lazima zifuate Mkondo wake
Mwisho wa kunukuu
Mwenyezi Mungu kwenye biblia anatueleza Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa Maarifa
Hatuna Maarifa ya Mifumo ya nchi iliyotupelekea hata kuwa watu wa kujichekesha na kushangilia chochote popote Baadhi ya Viongozi wanazisikigina Sheria na kukiuka Viapo vyao.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka Tarehe 03/08/2024
Alisema
Kwa hiyo niwaombe saana ndugu Zangu Wanaanchi wote ,
Tuishi kwa salama ,
Na katiba yetu Ina Maelekezo
Yanayo jitosheleza.
Mwisho wa kunukuu
Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1)(2) ibara 09 a,b,f na h ibara 12(1)(2) ibara 13(1).
Pia hatuna Maarifa ya Maandiko ya Mwenyezi Mungu
Ndiyo Maana tunaburuzwa
Kushoto kulia
Kulia kushoto
Nasi hatupinduki
Tunacheka cheka utadhani tunafanyiwa hisani kumbe watu wanatuumiza
Tubadilike.
Nakumbuka Tarehe 05/08/2024
Mheshimiwa Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan
Akiwa Ruaha
Alisema
Tubadilike na tujenge nchi yetu
Si ndiyo !?!?
Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka katika Ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikiwa kimya kabisa .

Kidumu Chama Cha Mapinduzi



Mathias Mugerwa Kahinga
 
Hatuwataki viongozi watokanao na maelekezo ya vijimiungu watu hatuwataki.

Tunawahitaji viongozi watokanao na sisi tulio sota nao. wenye kujuwa ilani , katiba kanuni miongozo na taratibu za chama. Hatutaki kupelekwa pelekwa kama gari bovu hatutaki

NCHI HII NI YETU SOTE

Nilisikika hivi hivi nikiuwasha Moto wa Neuclear huko katika Ulimwengu wa kiroho huko ndotoni kukemea Tabia za kijinga zisizo na uzalendo kwa nchi bali zenye harufu Kali za Rushwa ya kunuka uvundo Nikaanza kuuwasha.

Nakumbuka Tarehe 07/08/2024 SACP Jumanne Muliro Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam
Alisema.

Jeshi la Police litaendelea kuheshimu katiba kwa watu wanao tumia vizuri haki Yao ya kikatiba ya kutoa maoni lakini maoni ambayo yanakwenda sambamba na Sheria na hayakinzani na Sheria au ibara hiyo ya Maoni haitumiki vibaya kwa kupotosha Umma au Jamii na kutoa taarifa ambazo zinajenga Taharuki.

Mwisho wa kunukuu

Mtu ukitaka kuwa Polisi lazima ujuwe unalo jukumu la kuitumikia nchi kwa Uadilifu na Uaminifu Ili kutimiza azma hii.

Polisi anatakiwa kujuwa Katiba ndiyo Sheria Mama nchini. Polisi anapaswa kujuwa Jeshi la Polisi limeundwa kwa Mujibu wa Sheria.

The Police force and Auxiliary Act ambayo inatakiwa kutiiwa Police anapaswa kujuwa Police General Oders inaelekeza Nini kwenye majukumu yake.

Sheria ya Polisi Wasaidizi inasemaje Ilani ya Chama kilichoko Madarakani inasemaje

Je Sheria zingine ndani ya nchi zinaelekezaje kwa Mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1)(2) na ibara 09 a,b,f na h Ibara 12(1)(2) na ibara 13(1)(4)(5) na ibara 08(1) a,b,c, d

Polisi akiyajuwa haya Walau kwa kiasi Fulani, kazi ya Upolisi inampelekea kuifanya kwa mwelekeo wa Uadilifu na Uaminifu.

Ni vigumu mtu kuokotwa from no where Kisha akafanywa police wakutegemewa kuisaifia Jamii
Ikifanyika hivyo itakuwa ni Usanii wa kisinema sinema.

Vivyo hivyo kwa Wanasiasa Nchi yetu ina mifumo ambayo ni lazima ifuatwe ambayo mifumo hiyo inakataza Vitendo vya Kibaguzi na Upendeleo

Mwanasiasa ataitwa Mwanasiasa wa kweli Asiyekuwa Chawa kwa kielewa Katiba ya nchi. Mwanasiasa lazima aielewe Sheria iliyounda vyama ya siasa The Political parties act aisome na aiishi.

Kisha arudi kwenye Ilani , katiba yake ya Chama , Kanuni , Miongozo na Taratibu. Aisome Ahiishi
Na kuitii. Huyu ndiye Mwanasiasa Asiyekuwa Chawa

Mwanasiasa lazima aelewe ya kuwa Ilani ndiyo Mkataba wa kuheshimiwa na kutiiwa kwani ni Makubaliano Kati ya Chama na Jamii husika ya namna ya ktekeleza Mambo kwa kuunda Serikali na kukidhi zile ahadi zilizomo ndani ya Ilani.

Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 5(4) ili kwenda kusoma Kitabu Cha Binaadamu na Maendeleo Cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uk 17-21 Mwongozo wa CCM 1981 uk 103 -105 Kwa Msisitizo itoshe tu kusema.

Ndani ya Chama Kuna watu wanavunja Mifumo ya Chama wanalindwa na Matokeo ya kuwalinda Waovu yametupelekea kuwa na Viongozi wa Chama wenye kuinyooshea vidole Serikali na kuiamuru iwe na Uadilifu huku wanyooshaji hao wakiwa wao wenyewe. Sio watiifu wa Mifumo ya nchi Sio watiifu wa Mifumo ya Chama

Sio watiifu wa maelekezo yaliyotolewa na The Political parties act na Bado wako Madarakani Ndiyo maana tunaanza kushuhudia watu waliovalia nguo Kama Wanachama wakiuza Ofisi ya Chama Kinyume na kanuni na Kisha wanadumu kwenye vyeo huku waovu Hawa tuwategemea kwenye michakato ya kutafuta Viongozi wa kulisaidia Taifa huku wao wakiwa manyang'au yenye Roho Mbaya yasiyo na utii kwa Jamii.

