WAKATI NI HUU TUKISAFISHE CHAMA KWA KUCHUKULIANA HATUA ZA KISHERIA
Tusome Ilani ya CCM uk 303 ibara 254,255
uk 04-05 ibara 07 ili itupe Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha ilani 2015 uk 296 ibara 189
uk 233 ibara 185b.
uk 230 ibara 177 bila ya kuacha kuisoma ibara 10 na 11 ya Ilani ya 2020.
Nakumbuka April 2019
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Mtetezi namba Moja wa Tanzania
Akiwa Makamu wa Rais
Katika kongamano la kumuenzi Hayati Abeid Aman karume
Alisema,
Si Sisi tunaodhulmu Mali za watu.
Kwa sababu tu umepata Kicheo , umekuwa Sheha, umekuwa Diwani,
Umekuwa mbunge, umekuwa Mwakilishi, umekuwa Nani
Unasimama
Unasimama kudhulmu haki ya Mwananchi mwingine
Mzee wetu hakutufundisha hayo ,
Alitufunfisha unapata cheo , tumikia watu.
Wewe ni Mtumishi wa Watu
Simamia haki zao
Ndivyo alivyo tufundisha.
Mwisho wa kunukuu
Tusome Standing order for the Public service 2009
Pursuant to s. 35ndogo 5 of the republic services act cap 298 uk 16 kifungu cha 6.9
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 uk 19 ibara 10
Sheria ya Mwaka 1984 namba 15 ibara 06.
Pia uk 26 Kifungu C.1kidogo 3.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2020 uk 152 kifungu cha 14 ili tupate Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha Tume ya Uthibiti na Nidhamu ya Halmashauri kuu ya Taifa uk 4-5 kifungu cha 7 b.
Maandiko yanasema,
Mtu anapoingia kazi ya Uaskari na kupasishwa kuwa anafaa kwa kazi hiyo , havui magwanda mara baada ya hapo na kutenda apendavyo nje ya Taratibu za Uaskari
Kinyume Chake hutakiwa afanye Mazoezi zaidi na kuwa tayari zaidi kutimiza Wajibu wake maana Sasa amehitimu .
Kuingia katika CCM Kuna Taratibu zake.
Na kuendelea kuwa Mwanachama wa CCM nako Kuna Masharti
yake.
Mwisho wa kunukuu
Tukisoma Kitabu cha Mwongozo wa CCM 1981uk 26-27 kifungu cha 37 kifungu kidogo Cha 2.
Maandiko yanasema,
Wanaccm ndiyo Askari wa Mstari wa mbele wa Mapambano ya kujenga Ujamaa .
Mwisho wa kunukuu
Wanaccm wenzangu haiwezekani Sisi ni Askari tumesoma katiba Kanuni Miongozo na Taratibu Kisha tukae kimya huku tukiona Chama Cha Mapinduzi kikihujumiwa hovyo tu.
Tutakuwa tumepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2020 uk 151 vifungu 1, 3, 6 na 8.
Tusome Kitabu cha The Political Parties act chapter 258 uk 11 kifungu cha 6A1,2, na 5.
Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26 na 9a,b bila kuacha ibara 18a.
Ilani ya CCM 2020 ibara 110c.
Azimio la Arusha uk 01 kifungu d.
Katiba ya CCM 1977 toleo 2020 uk 2-3 ibara 5 kifungu kidogo Cha 8.
Ilani ya CCM 2020 uk 161-168. bila kuacha kurudi uk 01 ibara 04.
Tusome Kitabu cha Sera ya CCM ya kujitegemea Kimapato na Kiuchumi uk 03 kifungu cha 6.
Kitabu cha Awamu ya Tatu ya Mradi wa kukiimarisha Chama uk 07.
Kitabu cha Binaadamu na Maendeleo uk 17-21 Kilichoandikwa na Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Tukisoma Kitabu cha The Magic of Thinking Big uk 41.
Professor David J. Schwartz Ph.D
Anaandika,
Fear is success enemy number one .
Fear stops people from capitalizing on opportunity.
Fear wears down physical vitality.
Fear actually makes people sick .
Causes organic difficulties, Shotens life,
Fear closes your Mouth when you want to speak .
