Upinzani bila kubadili siasa mtapata hasara kubwa Kwa Samia..

Wewe nae umekuwa km ndugai! Kutwa humu ulikuwa unamponda jpm! Kipi kilichofanya uchenji gia hewani?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hakuna serikali isiyokuwa na madudu yanayoonekana wazi. Mambo ya kuongelea ni mengi, na mama sio malaika
Nazungumzia matatizo ya wananchi, sijasema yeye atakuwa perfect.

Mfano sasa hivi watu wana matumaini naye kama wafanyabiashara, ajira, wafanyakazi, n.k
Ikionekana ahadi zile zile, miska inakata wakata pesa wanatafuna kina Kakonko na TASAC tayari watu wanapoteza matumaini.
 
Samiah hawezi kuleta katiba unless kama hana interest ya kugombea 2025
 
Wewe mwenyewe umeshakosea . Ni kwanini wapinzani tu ?!. Kwanini siyo pamoja na wewe ?!. Tatizo mnauchukulia upinzani kama ni group fulani hivi , yenye kupigania maslahi Fulani na si ya nchi !!!.

Upinzani si fulani na fulani ni Ile kuwa na idea tofauti na wanaoongoza kwa wakati huo. Jambo ambalo ni la kikatiba na wala si aibu wala utovu wa nidhamu.
 
Samiah hawezi kuleta katiba unless kama hana interest ya kugombea 2025
Siyo Samia tu, hakuna mwanasiasa ataleta katiba ya wananchi.

Kenya, Zanzibar kote huko katiba za wananchi ziliandikwa baada ya wananchi wenyewe kusimama kwa mapigano makali.
 
Ni kweli kabisa
It's either walipaswa wakae kimya huku wakisubiri the right time to attack her as i am sure kila mtawala huwa na flaws ambazo hata wananchi wanaweza kuziona
Ila kwa sasa ni mapema sana wao kupinga as mama ameanza vizuri, ni kama anaonekana atarudisha tumaini lilipotea!sasa wao wanavyopinga na kushambulia inaonekana it,s either hawako wise au wameishiwa hoja so they are just trying so hard to survive
Ni mtazamo wangu tu jamani chondechonde wanachadema msinipopoe kwa mawe manake hamkawii,
 
Mara hii mmeanza kuwatosa Mbowe na Lisu?
 
Maneno ya shimboni yatawaaribia kukutana na Mama SSH. Kujifanya makubwa kwa kutoa amri kwa Rais. Kitu ambacho JPM alikikataa. Hasa chadema
 


Samia kasema atakutana na wapinzani..
Sio Sisi wananchi wa mitandaoni..
Atakapo kutana nao wao ndo Wana nafasi ya kuweka maombi ya wananchi ..na kum influence Samia kuelekea agenda za wananchi..

Sisi tutabaki kupiga kelele Tu huku mitaani na mitandaoni lakini wao wapinzani Wana nafasi kubwa zaidi baada ya Rais kusema atazungumza nao
 
Kwa kweli The Boss umewawekea msingi mzuri upinzani nini wakifanye. Wakifuata ushauri wako basi watachukua nchi 2025.
 
Si kweli,rejea kuagwa kwake,hiyo ndio picha halisi
Wewe ndiyo mmoja kati ya wanaofanya Watanzania wengi waitwe wapumbavu. Yaani maiti imewekwa uwanjani, na Serikali imesema ni mapumziko, kwa nini unashangaa watu wanakwenda kuaga?
Ubora wa mtu haupimwi na watu waliokwenda kuaga kwa kuwa Afrika hata wachawi na wezi huwa tunakwenda kuwaaga.
 
Mwingine eti Mama anaogopa kivuli cha Magufuli, kumbe yeye ndiye bado ameweka "gea ya kupita kwa Magufuli" unajiuliza huyu ni mwanasiasa kweli?
 
Wewe nae umekuwa km ndugai! Kutwa humu ulikuwa unamponda jpm! Kipi kilichofanya uchenji gia hewani?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mimi ni mtu ambae niko open minded, napendela majadiliano ya hoja zaidi.