Mheshimiwa Dkt Lameck Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha nakumbuka Tarehe 12/07/2024 Alisema

Mara nyingi Mimi huwa nakamatwa kwenye mtego wa kutumia lugha isiyo na Mafuta . Lakini Ukweli lazima tuambizane mwisho wa kunukuu Wakili Harold Sungusia Ex Rais wa TLSNakumbuka Tarehe 03/08/2024
Alisema Tendeni haki Fanyeni haki Simamieni haki Mwisho wa kunukuu.

Kwa Hali hii twawezaje kusema tunayo Nia njema ya kuiletea Maendeleo nchi yetu. Mijitu Aina hii Baadhi ikimuona Mheshimiwa Rais inajifanya Kama inamkubali huku nyuma ya pazia ikiwa haitekelezi maelekezo ya Mheshimiwa Rais Unafiki Mtupu.

Twawezaje kutembea kifua mbele tukijichekesha chekesha ikiwa Yale anayoyaelekeza Mheshimiwa Rais hatuyafuati na hatuyataki kwa hofu ya kuharibu safu za watu wa hovyo waliowekwa kwenye vyeo na Baadhi ya Wabunge waovu , Madiwani waovu na Wenyeviti wa Mitaa na vitongoji waovu Baadhi ambao Wana sura ya ndege nyakati za mchana huku usiku wakiwa ni Mapopo .

Nimekuwa nikishauri Viongozi wa Juu Pangeni muda shukeni chini ili kwa vyeo vyenu mfanye maamuzi magumu ya kusambaratisha safu za watu Waovu wasiojali ilani katiba Kanuni Miongozo na Taratibu
Tukisambaratisha Mitandao ya uovu baada ya hapo tutaanza Sasa kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais na Viongozi wengine wa Juu kwa utii baada ya kuwa Wasanii ndani ya Chama wasiojuwa lolote kuhusu Chama kuwa wameondolewa kwenye vyeo walivyopata kwa Mipango ya safu.

Naamini Rais wetu ni Msikivu na anakipenda Chama na hivyo atasema neno litakaloleta ukombozi kwa Mafukara na Wanyonge ma voice less Nakumbuka Tarehe 05/08/2024 Mohammad Mchengerwa Waziri wa TAMISEMI Akiongea katika Uwepo wa Rais huko Mlimba - Morogoro Alisema Mheshimiwa Rais ,Wewe Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ndiye Mkombozi wa Makundi yote haya Mbali Mbali katika Jamii . Tumpigie makofi mengi saana kwa Rais wetu .

Mheshimiwa Rais Wewe ni Mtetezi wa Wanyonge Mheshimiwa Rais Wewe ni Msikivu kwa Watanzania wote
Mwisho wa kunukuu

Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 uk 54 ibara 55(1) ibara 57(1) ibara 58
Tusome Kitabu Cha Standing Order for the public service 2009 Pasuant to S. 35(5) of the Republic Service act Chapter 298 uk 13 kifungu B1.

Tunamuomba Sasa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan atupatie neno ili lituokoe
Nakumbuka Tarehe 08/08/2024 Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwenye kilele Cha Maonyesho ya nanenane huko Dodoma Alisema Chagueni Viongozi wanaopenda Maendeleo. Msichague Viongozi wanaopenda Matumbo Yao au nafsi zao. Chagueni Viongozi wanaopenda Maendeleo. Na msikubali kupangiwa Viongozi Mwisho wa kunukuu

Adamu Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Nakumbuka Tarehe 07/08/2024 Alisema Mheshimiwa Rais
Umeacha maelekezo Mbali Mbali Na Sisi na wenzangu wote upande wa Chama na upande wa Serikali tunakuahidi utekelezaji Mwisho wa kunukuu.

Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 21(1)(2) ikisomwa kwa Pamoja na ibara 08(1)(d) uk 17 uk 58 ibara 61 inayosomwa kwa Pamoja na Standing Order for the Public Service 2009 pursuant to S.35(5) of the Republic Service act chapter 298 uk 20 kifungu B.15(1)(3) Kwa angalizo la ibara 35(1) na 34(4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005.

Ngazi zetu za huku chini Bado tunao Viongozi waovu waliovunja Sheria na Kisha kulindwa .
Mfumo wa Chama unaagiza vikao vichakate na watu wa vikao hivyo Baadhi ndiyo wenye kutuhumiwa kwa Rushwa na Mambo yote ya hovyo na ni hao hao ndiyo wenye Chuki dhidi ya watu wasema kweli na wapenda haki .

Kwa msingi Huu Wanaanchi wanaotegemea watu hao wakae vikao na kuwaletea Viongozi wema itawezekanaje? Nishauri tu Viongozi wa Juu Shukeni chini Ongeeni na Wanachama wenye Chama Chao ikiwa kweli tuna Nia njema na kuisaidia nchi na kuyaishi maelekezo ya Rais. Ongeeni na Wanachama

Wasiyemtaka alikalia cheo kwa Rushwa atolewe. Na nyakati za kuelekea Chaguzi Viongozi wanao lalamikiwa kunuka uvundo wa kuto kutenda haki wahamishiwe Mbali au wayolewe ili nafasi zikaimishe kwa watu Waadilifu ili watimize maono ya Mheshimiwa Rais.

Nakumbuka Tarehe 08/08/2024 Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Akiwa nanenane huko Dodoma
Alisema Kama Sisi Wanasiasa tunawapangia Viongozi ili ( kwetu Sisi) iwe ndiyo conduit yetu ya kupita huko mbele .."Kataeni Wekeni wale mnaowajuwa watasimama kwa Maendeleo yenu Watafanya kazi kwa Maendeleo yenu.

Kachagueni watu Madhubuti Watakao simamia Maendeleo yenu. Mwisho wa kunukuu Mheshimiwa Rais watu Madhubuti Wenye kukijuwa Chama na kukiishi. Wasiokula Rushwa Wamejaa tele Ila wako nje ya mfumo wa maamuzi Wasiokijuwa Chama Baadhi Wababaifu Wasiotokana na maelekezo ya Ilani katiba kanuni Miongozo na Taratibu ndiyo Baadhi waliokalia vyeo vya maamuzi na wamejiimarisha kwa Rushwa.

Kwa Hali hii tunaomba Rais useme neno tu japo neno moja tu la nyongeza ili kubomoa mfumo huu usiotenda haki uliojivalisha ngozi ya Mwanakondoo huku ukiwa na mazalia ya Mbu tu.