Mwisho wa kunukuu
Mfumo wa nchi yetu
Chama ndicho huisimamia Serikali.
Tunapokuwa na nia njema ya kuisimamia Serikali ili iwe na Uaminifu na Uadilifu
Ni lazima Sasa Chama tuchukuwe hatua za maksudi kujisafisha pale tunapohisi tumeteleza.
Tusome Mwongozo wa CCM 1981 uk 45-46
Tukisoma Tena uk 26 Maandiko yanasema,
Kukiri upungufu si kitendo Cha kujidhoofisha Bali ni kitendo Cha kujiamini na kujiimarisha .
Mwisho wa kunukuu
Tukisoma Kitabu cha Ujamaa Essay on Socialism uk 80-81
Mwl Julius Kambarage Nyerere
Anaandika
The Rule of law and Equality before the law are one essential means of preventing exploitation.
But they are are only practical when the society as the whole is based on the principle of Equality - When, in other words a socialist policy is being followed.
Mwisho wa kunukuu.
Tusome Kitabu cha Kujenga Ujamaa Tanzania
Miaka Kumi ya Kwanza
Matatizo Mafunzo, Matamanio uk 27-30
Ambacho Mheshimiwa Benjamini William Mkapa alishiriki Uandishi.
Lazima tukubali CCM tulikosea Mahali
Simaanishi kufukuwa makaburi.
Namaanisha kwamba tumeshajuwa ni wapi tulikosea na Sasa kazi tuliyo nayo ni kuyarekebisha makosa hayo.
Inapotokea Kuna Wanaccm wanatulazimisha kuheshimu na kuyatii makosa na kuyaishi kimazoea kinyume na Maelekezo ya ilani ,Tafsiri sahihi inakuwa ni kwamba watu hao Wana agenda ya Siri ya kuunga mkono Upinzani huku wakituonyesha sura za Tabasamu kumbe Wana ngozi za Mwanakondoo.
Inapotokea kwa mfano baadhi ya Viongozi walioko kwenye Dola
Kwa aina moja ama nyingine
Wakatumia Rushwa na Ghilibu
Na nguvu zao za Kiuchumi kuwasimika Viongozi wawatakao wenye Uelewa Mdogo na Mambo ya Chama, ambao hawatokani na ridhaa ya Wanachama kwenye Chama,
Hii dhana ya Chama kuisimamia Serikali inakuwa imekaaje.
Waasisi wa CCM walikuwa na Maono kuweka katiba Kanuni Miongozo na Taratibu kwani vitu hivi ndiyo huwa chachu ya kujenga uaminifu na Uadilifu ndani ya Jamii.
Vitendo vya watu fulani kuisigina katiba na sheria zingine kwa kujihusisha na Mambo ya Ubaguzi na upendeleo vinajenga Chuki na kustawisha roho za usaliti kwa Wanaccm walio wengi walio dharauliwa na kutokusikilizwa kwa Chochote.
Masharti ya kuwa Mwanaccm sharti mojawapo kila Mwanaccm awe ni mtu Mwenye kuheshimu watu.
Nauli Miongoni mwetu wale waliotumia nguvu ya Kiuchumi kuwaweka watu je
NI kweli waliiheshimu Matakwa ya katiba ya CCM.
Kama walikiuka ni Nani wa kuwawajibisha.
Katiba ya CCM ibara 13 na 19 imeeleza hatua za kuchukuliwa kwa wale wanaokiuka masharti ya uanachama je
Tutaleana mpaka lini.
Tunalea uozo Kisha tunatoka hadhani tunalaumu kwa wale wenye kustahili kuchukuwa Maamuzi.
Tunachukuwa Maamuzi kwa kuangalia ni Nani alitulisha Rushwa.
Sheria inapomgusa mlisha Rushwa wahusika wanajifanya Wamekuwa Samaki maji yamewajaa midomoni sauti zao hazitoki.
Mikakati inaanza ya kuandaa kumpoteza yule anaye ligalambuwa kwa vile anakuwa anaharibu ulaji haramu wa Watu.
Wito Wangu kwa Viongozi Wakuu ndani ya Tanzania.
Kwanza tusome Katiba ya CCM uk 152 kifungu cha 2 ili tupate Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha Kanuni za Uchaguzi wa CCM toleo la 2017 uk vi-ix
Tukiweza turudie hata mara tatu .