Nikikukabi leo haina maana kua nitakukubalia daima, mimi sina upenzi na haina maana kua nikikuponda leo basi nitakuponda daima.

Napenda kuona watu wanajenga hoja based on facts and not assumptions or hearsay.

Sasa mtu anapokuja na kuandika uharo eti watanzania walimchoka JPM unajiuliza hao watanzania ni wapi, hawa waliokua wanaandamana hadi kufa kuuona mwili wake?

Maana ukisema watanzania halafu hukuweka specific ni watanzania gani maana yake umewasemea watanzania wote wanaokadiliwa kua 60 million, hilo jambo sio sahihi.

Kwa mfano mimi binafsi sikua nampenda JPM lakini mama yangu alikua anampenda, sasa siwezi kusema kisa mimi simpendi basi Watanzania wote walikua hawampendi, huo ni utaahira. Na usemi ama uandishi wa kitaahira kama huo ndio haukubaliki.
 
Bado ninaamini mpinzani ni kila mtu. Siyo watu special . Wote tunataka maisha bora bila kujali ni mfuasi wa watawala au wa hao uliowaita wapinzani
 
Mama ukimgusa unamuonea ama huna adabu.,interesting times
Ha ha haa!
Wanasahau ujinga hauna jinsia.
Ukiuendekeza jinsia yako sio kigezo
Ni jukumu la upinzani kuukosoa ujinga wa chama kilicho madarakani.

Kuna wajinga wanainama kumuombea mwendazake lakini hawazioni roho walizoziuwa Zanzibar kwa uchu wao wa madaraka.

Ni moja kati ya maujinga ya watawala.

Ipo siku ninyi wapiga matarumbeta wa watawala waovu mtakinywea kikombe kwa majisifu yenu yasiyoisha

kama baba yenu mwendazake alivyokinywea kwa mkono wa Mungu .

Ipo siku kisasi kitawaka juu yenu na nyumba zenu kwa roho zenu za kinyama na uharibifu.

Tubuni sana msijifanye ninyi ndio the blessed!
The untouched!
the rightful to kill!
The soul taker!
The undertaker
The loudest
Ipo siku ya kiama chenu
 
Huna lolote unafiki unakusumbua!

Humpendi jpm halafu kutwa unamtetea humu jamvini tena kwa maneno ya shombo!

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 

Mimi napingana na wewe
Kinachowanyima kiti wapinzani ni tume na sio sera wala jambo lolote

Uchaguzi 2020 ni ushahidi tosha

Halafu kwani huyo CCM ana sera zipi za maana
 
View attachment 1763203
hapa moja ya kiongozi wa upinzani anajaribu kupaka rangi ukuta,usionekane.

ameshindwa kabisa kabisa kusoma alama za nyakati.matokeo yake michango ya wananchi hapo chini imekuwa migumu sana kwa upande wake.
Upinzani wetu hauaminiki kabisa, wengine wakanunuliwa kiurahisi sana kisa kukeep ubunge wao or kuhakikishiwa cheo fulani! When maslahi yao yanapoguswa (Hasa kifedha/mali) wanakuwa wajinga kabisa. Upinzani wa kweli utatoka CCM-Nyerere, hii kauli itatimia siku moja (Almanusura itimie 2015)
 
Mimi napingana na wewe
Kinachowanyima kiti wapinzani ni tume na sio sera wala jambo lolote

Uchaguzi 2020 ni ushahidi tosha

Halafu kwani huyo CCM ana sera zipi za maana
Hili suala la tume na Katiba mpya ni kelele za viongozi wenu ambao hawana dhamira ya dhati ya kuiondoa CCM, ni baadhi ya visingizio ambavyo hawata kosa kuwa navyo hata ikipatikana hiyo Tume. Jambo moja rahisi sana mkuu; Hivi fedha ambazo CDM wamekusanya kama Ruzuku from 2015-2020 wamefanyia nini cha maana (Katika kukijenga chama)? Maana ilikuwa fedha nyingi mnoo, kwa upinzani serious ile fedha ingewatengenezea msingi mzuri sana maana huwezi fanya siasa bila fedha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…