Dkt Lameck Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha Akiwa katika hafla ya kufunga kikao Cha Tathmini ya Utendaji kazi ya Mamlaka ya Mapato nakumbuka Tarehe 12/07/2024

Kama Mtu mmoja , wawili , watatu, ( watu hao waovu) wamesababisha ( watu wengine) woote tunaanza kutukanwa ( je) wote ( Ninyi) mko tayari nao hao? Kama anatokea ( mtu) anayetanguliza Maslahi yake binafsi anaweka Maslahi ya nchi nyuma , Watu wa Aina hiyo ( ukiwa mkuu wa kitengo) usiwahamishe idara
Ehee wafukuze Wafukuze Nchi hii Ina vijana wengi Wapo tu a ni Wazalendo wangetamani ( na) wanatamani wafanye kazi kwa ufanisi ( kwa kuitii Mifumo) Mwisho wa kunukuu

Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 34(4) na ibara 35(1) huku tukikumbuka kusoma ilani ya CCM 2020 ibara 04 uk 01 uk 161 -168 na Kisha ibara 10 na 11.

Rais Samia Suluhu Hassan Alisema Tarehe 08/08/2024 Kama ilivyo elekezwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Hili ni lengo lililotolewa na ilani ya Uchaguzi. Mwisho wa kunukuu.

Nikashtuka katika Ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikiwa nikiwa nasema Kama nimekukera nenda kasome Mifumo ya nchi na utende kazi Kama mitumo inavyotaka Tumechoka na Usanii Jazz band.

Tuwasaidie Viongozi wakuu wa kitaifa kutimiza Ndoto zao na kuweza kuisaidia nchi ili Mafukara wasiishi Kama fisi aonapo Mkono wa Binaadamu na kuanza kuufatilia kwa matumaini akidhani utaanguka apate msosi.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Mathias Mugerwa Kahinga
 
ELIMU KWA UMMA LIWE NI JAMBO LA MSINGI NA
ENDELEVU
KUTOKA KWA KILA MMOJA WETU
ILI KULINUSURU TAIFA
LISIZIDI
KUANGAMIA.

Nilisikika katika Ulimwengu wa kiroho huko Ndotoni nikiunguruma Kama Simba aliyeshika Windo
Nikaanza
Katika Maisha yetu ya kila siku tunakutana Mara kwa Mara na Baadhi ya watu Wajinga ambao wanao ujasiri wa kuuamini Ujinga wao na kufanya jjtihada za kuueneza Ujinga ule kwa Jamii ili ukubalike kuwa ndiyo mfumo sahihi wa kimaisha.
wanaamini kabisa Ujinga ule unaweza kulisaidia Taifa .
Tunalo jukumu Sasa la kulinyoosha Taifa na kuwapa watu elimu ili wasiendelee kupotoka kwa Ujinga unao zagaa unaopelekea watu kuishi Kama vipofu wakukataa Ukweli na kuukumbati Uongo .
Tumefika Mahala Mtu Mkweli anachukiwa na mtu Muongo anashangiliwa .
Kuna watu ukiwaangalia Wana Mionekano Kama wanaona ila katika Ulimwengu wa kiroho ni vipofu kwani Tayari hawaioni kweli Bali Batili imewawekea wingu machoni mwao.
Pastor Sunbella Kyando
Wa The Reality of Christ Church
Akitoa Mahubiri
Nakumbuka Tarehe 22/09/2021
Alisema
Usipokuwa na Maarifa unakuwa Blind .
Mwisho wa kunukuu.
Katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk 10-11 ibara 15(3)(6), uk07 ibara 12(1)(a) ili kwenda uk 152 vifungu (3)(6)(8)
Yote hii ni kuonyesha ni kwa jinsi gani Elimu inastahili kupewa kipaumbele kwa kuipata na Kisha kuwaelimisha wengine.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka Tarehe 12/August/2022
Akiwahutubia Wananchi katika Uwanja wa Samora -Iringa
Alisema
Ndugu Wananchi , Elimu ni Msingi wa Maisha na Maendeleo kwa kila Taifa.
Mwisho wa kunukuu
Tuielimishe Jamii ielewe mifumo ya nchi
Na tuisisitize Jamii kuitii mifumo huku na Sisi Waelimishaji tukiwa mstari wa mbele kuyatenda hayo tuyaelimishayo kwa Vitendo.
Professor Joyce Ndalichako
Akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi , Ajira , Vijana na watu wenye Ulemavu
Nakumbuka Tarehe
20/07/2022
Alisema
Masuala ambayo yanahusiana na Elimu ,
Tutaimarisha utoaji wa Elimu kwa Umma ili watu wawe na Uelewa na wasiwe na hisia (Potofu).
Mwisho wa kunukuu
Tukisoma Ilani ya CCM 2020 uk 229 ibara 181 ibara 182, uk 124 ibara 78
uk 128 ibara 80 ukisomwa na uk 08 ibara 10 na 11 kwa msisitizo.
CCM inatambuwa kuwa Raslimali watu ndiyo nyenzo muhimu ya Maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Aidha CCM inaamini kuwa Elimu Bora ndiyo nyenzo muhimu ya kuijenga kuilea na kuendeleza Raslimali watu ili ziweze kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.
Mwisho wa kunukuu
Tusome Ilani ya CCM 2020 uk 152 ibara 102, uk 299-300 ibara 252(e)
Ilani ya CCM 2020 uk 04-05 ibara 07 ili kupata Uhalali wa kwenda kusoma ilani ya CCM 2015 uk 296 ibara 188 huku tukizingatia ibara 177uk 230.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka Tarehe 13/05/2022
Katika Maadhimisho ya miaka 10 ya Tanzania Human Rights Defenders Network (THRDC)
Alisema
Elimu kwa Umma (ni Muhimu saana) kwa sababu mtakapo elimisha Umma
Kazi yetu (Watetezi wa haki) itakuwa ndogo saana ya kutetea watu.
Ahaa, hizo Rights hazitavunjwa saana.
Kila Mtu atakuwa anajuwa Wajibu wake unavyokaa wa kikatiba
Haki yake
Wajibu wake
Kwa hiyo Rights hazitavunjwa saana.
Kwa hiyo ongezeni hilo la Elimu kwa Umma.
Mwisho wa kunukuu
Wanaccm ni lazima tujielimishe saana ili tukwepe tabia inayoshamiri ya Sisi Mafukara kulishwa Ubwabwa na kupewa Buku jero huku wanaotupatia vitu hivyo tukiwashuhudia wakijenga Migorofa na Mijumba ya maana huku Sisi tukiaminishwa kuwa ni watu wa kutumiwa tu na kulishwa Ubwabwa huku maisha yakitupa kichapo na kuishi Kama tuko Dampo tumetupwa
.Mwl Nyerere Mwenyewe alikuwa Msomi na hakukubali Wajanja wachache Wawa brain wash walio wengi.
Wewe usiye Soma unayefurahia kulishwa Ubwabwa unawezaje kujisifu ya kuwa unamfuata Baba wa Taifa Mwl Nyerere Wakati matendo yako ni matendo ya hovyo ya kuchukia Mambo ya Elimu na kujiweka katika kutumia hisia Binafsi kuwaongopea wenzio.
Professor Issa Shivji
Nakumbuka Tarehe 13/04/2022
Katika Hafla ya Uzinduzi wa vitabu kwenye kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa
Shule ya Uongozi Kibaha
Alisema
Mwl (Nyerere) Mwenyewe alikuwa Msomi
Alikuwa Mwana zuoni
Mwenye kipaji kikubwa.
(Mwl Nyerere) alikuwa anasoma saana.
Mwisho wa kunukuu
Na Ninyi Wasomi mnaojifanya Mmesoma
Onyesheni ni kwa jinsi gani mnaweza kuwainuwa Wanaccm Mafukara na sio kututisha na kiingereza kingi huku mkiwa hamfanyi jitihada zozote za kuwainua Wanaccm wenzenu wanaoaibika na kuitwa Ombaomba.
Mheshimiwa Albert John Chalamila
Wakati huo Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Nakumbuka Tarehe 03/09/2022
Alisema
Sitaki Kiingereza Wala sitaki makaratasi,
Nataka namna gani utakavyoitumia Elimu yako kuibadilisha kuwa Maendeleo.
Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Katika Hafla ya kukabidhi Magari kwa mamlaka za maeneno ya utekelezaji kwa Sughuli za TASAF Tanzania Bara na Zanzibar
Nakumbuka Tarehe 01/06/2022
Alisema
Naomba saana
Mbali ya kazi mnayo ifanya , fanyeni kazi ya Elimu (ya) kuwatoa watu kwenye Umaskini wa fikra na Waishi maisha ambayo yanaeleweka
Mwisho wa kunukuu
Elimu itasaidia hata Mabinti zetu ndani ya Chama kuto kutumiwa hovyo kwa Maslahi ya Wajanja.
Wanu Hafidh Ameir
Mwenyekiti wa Wanawake Initiative Foundation Zanzibar
Mtoto wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka Tarehe 19/06/2022
Alisema
Elimu ndiyo nyenzo muhimu itakayo msaidia kijana hususa ni msichana kuendesha maisha yake na kuepuka Unyanyaswaji.
Mwisho wa kunukuu
Mfano Diwani wa Nkiwansensaaaa
Asiyekuwa na Elimu
Hutumia hila kuwahadaa Mabinti wa Shule za Msingi ,na Sekondari
Na wengine huwatoa Mimba Guest
Na wengine kuwapiga picha za utupu na Kisha kuonyesha wapambe zake
Akiulizwa
Diwani huyu hujibu
Wasichana wananitaka wenyewe
Sasa nifanyeje
Diwani amesahau kuapo Cha maadili alichokiapa .
Mabinti Hawa tukiwapa Elimu watajielewa na kamwe hawatachezewa Tena .
Tukimpenda Mwenyezi Mungu , tutapenda Maamrisho yake .
Mwenyezi Mungu anatutaka pia tuikamate saana Elimu.
Apostle Deonis Mutalemwa Bushir
Wa ECG Church
Nakumbuka Tarehe 26/05/2022
Akitoa Mahubiri akiongelea Maagizo ya Yesu Kristo kwa Wanaadamu alisema
(Mathayo 12:50)
Kwa Maana yeyote atakayefanya Mapenzi ya Baba yangu aliye Mbinguni ,
Huyo ndiye ndugu yangu na Umbu langu na Mama yangu
Mwisho wa kunukuu
Mwenyezi Mungu anataka tusome tuwe na Elimu ili udugu wetu na Yesu Kristo ushamiri.
Sisi Baadhi tumeikataa Elimu
Tumejiweka rehani kwa watoa Ubwabwa
Tunajichekesha hovyo kwa wenye Fedha na kuwachukia wanaotukumbusha haki zetu zilizo ndani ya katiba , kanuni Miongozo na Taratibu .
Tumemkufuru Mwenyezi Mungu na kuzifurahia kufuru zetu kwa Ujinga wa kulikataa neno la Mungu.
Biblia Takatifu Hosea 4:6
Watu Wangu wanaangamizwa kwa kukosa Maarifa ,
Kwa kuwa Wewe umeyakataa Maarifa
Mimi nami nitakukataa Wewe .
Mwisho wa kunukuu
Biblia Takatifu Mithali 4:13
Mkamate saana Elimu
Usimuache aende zake
Mshike
Maana Yeye ni uzima wako.
Mwisho wa kunukuu
Sasa Wewe jitie Wazimu kamata saana Ubwabwa na Buku jero
Watajirishe Wajanja ili ukifa ukafikie Jahannam kwa Ujinga wa kupangwa safu na kuzikubali Kama umerogwa kwa kukosa Elimu ya katiba kanuni Miongozo na Taratibu.
Mtume Mohammad SAW aliambiwa Asome
Na baada ya kusoma akatuambia Umma wake Tuende mpaka Uchaina kuitafuta Elimu.
Wewe vitabu vya Chama viko huvisomi ukalia kuendekeza Ubwabwa na besenga unatajirisha watu wenye Roho Mbaya wasio kufikiria Wewe Wala familia yako kwa Ujinga tu ulio uendekeza wa kuto kusoma na kuujuwa Ukweli.
Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete
Akiwa Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi
Nakumbuka Tarehe 29/08/2022
Alisema
Ninafikiri hata kwenye Qur aan ,
Mtanisahihisha Mashekhe Wangu Kama nitakosea
Aya ya kwanza
Iliyoshushwa
Ni kwamba Mtume wetu (Mohammad SAW)
Anaelekezwa kwamba asome
Mwisho wa kunukuu
Wewe unayelishwa Ubwabwa na Kupewa Buku jero bila kusoma katiba kanuni Miongozo na Taratibu unamfuata Mtume gani Wewe.!?!?
Uhuru wako umeuweka rehani Kijinga kijinga mpaka uamuliwe Cha kufanya na watu walioiteka Akili yako kwa Ujinga tu huku wakikuongopea na Kijicheo kitokanacho na Rushwa kisicho na uhalali wa Wananchi walio wengi.
Umekubali kuwa mtumwa kwa Ujinga wa kukataa kujibidiisha kujuwa maandiko ya Chama na kuyaishi.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk( i ) Kisha uk (iv) -(vi)
Then uk 02 ibara 5(4) ili kupata Uhalali wa kwenda kusoma kitabu Cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu uk 148
Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema
Elimu ni Kama Mlima Mkubwa unaofika Mawinguni.
Kila unavyopanda
Ndivyo unavyoona vizuri Zaidi upeo wa macho yako.
Tusipo azimia kujielimisha
Tutaachwa nyuma
Tena Uhuru wetu
Utategemea tu hutuma za watu wengine na Mataifa mengine .
(Na Wala) sio uwezo wetu Sisi wenyewe.
Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka kutoka Ndotoni huko katika Ulimwengu wa kiroho huku nikiwa nafoka foka hovyo ,Someni nyie
Tusikkubali kufokewa Wala kutishwa
Uongozi ni Unyenyekevu
Ukiona Kiongozi
Anakufokea
Anakutisha
Kinyume na alivyoapa huyo ujuwe ni Mbwa Mwitu aliyevaa ngozi ya Mwanakondoo.




