Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Kabisa, ni muda wa kuyashukudia maajabu aliyoahidi jiwe, ni muda wa viwanda vyote moshi kufufuliwa, ni muda wa arusha kuwa California, ni muda wa Tanzania kuwa Ulaya,
maendelo sasa yatakuwa kila mahali na hakika mabeberu watatukoma.
kina lissu kazi yao imetosha, wametutetea sana
Wakae kimya kama hakuna vyama vya upinzani?
 
Watanzania tumekamilisha jukumu letu la kikatiba la kuweka viongozi madarakani na maisha baada ya uchaguzi yameanza.

Sasa tuchakarike na maendeleo yetu binafsi na ya taifa letu tukijua maendeleo hayana chama. Wenzetu wa upinzani sasa tuungane na tushirikiane katika masuala yote yanayogusa maslahi yet bila kujali itikadi ya vyama vyetu.

Kwenye hatua ya maendeleo ama wote tunashinda au wote tunashindwa. Kwa mfano, Tanzania ilipotangazwa kuwa nchi ya kati, wote tulishinda katika ngazi hiyo. Tukubali uchaguzi umeisha.

Ni kweli kibinadamu wengine watakuwa wameumia baada ya matarajio yao kutokufikiwa. Hili ni jambo la kawaida. Tujipe siku mbili tatu hali yetu itarudi kawaida na tuendelee kuchapa kazi. Mungu ibariki Tanzania.
 
Upinzani inabidi wasome alama za nyakati tu kwa sasa, hapa Tanzania hatuna upinzani wa ukweli ni kelele tu zisizo na tija. Mtu anakwenda bungeni kupiga kelele na kuleta bifu ili aandikwe mitandaoni lakini hana msaada wowote jimboni kwake, mfano Halima Mdee, Sugu, Zitto Kabwe, Lissu, na wapuuzi wengine. Tunataka upinzani wa ukweli hapa Tanzania.
Sasa mmebaki wenyewe wenye msaada, shida iko wapi?
 
Naunga mkono hoja:
kwanza kabisa kwa kuwashukuru wapinzani kwa kutupigania na pongezi nyingi sana kwa ccm kwa ushindi usio wa kawaida.
Ingependeza awamu wapinzan wajikite na mishe zao kwenye na kujenga vyama vyao watuache na wateule tuijenge tanzania iwe ulaya.

Naamin kabisa itafika muda hata hatutohitaji msukumo wa wapinzan na kujikuta wananchi wa vyama vyote na wasio na vyama tunaongea lugha moja.

Kumpigania mtu ambaye hayuko tayari sio rahisi na watu wengi hatujajua bado umuhimu wa upinzani bungeni. Naamin hii miaka mitano ya TANU itatufungua akili tulio wengi. Tuombe uzima tu, its just a matter of time
 
Huku mtaani tunafahamu tulio wapigia kura lakini siyo waliotangazwa. Cha kukubali hapa ni kuwa Magufuli aapishwe kama Mfalme wa Tanzania na awe amateur wasaidizi wake kuanzia serikali za mitaa. Tutaokoa pesa nyingi katika maigizo ya uchaguzi.

Tukikubali hali hii it akirudi a tena 2025.
 
Well said.. niko natoa macho na kutega masikio kwa utopolo wa hatari unaoenda kutokea miaka hii 5 na kuendelea, tukianza na kubadilishwa ukomo wa uRais.
 
Tukubali:
1.Hatuwezi tena kukosoa,bali kila kitu itakuwa unaambiwa ni 'maelekezo toka juu'
2.Ukiwa na wazo mbadala,utaambiwa ni 'msaliti'
3.Hakuna tena mtu wa kuidhibiti 'Serikali',hapo ni "ndiooo",hata kama kiongozi anakosea!!!
 
Tukubali:
1.Hatuwezi tena kukosoa,bali kila kitu itakuwa unaambiwa ni 'maelekezo toka juu'
2.Ukiwa na wazo mbadala,utaambiwa ni 'msaliti'
3.Hakuna tena mtu wa kuidhibiti 'Serikali',hapo ni "ndiooo",hata kama kiongozi anakosea!!!
Kipigo walichopsta walio jaribu kuandamana ni onyo kuwa sasa hivi unaiabudu CCM. Na polisi wanao uwezo wa kukufanyia chochote ukipinga maelekezo kutoka juu.
 
Kwenye hatua ya maendeleo ama wote tunashinda au wote tunashindwa. Kwa mfano, Tanzania ilipotangazwa kuwa nchi ya kati, wote tulishinda katika ngazi hiyo. Tukubali uchaguzi umeisha.
Kaa ukitambua kwamba, duniani hakuna mashindano ya kutafuta mshindi wa uchumi wa juu, wa kati na losers! Tambua hilo! Kushinda au kushindwa lipo kwenye maisha yako wewe binafsi, familia yako, ndugu na jamaa na zako, na Watanzania kwa ujumla!

Tuache hao wengine na tuje kwako binafsi: baada ya Tanzania kutangazwa kuwa nchi ya uchumi wa kati, wewe binafsi maendeleo yako yamebadilika kwa kiwango gani tangu Tanzania itangazwe kuingia kwenye uchumi wa kati?!
 
Tukubali:
1.Hatuwezi tena kukosoa,bali kila kitu itakuwa unaambiwa ni 'maelekezo toka juu'
2.Ukiwa na wazo mbadala,utaambiwa ni 'msaliti'
3.Hakuna tena mtu wa kuidhibiti 'Serikali',hapo ni "ndiooo",hata kama kiongozi anakosea!!!
Lakini uzuri ni kwamba, hawa hawa wapumbavu wanaoshangilia hii leo na wenyewe watakuwa ni miongoni mwa waathirika!! Tena bila kwenda mbali, leo hii si wanaumia wote kwenye issue ya internet!!

Serikali wakileta ule uwendawazimu wa bomoa bomoa kama ile ya Morogoro Rd, wote wataumia... wanaopinga hii serikali ya kidhalimu na hawa mazuzu wanaoshangilia!!

Walivyo wapumbavu, donors wakitutupa mkono wataanza kulaumu wapinzani, na hayo yakitokea sote tutaumia!

Na amini usiamini, wanaoongoza ku-support hii serikali ndio hao hao wanaoongoza kwa kuwa na maisha magumu... wengi ni maskini wa kutupwa, wengine wamemaliza vyuo mwaka wa 5 sasa na ajira hawana; yaani full matatizo lakini ndo hayo hayo yanayoongoza kushangilia as if ugumu wa maisha umewatoa akili!!
 
Tusiukubali ujinga uliotokea. Kama raia tutimize wajibu wetu kuhakikisha Taifa letu linaongozwa kwa haki.

Sasa uwe mwanzo wa harakati kubwa za kuukataa udikteta. Tusikome jitihada mbalimbali mpaka siku Taifa letu litakaporudi kwenye misingi ya haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom