Upigaji Uyui: Waziri Mkuu ashangazwa kibanda cha Mlinzi VETA kujengwa kwa Tsh. milioni 11, aagiza waliyosimamia ujenzi kukamatwa

Waziri Kassim ameteleza
 
Sema awamu ya tano kulikuwa Kuna majambazi wakubwa nikikumbuka ile TL 1.5 ilivyoibwa kama mvua
 
Waziri mkuu Majaliwa ameiagiza Takukuru kuwakamata wote waliosimamia ujenzi wa Chuo cha Veta Uyui

Majaliwa ameshangaa kuona kibanda cha mlinzi kimegharimu tsh 11 milioni

Source ITV habari
 


Mupe.....Muruke.....

Imerudi Tena Kwa Kasi
 
Wewe utajenga kwa kutumia Kodi / Jasho la wananchi ambao hata milo miwili kwa siku tatu ni tatizo ?
 
Kuna wakati ni vigumu sana kufananisha ujenzi kwa kutumia force account kuoka eneo moja na lingine.

Kuna baadhi ya maeneo wananchi wanajitolea nguvu kazi na kukusanya mchanga pamoja na mawe.Maeneo mengine kila kitu unanunua kuanzia mchanga.
Hata kama ni hivyo. Hicho kibanda ndiyo kigharimu Milioni 11?
Kila kitu ni tozo bila kujali uchumi wa wananchi. Sasa hivi kumtumia mtu 150,000 unakatwa kama 3,000 hivi bado huko hajatoa. Vifurushi kila siku vinabadilishwa wanavyotaka ndiyo matokeo yake haya. Wanapesa nyingi ambazo wamezipata siyo kihalali.
 
Iko aina ya 4 ya Demokrasia inaitwa homophrodite demokrasi. Hii wananchi wanakua na vyama vingi. Hivyo vyama vingi vinaunda mirengo. Mirengo inatoa mgombea Urais atayepigiwa kura na wananchi akishindanishwa na wamrengo mingine na wagombea binafsi wa Urais. Vyama pia vinatoa wawakilishi wagombea wa ngazi mbalimbali wachaguliwe na wananchi. Baada ya hapo mrengo utakatoa utakaotoa Rais na Makamu wake wanaunda serikali kutoka vyama vya mrengo huo. Wakati mwengine waziri mkuu asiwepo wakati mwengine awawepo inategemeana ilimradi wanasiasa wamethia jinsi ya kugawana vyeo. Wakati mwengine Rsis aamue kuendesha serikali na makamu wake au amuache na aendeshe na wapinzani wake. Wakati mwengine makamu wa Rais ampinge Rais na aendeshe shughuli zake za kisiasa kivyake.
 
Gharama ya ujenzi inachangiwa na factor nyingi sana...Kuna gharama ya kuendesha ofisi ambapo utakuta mkandarasi yupo Dar, Kuna gharama ya kusafirisha vifaa kutoka Dar hadi Tabora, unaweza kuta gharama ya kufanya plumbing (piping) ni kubwa sana kutokana na kibanda Cha mlinzi kuwa ghetini ambapo ni mbali kutoka sehemu ya mwisho wa maji taka.

Hapo bado utakuta waya wa Armoured kwa ajili ya kuepeleka umeme kwenye hicho kibanda kimetembea umbali zaidi ya mita 300m kutoka sehemu yenye main panel. Bado Kuna cut and fill kibao ili mandhari yawe mazuri.

Kuna factor nyingi sana, Kama angesema mradi wa Chuo kizima ni kibubwa ingeleta maana, yaani viongozi wanachukulia majengo madogo baada ya final fix.

Hapo bado kuleta miundombinu ya simu kwenye kibanda Cha mlinzi ambapo ni mbali sana na main saver..
 
eee Mungu wetu watu watakoma lini kuiba fedh za umma?!

mara nyingi huwa njiuliza, inakuwaje mpaka Waziri Mkuu afike ndipo ubadhirifu uonekane?!! inamaana viongozi wengine k kt eneo husika huwa wamelala?!
 
Akili za Watanzania ni finyu pamoja na viongozi wetu.
Watanzania wakisikia kuna mtu kasimamishwa kazi au katumbuliwa mioyoni wanapata raha.
Hapa haijaibwa hata mia
 
Hapo hakuna tiles za Mable,hakuna scating ya Mable,hakuna pvc windows wala bati ya msouth. Hata kama unaunga juhudi sio hivi.
 
Hapo weka na kunywa bia na nyama choma baada ya kikao,pia weka mafuta ya magari ya mabosi waliopo kwenye kikao.
 
Aisee! I was sarcastic sijui wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…