Kidumu Chama Cha Mapinduzi





Mathias Mugerwa Kahinga




🙏🏿🙏🏿🙏🏿🔨🔨🔨💪🏿💪🏿💪🏿
 
Duuh! Hii Ilitakiwa nisome nikiwa nimeshapata breakfast 🤔
 
ULIMWENGU WA KIROHO UNA NGUVU KUBWA SANA
KULIKO
ULIMWENGU WA
KIMWILI

Nilisikika katika Ulimwengu wa Kiroho nikitoa Mawaidha walau kuwapa kauelewa watu wasio uelewa Ulimwengu wa Kiroho
Nikaanza.

Nakumbuka Tarehe 28/03/2020
Apostle Deonis Mutalemwa Bushir
Wa ECG Church
Akitoa Mahubiri alisema
Huwa ninapenda kusema hivi ,
Ninapofundisha
Usinisikilize
Dakika moja (Wewe) ukakimbia .
Nisikilize mpaka Mwisho
Na huwa nimejitahidi ninapofundisha nikupe reference ya Maandiko .
Hata Kama Jambo Hilo ambalo ninaloanza kuliongelea Kama linakukera
Weee sikiliza Hadi Mwisho
Ninalenga msikose Baraka kabisa.
Na ili msikose Baraka ninagusa kila eneo ambalo (Mwenyezi) Mungu atanisaidia kwa neema yake.
Mwisho wa kunukuu.
Watu wengi katika Ulimwengu wa Mwili wamenyimwa macho ya Kiroho .
Kimuonekano ni Kama wanaona ila kiuhalisia katika Ulimwengu wa Kiroho watu hao wamepofuka macho
Ndiyo maana tunaanza kushuhudia Baadhi ya watu wakila Viapo na Kisha kujitokeza hadharani wakiwa wanafanya Mambo yaliyo Kinyume na Viapo vyao walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu wakimuahidi kufuata Maandiko waliyoapa kuyafuata ndani ya Jamii husika
.hapo ndipo Mwenyezi Mungu anatuma Watumishi wake kuja kuwaondolea Upofu kwa Baadhi Yao wale wenye kugundua upotofu wao ulio wapelekea kupofuka macho huku wakijiona Kama Bado wako sawa ili kuwanusuru Watu walio wengi wanaoteseka kutokana na upotofu wa vipofu walioapa kutenda haki na Kisha kuacha kutenda haki na kumtumikia ibilisi pasipo wao kujielewa Kama Tayari ni Watumishi wa Shetani.
Apostle Deonis Mutalemwa Bushir
Wa ECG Church
Akitoa Mawaidha Tarehe 28/03/2020
Alisema Mungu anapoyaona mahitaji ya Watu wake response ya Mungu anapoona Mahitaji ya Watu ni kuwaletea Mtumishi.
Mwisho wa kunukuu
Ni juu yetu kufumbua macho kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ili kuweza kuwaona Watumishi tunaoletewa ili watutoe kwenye Utumwa wa fikra.
Nasema hivi kwa sababu
Kuna watu Wanavyeo
Na wengine Wana fedha
Ila wanatumia vyeo na fedha kujinufaisha wao huku wakiwaonea Mafukara .
Cha kufanya Sisi Mafukara tunatakiwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu mbele Kisha kujipa muda kujisomea mifumo ya nchi na Kisha kuwaadabisha hao watesi wa Ulimwengu wa Mwili kwa kutumia Ulimwengu wa Kiroho.
Disciple Noel Christopher
Wa The Reality of Christ Church
Akitoa Mahubiri
Nakumbuka Tarehe 15/09/2022
Alisema
Usiangalie tu katika Ulimwengu wa Mwili ni nini kinatokea
(Katika Ulimwengu wa Mwili) Kuna watu wanaonekana ni Ma - Giants saana
Katika Ulimwengu wa Mwili.
Lakini
Katika Ulimwengu wa Kiroho ni Wadogo
Mi nakuambia katika Ulimwengu wa Kiroho ni Wadogo saana
Lakini katika Ulimwengu wa Mwili wanaonekana ni Ma Giants Wakubwa.
Mwisho wa kunukuu
Ili tuwachape Hawa Ma Giants wanaotuonea katika Ulimwengu wa Mwili Sisi tunaingia katika Maombi .
Mwenyezi Mungu anatupatia nguvu tukiwa tumelala huko Ndotoni baada ya kuwa tumefanya kazi za kimwili tumemaliza .
Apostle Deonis Mutalemwa Bushir
Wa ECG Church
Nakumbuka Tarehe 16/06/2021
Akitoa Mahubiri alisema
Maandiko yanasema
Itakuwa siku za Mwisho ,
Asema Bwana
Nitawamwagia watu wangu
Roho Wangu .
Wana wenu
Na Binti zenu
Watahubiri
Na Wazee wenu wataona Maono
Wataota ndoto
Mwisho wa kunukuu
Mchungaji Mwl Aliko wa Dorcas Mwalulili
Wa huduma ya Uhuru wa Kristo kwa Mataifa yote
Nakumbuka Tarehe 14/08/2023
Alisema
Ndoto wakati mwingine inakuja kwa sababu Mungu anataka akupe Taarifa ya kinachoendelea kwenye maisha yako
Kile adui anachokifanya.
Mwisho wa kunukuu
Pastor Sunbella Kyando
Wa Reality of Christ Church
Nakumbuka Tarehe 18/12/2020
Akihubiri alisema
Kwa Nini tunajifunza kwa habari ya Ulimwengu wa roho.
Kwa sababu ni Ulimwengu ambao upo na unafanya kazi
Wether tunaukubali au tunaukataa ,
Wether tunaupenda au hatuupendi ,
Ni Ulimwengu ambao upo na una exist.
Na kibaya Zaidi
Au kuzuri Zaidi
Ni Ulimwengu wenye nguvu kuliko Ulimwengu wa Mwili.
Ulimwengu wa Kiroho ni Ulimwengu wenye nguvu Sana kuliko Ulimwengu wa Mwili
Kwa hiyo mtu yeyote anayeufahamu vizuri Ulimwengu wa roho watu huwaga hawashindwi Jambo (lolote) katika Ulimwengu wa Mwili .
Mwisho wa kunukuu
Baadhi ya Viongozi na Watu wenye fedha walioamuwa kuwa Wachawi tutapambana nao na kuwashinda kwa Sisi kujiweka upande wa Mwenyezi Mungu na kumuomba atuzidishie ndoto nyingi ili tuwapo katika Ulimwengu wa Kiroho tupambane na hao walioamuwa kujimilikisha kila kilicho kizuri kwa Maslahi yao walio wachache.
Pastor Sunbella Kyando
Wa The Reality of Christ Church
Nakumbuka Tarehe 16/02/2022
Anasema
Wenzetu (wenye vyeo na fedha Baadhi walioamuwa kuwa Wachawi) wameenda mbali (kiuelewa)
Wana ufahamu Mkubwa saana.
Ili tuweze kushinda Vita vya Kiroho ni lazima ufahamu wetu uongezeke
Mwisho wa kunukuu
Hatutaviweza Vita vya Kiroho pasipokuwa Sisi watu wa Rohoni.
Mchungaji Jonas Singo
Katika Mahubiri Tv
Nakumbuka Tarehe 03/09/2022
Akitoa Mahubiri alisema
(Mtume) Paulo anaeleza ya kwamba kushindana kwetu si juu ya vitu
Juu ya nyama na Mwili.
Sio Vita ya Mapanga
Hatuzungumzi habari ya Vita
vya Mishale .
Lakini tunazungumza juu ya Vita vya Kiroho
Tunazungumzia katika Ulimwengu wa Kiroho.
Na katika Vita ya Kiroho ni Vita isiyoonekana.
Ni Ulimwengu usio shikika
Ingawaje Matokeo yake yanaweza yakashikika.
Yanaweza yakaonekana.
Mwisho wa kunukuu
Twendeni Sasa Ulimwengu wa Kiroho tukapambane na nafsi zoote zilizo jiinua kutuaminisha kuwa Sisi tutaendelea kuwa Vibaraka Vikaragosi na Vijibwa vya kulishwa Ubwabwa na kupewa buku jero
Wote tuseme Maisha ya kijinga Basi.
Turudi katika Ulimwengu wa Kiroho tusome katiba Kanuni Miongozo na taratibu tukiwa huko huko Katika Ulimwengu wa Kiroho ili tunapotuwa katika Ulimwengu wa Mwili tuwe tunatisha Kama Simba kwa misimamo ya kuuchukia ujinga ujinga usio na faida kwa vizazi vyetu na Sisi wenyewe.
Watu wachache wanakula vinono na masalia kuwapa Mbwa
Huku sisi tukitafuta hata makombo tu inakuwa Shida kwetu.
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Katika Hafla Silver Jubilee of Equal Opportunities for All Trust fund EOTF.
nakumbuka Tarehe 27/06/2022
Alisema

Umaskini ni nini!?
Ni njaa
Ni ujinga
Ni Maradhi.


Nataka nisisitize kuwa kazi ya kupiga Vita Umaskini, ujinga na Maradhi ni lazima iwe shirikishi .
Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka kutoka Ndotoni nilipokuwa naota huko Katika Ulimwengu wa Kiroho
Huku nikiwa nasisitiza kuwa wale wote waliojipatia vyeo kwa Rushwa waachie ngazi haraka
Hatuwatakiiiii.


Kidumu Chama Cha Mapinduzi



Mathias Mugerwa Kahinga


🙏🏿🙏🏿🙏🏿💪🏿💪🏿💪🏿🔨🔨🔨
 
WITO WA UTII WA KATIBA KANUNI MIONGOZO NA TARATIBU ZA CHAMA
VIONGOZI WOTE NGAZI ZA SHINA , TAWI ,KATA , JIMBO , WILAYA , MKOA
WATOKANAO NA CCM
WALIOHAMA
MAENEO YAO YA KIUONGOZI
WAMEPOTEZA
VYEO VYAO KIKANUNI NA KISHERIA
ITISHENI UCHAGUZI MJAZE NAFASI HIZO.

