Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Pre GE2025 Upendo Peneza aeleza sababu za kuondoka kwake CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Asingeweza; hakuwa na mamlaka hayo. Teknik ya hayati JPM ya kuufuta upinzani ilikuwa ni utendaji kazi uliotukuka, uliokuwa unapelekea wapinzani wahame wenyewe kutoka upinzani kurudi CCM
Mbona alizuia mikutano ya siasa alikua na mamlaka hayo?

Mbona alikataa Lissu asitibiwe kwa pesa ya serikali kwani alikua na mamlaka hayo?

Alipompa maelekezo spika afukuze wapinzani bungeni ilia "awashughulikie" alikua na mamlaka hayo?

Alipomkataza CAG asikague manunuzi ya ndege na mikataba ya SGR alikua na mamlaka hayo?

JPM hakuwahi shindwa fanya kitu kisa eti sheria.
 
Dada anafunguka vibaya huko clouds FM kuhusu mambo ya cdm. Anamuanika Mbowe hadharani.
Hapo unashangaa kipi mbona nimarudio ya kila siku kama waliondoka makatibu wakauu wa chama na chama kikabaki imara hadi leo nae atasahaulika na tunamshukuru kwa mchango wake alipokuwepo
 
Hapo ni kama mtu alikuwa kwa shetani yupo kwa Mungu anamponda shatan ila asitukane mamba siasa haina yako ujui
 
Wamuhoji na Uraia wake maana ni Mnyarwanda ..

Anafanya kila namna ili CCM imuamini impe nyadhifa kubwa baadae aitumike Rwanda kwa mgongo wa CCM..

upendo peneza
Wakati akiwa muaminifu kwa Mbowe mbona hukuyasema hayo ya habari ya uraia wake?
 
Swali LANGU ni kuwa,

Ikiwa hakupenda Utaratibu huo wa kuchangisha wabunge kiasi Fulani Cha pesa kubaki kuendesha chama,

Kwanini asipinge Utaratibu huo akiwa CHADEMA?

Naongelea point ya hypocrisy!!
Kwani kuchangia jengo kama hatua ya kustawisha chama au taasisi yako kuna shida gani
 
Mbowe yupo kibiashara zaidi. Ndio maana, hataki kuachia uenyekiti. Yupo hiari haya mambo ya CCM na ufisadi wao uendelee, huku yeye anaendelea na biashara yake ya ruzuku na wabunge.

Yaan akipata wabunge let say 100.Kila mbunge akatoa one million kwa mwezi, ni 100,000,000 kwa, mwezi. Kwa mwaka anapata 1.2 billion. Kwa five years anapata 6 billion. Kwann atoke kwenye uenyekiti??? Hapo bado ruzuku ya 2 billion.
Kama walinunua jengo la ofi Mikocheni hiyo ni nzuri walifunge rasmi kwa hafra.
 
Mimi sio kwamba sipendi Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa cdm, bali ni sitaki kabisa. Sina tatizo binafsi na Mbowe maana hatujuani kabisa. Mimi namjua kutokana na umaarufu na nafasi yake, lakini mimi hanijui hata kidogo.

Kimsingi kabisa Mimi sio muumini wa kiongozi yoyote wa kuchaguliwa kukaa nafasi Moja kwa zaidi ya miaka Kumi, na sababu hasa ni kuwa kiongozi akikaa zaidi ya miaka 10 kwenye nafasi Moja anaweza kuharibu mazuri, ama kuongoza kwa mizengwe. Mifano halisi ya viongozi hao ninao. Na Mbowe anaangukia kwenye hali hiyo Sasa. Hivyo hili jambo kwangu kwa Mbowe sio personal, bali ni kwa afya ya Taasisi.
Mbona CCM ipo miaka 60 sasa km ni muumini wa kubadilishana mambo ya siasa ni magumu sana. Chadema kiko kwenue wakati mgumu sana serikali ya ccm inawawinda kuwabomoa. Mabadiliko yoyote ni ku risk
 
Peneza mwenyewe alishawahi kusema michango ya wabunge ndio imetumika kununua Hilo jengo la makao makuu. Nashangaa Leo anapodai hajui pesa zilienda wapi. Huyo anafustrations zake tu.
Pengine Peneza amelipwa aseme hivyo kwa manufaa ya kipropaganda..
Kuhusu masuala ya upinzani usitarajie ukweli kutoka kwenye media za ccm kama:-
Tbc, Clouds, Channel 10, Wasafi, nk
 
Kwani kuchangia jengo kama hatua ya kustawisha chama au taasisi yako kuna shida gani
Peneza pesa zake kukatwa kuchangia jengo Yeye hakupendezwa,

Akanyamaza, aliponunuliwa, Akaenda kulalamikia CCM!!
 
Hatuwezi kumlaumu wala kumshangaa, ni haki yake. Akiondoka CCM atawasema tu vile vile kama ambavyo anawasema CHADEMA sasa hivi.
Na muogope sana mtu wa namna hiyo.
 
Back
Top Bottom