Kisha tusome Tena Maharti ya kuitwa Mwanaccm kwenye Katiba ya CCM uk 6-7 ibara 8 kifungu kidogo Cha 2,4,5,6
Ibara ya 15 kifungu kidogo cha 2,4,7
Tusome ibara 13 kifungu kidogo Cha c,d,na e.
ibara 19 kifungu kidogo Cha c, d.
Turudi kwenye Kanuni ya Uchaguzi wa CCM toleo la 2017 uk 58 kifungu cha 116 c.
Tusome katiba ya CCM uk 152 kifungu cha 8 ili tupate Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha Kanuni za Uongozi na Maadili toleo la 2017 uk 2 kifungu cha iv. Na kwa Msisitizo na Mazingatio bila ya kuonyesha kiburi Cha Fedha na Nyadhifa tusome uk 4 kifungu cha vii.
Tusome uk 31 - 32 kifungu cha vii na viii.
Tusome katiba ya CCM uk 152 kifungu Cha 4 ili tupate Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha Kanuni za Fedha na Mali za Chama na Jumuiya zake toleo la 2018 uk 164-165 vifungu 14,2 na 14,3. uk 162 kifungu cha 14,1 a.
Tusome katiba ya CCM uk 152 kifungu cha 13 ili tupate Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha Kanuni za Utumishi za Wafanyakazi wa CCM na Jumuiya zake toleo la 2019 uk 01 kwa Mazingatio Makubwa na kujifikirisha bila ya kuacha uk 73 wote.
uk 81 kifungu cha f.
Tusome katiba ya CCM 1977 toleo 2020 uk 152 kifungu cha 14 ili tupate Uhalali wa kwenda kusoma Kitabu cha Tume ya Uthibiti na Nidhamu ya Halmashauri kuu ya Taifa uk 4-5 kifungu cha 7 b.
Maandiko yanasema.
Mwanachama anao wajibu wa Kikatiba ambao anatarajiwa autimize.
Lakini tunao ndani ya Chama watu wengi kidogo wanaoitwa Wanachama ambao hawatimizi wajibu Wala Masharti .
Tunao Mabepari , walanguzi, walevi ,
Wazururaji nk waliodumu kwa miaka mingi na Wala hakuna Uthibiti unao wasaidia kujirekebisha.
Iko haja ya kuwathibiti Wanachama hao.
Wale wasioweza kurekebishwa waondolewe kwenye Chama katika jitihada za kukitakasa Chama.
Mwisho wa kunukuu.
Hayati Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
Akiwa Singida -2020
Alisema
Haya yanahitaji Uongozi wa Kweli unao mtanguliza Mungu Mbele.
Tunahitaji Taifa hili liendelee kwenda mbele.
Mwisho wa kunukuu.
Naye Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Tarehe 22/03/2021
Alisema,
Mimi na Mwenzangu Dkt Hussein Ally Mwinyi tutaendeleza alipoishia na tutafika pale alipopatamani.
Mwisho wa kunukuu
Mheshimiwa Rais Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli alitamani tuwe watu wa kutii Maamrisho ya Mwenyezi Mungu
Tuanze Sasa kutendeana haki na Usawa kwa kusoma na kuyafanyia kazi maneno yaliyomo ndani ya katiba Kanuni Miongozo na Taratibu.
Kwa kufanya hivi tutakuwa hata tukiwashirikisha Viongozi wa Dini it's kuwa ni sahihi.
Tunapopinda Mambo na kuwaumiza Makapuku kisha kuwashirikisha Viongozi wa Dini wawe mashuhuda wa Mambo yasiyo mtukuza Mwenyezi Mungu tujuwe tunamlazimisha Mwenyezi Mungu aonyeshe hasira zake juu yetu.
Tusome Kitabu cha Mwongozo wa CCM 1981 uk 104 kifungu cha 110
Tusome kijitabu Cha Azimio la Arusha uk 01
Tusome Kitabu cha The Political Parties act chapter 258 uk 11 kifungu cha 6A1, 2,na 5.
Mwandishi John C Maxwell wa Kitabu kiitwacho The 21 Irrefutable laws of leadership uk 78
Anaandika,
No leader can break trust with his people and expect to keep influencing them.
Trust is the foundation of leadership.
Mwisho wa kunukuu
Tusome Kitabu cha Ilani ya CCM 2020 uk 298 kifungu 251 na uk 4-5 ibara 07 ili kwa ibara hii tupate kibali Cha kwenda kusoma Kitabu cha ilani ya CCM 2015 uk i kifungu cha 01.
uk 229 ibara 175.
Na uk 230 ibara 177 bila kuacha kurudi kusoma ibara 10 na 11 ya ilani ya CCM 2020 uk 08.
Mwenyezi Mungu ametupa akili za kupambanua mema na Mabaya .
Tutumie akili zetu kuishi kwa kufuata Taratibu tulizojiwekea .
Kuwa na viburi na jeuri ya kusigina katiba Kanuni Miongozo na Taratibu ili kuwa Furahisha Wachache na kuwaudhi waja wa Mwenyezi Mungu walio wengi ni ishara mbaya mbele ya Jamii inayotuamini
Tuachane ya Matendo haya yenye Viashiria vya Ujinga na Upumbavu .
Wewe Mungu ameisha kubariki .
Unaona Choyo gani kuwasaidia wenzio
Kila unavyojilimbikizia Mali kinyume na sheria ndivyo unavyozidi kuwa na Roho mbaya ya kuwanyari na kuwaonea Maskini.
Halafu kweli mtu Jamii hii anaweza kudai ana akili.
Hofu ya Mwenyezi Mungu iko wapi.
Imani anazo agiza Mwenyezi Mungu za kuwapenda Maskini ziko wapi.
Tunafanya jitihada gani ili tuonekane sio Wajinga Bali watu wenye akili.
Nakumbuka. Miaka fulani
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa
Akiwa Chato.
Alisema,
Ni Muhimu kurejea falsafa na kauli za Muasisi wa Taifa hili Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye alitamka kwamba ili kuweza kupata maendeleo ya kweli nchini Tanzania hatuna budi kupambana na maadui Wakuu watatu.ambao ni Umaskini maradhi na Ujinga
NI dhahiri kwamba Maono hayo ya baba wa Taifa Bado yapo hai na yanapaswa kuzingatiwa na kila Mtanzania kwa nafasi yake na kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu.
Mwisho wa kunukuu
Tulikosea kuwakaribisha wageni kutoka Upinzani .
Walipofika kwetu pasipo kuangalia Wala kukumbuka nyakati za mapigano ya kisiasa Kati yetu tuliwapokea na kuwapa Ofisi zetu za CCM Kisha Sisi wafia Chama tukatoka kwenye Ofisi hizo tukakaa nje na mbali ya Ofisi zetu kwa Msaada wa watu Wachache Wabinafsi.
Tukumbuke walivyokuwa wakitutukana nakutubeza je ni lini walisimama kutuomba radhi kiasi kwamba tulikubali msamaha wao na tukiamua kusigina katiba Kanuni Miongozo na Taratibu tukawalisha bata la Ukweli.
Kwa vile baadhi ya wageni hao hawakuwa na nia njema ,
Baada ya kujiimarisha wageni hao wamerudi kwao wakawasomba Ndugu zao ili waje waongeze nguvu ya kuwasaidia kuwaweka pembeni Wanaccm Wafia Chama.
Matokeo ya haya mfano tu ofisi ya imebomolewa Kisha kiwanja kuuzwa kwa mtu Binafsi kinyume na Maelekezo ya Kanuni ya Mali za Chama na Jumuiya zake.
Waliyoyafanya haya wapo Madarakani na wanalindwa.
Kwa tabia Kama hizi na zinginezo ni wazi tusipo chukuwa hatua kujirekebisha maana yake
Kwanza Chama kitapoteza maana halisi ya kuisimamia Serikali kwa Uadilifu na Uaminifu.
Tusipojirekebisha tutakuwa tunazalisha Viongozi wa Chama ambao kazi yao itakuwa nikuwatia misuko suko Wataalamu na Wasomi ambao waliumia kusoma na Matokeo yake wanakuja kuishia mikononi Mwa Viongozi waovu Wabinafsi wasiojuwa Wala kujali katiba Kanuni Miongozo na Taratibu za nchi.