Nilisikika nikiunguruma katika Ulimwengu wa Kiroho huko Ndotoni baada ya kuona katiba Kanuni Miongozo na taratibu zinatumika tu kuwahukumu Mafukara na Watumishi wa Umma
Huku watu wa Chama wakiachwa Kama Malaika Wasafi.
Huko Ulimwengu wa Kiroho nikaanza kutema cheche

Ndani ya CCM tunayo Makundi Mawili ya Wanachama
Kundi la kwanza Dogo ni la Wanachama watiifu kwa ccm wenye muonekano Duni kimaisha ila vichwa kweli kweli
Huwatoi kwenye Misingi ya katiba Kanuni Miongozo na Taratibu
Wanaivumilia njaa hata Kama mifuko Yao imetoboka.
Wanaofuatilia hotuba na kuziishi Kauli za Viongozi wa Kitaifa.
Kundi la pili ni kubwa
Lina watu mchanganyiko mpaka wale waliotokea kuleee Uuupinnzzaan ambao wengi wao
Hawajuwi kabisa katiba Kanuni Miongozo na Taratibu
Ni waropokaji wanao tumia mdomo na maneno mengi yasiyo rasmi kuishi.
Hupenda Vyeo kuliko Taratibu za Chama
Kwao Maslahi Binafsi ndiyo kipaumbele
Ukipaza sauti kutetea utaratibu wa Chama wao hukasirika .
Wanavaa sare za Chama zile nzuri za bei Mbaya huku wakiwa hawajuwi lolote kuhusu Chama
Hulazimisha Mitazamo Yao isiyo ya Chama kuwa ndiyo Taratibu za Chama.
Hawa ndiyo vyanzo vya Migogoro ambao huamini Sheria zooote zilizo Tanzania ni kwa ajili ya Mafukara na Watumishi wa Umma na hapa ndipo huanzia Migogoro mingi isiyo na utatuzi.
Nakumbuka Tarehe 20/08/2015
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
Alisema
Baadhi ya Migogoro hii inasababishwa na Watumishi wasiofuata sheria
Na hii Zaidi ni Mijini
Lakini Hawa wasiofuata sheria hata vijijini wanazua zogo.

Nchi isiyokuwa na Utawala wa sheria ni sawa na watu wanaoishi katika Msitu ambapo mwenye nguvu ndiyo anayeishi salama.

Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Katibu NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Taifa
Nakumbuka Tarehe 11/11/2023 Akiwa Geita
Alisema
(Eeehee Mwenyezi Mungu) isaidie CCM isimame imara .
(CCM)iwe Mtetezi wa *Haki *na (watu) Wanyonge.
Wakapate Haki zao kupitia CCM.
CCM hoyeeee
Mwisho wa kunukuu.
Tukisoma Kitabu cha Sera ya CCM ya kujitegemea Kimapato na kiuchumi Chapisho la 2014 uk 03 kifungu Cha 06 kinatueleza
Katika Chama hiki tokea 2000 yamekuwepo maamuzi Mbali Mbali ya vikao vya juu vya Chama kuanzia Sekretarieti, Kamati kuu , Halmashauri kuu ya Taifa na hata Mkutano Mkuu wa Taifa kuhusu Chama .
Changamoto kubwa imekuwa ni utekelezaji wa maamuzi hayo.
Mwisho wa kunukuu
Wanaccm tunapaswa kujiamini katika usimamiaji wa Taratibu za Chama
Haijalishi tuko wachache lakini naamini tukijiamini ,
Hao walio wengi wasiofuata sheria tunao uwezo wa kuwafanya waone aibu na kubadilika kitabia
Imefika mahali watu wenye Vyeo na fedha wamejiaminisha kuwa ni watu wasio gusika
Ndiyo maana wanahama maeneo Yao na Wala hakuna mtu wa kuwagusa .
Ukiandika mbakuleba nke embeba egwile omumata agabisi.
Mheshimiwa DktJoseph Kasheku Msukuma
Mbunge wa Geita Vijijini
Nakumbuka Tarehe 08/11/2022
Alisema
Kwa kweli unafika Mahala unajiuliza ,
Pengine hii nchi ni ya Matajiri tu
Maskini hatutakiwi kuwa Tanzania.
Mwisho wa kunukuu
Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 12 na ibara 13(1)(4)(5).
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Akiwa Geita
Nakumbuka Tarehe 11/11/2023
Alisema
Mimi niwaombe ( kila mmoja wetu kwa nafasi yake) tutende Haki
Tuwe watu wa kutenda Nini..!?
(Hakiiiii...)
Mwisho wa kunukuu
Ebu tujifunze kitu kutoka kwa IGP MSATAAFU.
Nakumbuka Tarehe 21/September/2019
Mheshimiwa Simmon Nyakoro Sirro
Akiwa IGP
Akiwa ziara ya kikazi Arusha alisema

Lazima (Police) ujiamini
Unasimamia sheria
Simamia sheria lazima ujiamini
Na ndiyo maana Mimi(IGPwenu) najiamini
Au sijiamini !?
Au sijiamini !?
Asa Kama Mkubwa wako anajiamini, Wewe kwa Nini (Askari Police) usijiamini !?
Na nikasema Sisi tunasimamia sheria
Sisi hatuko kwenye upande wa Siasa
Kwa hiyo (Askari Police)
Simamia sheria
Kwa sababu sheria zipo
Na Kama kunaonekana Kuna sheria ambayo haifanyi kazi zitarudi Bungeni halafu sheria zitaondolewa au zitafutwa.
Lakini Wajibu wetu Mkubwa (Sisi Police ) ni kusimamia Sheria
Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Katibu NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Taifa
Nakumbuka Tarehe 10/11/2023
Akiwa Chato
Alisema,
Mimi nataka kufuata Sheria
Chama hiki (Cha CCM)kinasema tufuate nini ....(*sheria).
Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Ni mtu anayesimamia kauli zake na hajawahi kuwa kigeugeu
Akisema kasema
Hageuki geuki.
Nakumbuka Tarehe 11/11/2023
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Akiwa Geita
Alisema
Sijawahi kugeuka na Wala sijawahi kuwa na tabia ya kugeuka geuka
Mwisho wa kunukuu
Kwa msingi huu ni lazima Sasa katiba Kanuni Miongozo na Taratibu zifuate mkondo wake.
Tusome katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26 yote kwa kuizingatia ibara 8(d) bila kuiacha ibara 9(a)(b)(f)(h)
Katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk i uk iv -vi, uk 02- 04 ibara 5(9)(11)
Ilani ya CCM uk 01 ibara 04, uk 161 -168 bila kuacha ibara 10 na 11.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk 153 Vifungu 04 na 13 ili kupata Uhalali wa kwenda kusoma Kanuni za fedha na Mali za Chama na Jumuiya zake uk 164-165 kwa msisitizo
Kanuni za Utumishi za Wafanyakazi wa CCM na Jumuiya zake toleo 2019 uk 73 wote . Huku tukizingatia katiba ya CCM 1977 toleo 2022 ibara 5(16)(17)(18)

Sasa tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk 153 kifungu cha 02 ili kupata Uhalali wa kwenda kusoma Kanuni za Uchaguzi wa CCM toleo la December 2022 uk 58 ibara 116(c)(f)
Inatueleza Bayana kabisa bila kificho
Nafasi ya Uongozi itakuwa imeachwa wazi endapo litatokea mojawapo katika matukio yafuatayo kumhusu kiongozi aliyekuwa ameshika nafasi hiyo
(C) Ataachishwa au atafukuzwa Uongozi kwa mujibu wa katiba ya Chama .
(f) kulihama eneo la Uongozi wa ngazi yake au Tawi lake Maalumu na hivyo
Kuwa nje ya upeo wa Madaraka ya kikao ambacho kabla ya *kuhama *alikwa Mjumbe wake .
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa hawafungwi na sababu hii kwa Maana upeo wa Uongozi wao ni nchi nzima.
Mwisho wa kunukuu
Kuna Viongozi tokea Shina Hadi Mkoa Matapeli huwadanganya Wanaccm kwa kuwaeleza Uongo kuwa kwa mfano
Mwenyekiti wa Shina anaweza kuwa na alishajenga nyumba katika eneo la Uongozi
Ila anapoihama nyumba hiyo hupoteza wadhifa wake.
Vivyo hivyo Tawi , kata , Jimbo Wilaya na Mkoa .
Kuwa na umiliki wa nyumba eneo lako la Uongozi wakati umeliahama eneo hiloukaiacha nyumba tu labda na wapangaji inakuondolea sifa ya kuendelea kuwa kiongozi
Kwa hiyo Wenyeviti wa mitaa , Madiwani , Wabunge nk na Viongozi wengine ambao hampo maeneo yenu Ninyi sio Viongozi Tena .
Tafuteni Mambo mengine mfanye.
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Katibu NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Taifa
Akiwa Mkoani Dodoma
Alisema
Kwenye nafasi ya usemaji Wangu nitakuwa kidoogo na maneno machache lakini (ni maneno )yenye Malengo ya Matokeo makubwa.

Kwa maneno hayo mtegemee Ukweli usiopinda
Kauli thabiti isiyoyumba
Lengo la kujenga Chama imara kisicho yumba kwa madhubuti ya kuisimamia serikali.
Mwisho wa kunukuu
Someni katiba ya CCM 1977 toleo 2022 uk 10 -11 ibara 15(2)(3)(4)(5)(6)(7), uk 07 ibara 12(1)(a) ili kwenda uk 152 Vifungu 3,6,8, uk 06 ibara 8(1)(2)(5)(6) ibara 13(1)(c)(d)(e) ibara 19(1)(c)(d)
Tusome Kitabu cha Awamu ya tatu ya Mradi wa kukiimarisha Chama uk 07 kwamsisitizo tukisoma kwa Pamoja na ilani ya CCM uk 01 ibara 04 na ibara 10 na 11.
Askofu Dkt Josephat Mathias Gwajima
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima
Na Mbunge wa Kawe
Katika clip iliyorushwa Mtandaoni Tarehe 31/102023
Mheshimiwa Askofu alisema
Ukiifukia kweli siku itakapofufuka (kweli hiyo ujuwe) haifi Tena.
Mwisho wa kunukuu
Comrade Daniel Godfrey Chongolo
Katibu Mkuu CCM Taifa
Akiongea katika Halmashauri kuu (w) Ubungo
Nakumbuka April 2022
Alisema
Hiki sio Chama Cha mtu (fulani )
Hiki sio Chama Cha Maslahi Binafsi.
Hiki Chama ni (Chama) Cha Wanachama (wote wa CCM)
Na ni lazima tutende Haki kwa sababu katiba yetu (ya CCM) inatutaka tufanye hivyo.
Mwisho wa kunukuu
Watu waliokiuka Taratibu ndiyo vyanzo vya Migogoro.
Na Viongozi wote Jamii ya Kobe aliye juu ya mti ni vyanzo pia vya Migogoro kwa sababu maamuzi Yao mpaka waulize watu waliowaweka hapo
Wote wafyekwe
Watolewe ili kweli CCM ikawe Mtetezi was kutumainiwa na Wanyonge.
Mtu akivunja katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za Chama
Maana yake amevunja sheria ya nchi The Political parties act chapter 258 inayovisisitiza Vyama vya siasa kuyafuata kikamilifu maandiko Yao.
Pia mtu Huyo anakuwa amevunja sheria Mama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1) ikisomwa na ibara 09 (a)(b)(f) na anakuwa ameikiuka kwa maksudi ibara ya 8(d) ya katiba ya nchi.
Anastahili kukamatwa na Jeshi la Police .
Tunapowalaumu Watumishi wa Umma tuyaone na haya kwa jicho la Kiroho la kuondoa boriti kabla ya kibanzi kilicho kwenye macho ya tuwatizamao
Nakumbuka Tarehe 11/11/2023
Mheshimiwa Paul Christian Makonda
Katibu NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Taifa
Akiwa ziarani Geita
Alisema
Natumia fursa hii kuziomba kamati za. Siasa za Wilaya na za mikoa zisiwavumilie Watumishi (wa Chama na Serikali ambao ni )Chanzo Cha Migogoro.
Mwisho wa kunukuu
Nikashtuka kutoka kwenye ndoto nikiwa nasema Bla bla Watanzania zimetutosha
We need action now.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi



Mathias Mugerwa Kahinga


🙏🏿🙏🏿🔨🔨💪🏿💪🏿
 
Dionis Mutalemwa Bushir wa ECG Makongo.....anayejiita mtoto was Apostle Bushir mmalawi aliyekimbilia AFRIKA kusini kutapeli watu....KAZI ipoooo!

Tutafika tumechoka Sana.
 
We ndo yule jamaa uliekua unaitika "Aaamina" kwenye kanisa la kiboko ya wachawi?
 
Back
Top Bottom