Nakumbuka April 2019
Hayati Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
Akiwa Naliendele Mtwara
Alisema,
Chama Chetu Cha Mapinduzi ni Chama kinachokubali kukosolewa.
NI Chama Cha kuambizana Ukweli na ndiyo maana na Mimi nimesimama hapa kuwaeleza Ukweli
Mwisho wa kunukuu
Nini Sasa kifanyike ili kusafisha haya.
Wa wamrudie Mola watubu wajute kusigina viapo na kumfanyia Mungu shirki.
Wajutie viburi vya wazi na jeuri walizoosha kwa Watanzania wakati wanajuwa Wana ahadi na Viapo vya Uaminifu na Uadilifu mbele ya Mwenyezi Mungu na Jamii kwa Ujumla.
Wanaccm tuko si Chini ya 16 million
Niwaombe Wakuu wangu wa Kitaifa.
Wekeni mkakati wa kukiimarisha Chama.
Mkakati wa dhati wenye hofu ya Mwenyezi Mungu usiowakumbatia wanjanja Wachache.
Mnapofika ngazi za huku chini
Kwanza waondoeni hofu Wanaccm Makapuku.
Wahakikishieni usalama wao
Kisha waaacheni watapike
Sasa sikilizeni wao wanamtaka Nani Kisha wapeni wanaye mtaka walio *wengi .
Kuwaziba midomo Maskini nakuwaacha bila ya kuwatetea huku tukitangaza Kama Sisi ni watetezi wa Wanyonge huku tukiwa hatuwajali wala kuwasikiliza tutakuwa tunaigiza na kuitafuta tiketi ya Jahannam kwa nguvu zote .
Tukiyarekebisha haya
Tujuwe Chaguzi zijazo tunateleza tu Ushindi mezani.
Katika Ulimwengu wa Kiroho naonyeshwa
Ugumu wa ccm unatokana na baadhi ya Viongozi wa Vyombo vya Dola wenye Tamaa ya Vyeo na kuwanyonya Maskini kwa ajili ya kuishi maisha ya kufahari waliwekeza fadha nyingi kusimika Viongozi maboya yasiyo just katiba Kanuni Miongozo na Taratibu kwa Maslahi ya kuitafuta na kuwadhulmu Maskini ili wakose wa kuwatetea.
Sote ni juu yetu kuamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwatendea wema Maskini
Au kumtumikia Shetani kwa kuviza haki za Wanyonge huku tukitumia Vyombo vya habari kuiaminisha Jamii ya kuwa Sisi ni wema huku tukiwa na vika Kali dhidi ya wema wenyewe.
Nakumbuka Mwaka 2019
Katika mashindano ya kuisoma Qur aan Dar
Hayati Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
Alisema
Tujitahidi kuyaishi Maandiko matakatifu tuliyoletewa na Mwenyezi Mungu.
Mimi naamini endapo tutaishi kwa kadri ya Maandiko ,
Sio tu tutaendana na Mapenzi ya Mwenyezi Mungu lakini pia itatusaidia kulijenga Taifa letu kwa kuwa Taifa Bora na imara lenye watu Waadilifu na ambao litakuwa mfano wa kuigwa kwa Maendeleo Duniani.
Hivyo sote tujitahidi kuishi kwa kadri ya makusudi ya Mwenyezi Mungu.
Mwisho wa kunukuu
Nakumbuka Tarehe 22/03/2021
Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
Alisema,
Alikuwa si tu Kiongozi, Bali pia Dkt John Pombe Joseph Magufuli alikuwa mzazi na Mlezi kwa wengi .
Mwenye kulea Sana
Zaidi alikuwa ni mtu Mkweli Sana .
Nataka kusema alikuwa ni mtu wa kutumbuwa pia.
Mwisho wa kunukuu
Naomba tuwatumbuwe waovu .
Tupo kwenye vyama pinzani tutende haki na kuswafiana Nia zetu.
Magunia tuyoyabeba migongoni yenye misumari huu ndiyo wakati wa kuyatupa Chini wakati tunatazama 2024
na 2025 kwa matumaini.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga
ππΏππΏππΏππΏπ€πΎπ€πΎπ€πΎ