Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Mkuu ukizunguka mtaani bado watu hawajaelewa siku wakiona kabisa siku mbili hawana chakula au mtu siku mbili hajui lile Wala lile ndio wore akili zitatukaa sawa.
Mkuu ukizunguka mtaani bado watu hawajaelewa siku wakiona kabisa siku mbili hawana chakula au mtu siku mbili hajui lile Wala lile ndio wore akili zitatukaa sawa.
Wataambiwa kwa sababu hawafanyi kazi ndio maana hawana chakula na papo hapo watajiona hawajala kumbe kwa sababu ya uzembe wao wenyewe na siyo serikali.
 
Sina mengine zaidi ya hayo, heading inajieleza vizuri.

Ni kweli mtakosa mapato, lakini mnaweza kujibidisha na kupata shughuli nyingine hata ikiwezekana kilimo...

Hawa ndiwo wawakilishi waliochaguliwa na wananchi, wananchi wanaipenda sana ccm, sasa nchi yetu inaenda kuwa kama ulaya
 
Jana nimepanda daladala Kuna mama mmoja kachoka tu,kapiga kelele daladala nzima akisifu ushindi na kuuponda vikali Upinzani,jinsi Yule mama alivyochoka hakuna abiria hata mmoja alithubutu kumjibu,daladala ikawa dead silence Kimya Kama tupo kwenye tafakari kuu.Mama akaona hakuna sapoti yeyote akabaki anajiongelesha Kama chizi mwisho akashuka bila abiria yeyote kuongea
Ukute hajachoka wala nini bali ameamua kuwaigizia ili kupima upepo wa makovu ya watu mioyoni mwao.
 
Hapo ndo tungeshuhudia idadi ya wapiga kura kufikia Milioni 70+.Kwa kilichofanyika hata watu wangejitokeza kupiga kura kwa wingi kiasi gani bado shida ingekuwa kwenye kutangaza matokeo ambapo ni kazi inayofanywa na vichwa vichache.Wengine tunakuwa wasikilizaji tu.
Ni vizuri kupiga kura ili kumpa uhalali Kiongozi wa kusema tumeibiwa kura.Sasa usipopiga utasemaje umeibiwa kura.Siku nyingine Kama viongozi wetu watagombea tupige kura kwa wingi ili viongozi wapate sababu ya kusema wameibiwa kura.Uchaguzi huu watu walikata tamaa kabla ya kupiga kura.Nina majirani zangu watano hawajaenda kupiga kura licha ya mie kuwashawishi
 
Wataambiwa kwa sababu hawafanyi kazi ndio maana hawana chakula na papo hapo watajiona hawajala kumbe kwa sababu ya uzembe wao wenyewe na siyo serikali.
Na walivyo wajinga wataamini.Kuna mtu kikokotoo kinaenda kumuathiri keshokutwa tu lakini Ni shabiki kindakindaki humuambii chochote,nikasema watu kama hawa Mungu atusamehe.
 
Ni vizuri kupiga kura ili kumpa uhalali Kiongozi wa kusema tumeibiwa kura.Sasa usipopiga utasemaje umeibiwa kura.Siku nyingine Kama viongozi wetu watagombea tupige kura kwa wingi ili viongozi wapate sababu ya kusema wameibiwa kura.Uchaguzi huu watu walikata tamaa kabla ya kupiga kura.Nina majirani zangu watano hawajaenda kupiga kura licha ya mie kuwashawishi
Kuna kuiba kura na kuna kutangaza aliyeshindwa kuwa mshindi.Hili la pili halitegemei la kwanza.Wizi wa kura ukishindikana basi ni mwendo wa kutangaza aliyeshindwa kuwa mshindi.Kulalamika kuibiwa kura hakujaanza leo na sijawahi kuona impact yake tangible ili kuthibiti wizi huo usijirudie tena.
 
Sina mengine zaidi ya hayo, heading inajieleza vizuri.

Ni kweli mtakosa mapato, lakini mnaweza kujibidisha na kupata shughuli nyingine hata ikiwezekana kilimo...
Wala usiogope, wacha waingie, watatibiana wenyewe, waliyataka wenyewe, bado kisiasa wako wanatambaa, ili ukinzani ukue, lazima wale magwiji wa ccm waingie mle wawape somo, swala wataelewa, maana wale magwiji waliochoka na ccm ndio wanajuwa siasa za ccm na jinsi wanavyohangaika kupata kura ili wale.

Ukinzani ni muda wa kuwafuata kina Makamba, Kinana, Nnape, Mzee Warioba n.k. n.k. Ama sivyo mkibaki na siasa za uanaharakati wa kina fulani kulewa na faru john na kukesha kupewa fadhila na wabunge wa kuteuliwa sidhani kama watafanikiwa.

Ila watasikia?!
 
Tatizo si Wananchi bali Serikali imeamua kuwa upande wa CCM
 
Acha Kupiga Mayowe Acha Waione Wenyewe
Maji Tutaita Mmaa!!!😁😂😅😄😐
Huzuni Imetanda Tanzania!!
 
Na walivyo wajinga wataamini.Kuna mtu kikokotoo kinaenda kumuathiri keshokutwa tu lakini Ni shabiki kindakindaki humuambii chochote,nikasema watu kama hawa Mungu atusamehe.
Ukiona hivyo basi kuna uwezekano Mkubwa kwamba kwenye huo ushabiki wake anapata manufaa makubwa kuliko ya 'kikokotoo' hivyo hatajali maadam manufaa ya ushabiki wake hayataguswa.
 
Ukiona hivyo basi kuna uwezekano Mkubwa kwamba kwenye huo ushabiki wake anapata manufaa makubwa kuliko ya 'kikokotoo' hivyo hatajali maadam manufaa ya ushabiki wake hayataguswa.
Namfahamu vizuri,katika ofisi yao wale wote wanaofanya kazi pamoja naye Ni yeye tu ndio yupo ovyo na hajajiandaa kwa namna yeyote ile kwa maisha ya badaye.
 
Yule Mama alileta Simanzi kwenye daladala.Halafu nimegundua Kuna wanaCCM wengi nao wameanza kulalamika walitegemea kutakuwa angalau na mchanganyiko kidogo
Hapana waambie wasilalamike nakumbuka Yesu alisema "ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake utawezaje kusimama?". Wakiwa wenyewe ndo mambo yao yataenda kama watakavyo.Hakuna kikwazo tena.
 
Tatizo si Wananchi bali Serikali imeamua kuwa upande wa CCM
Wananchi nao Ni jipu.Pita pita mtaani uliza washabiki wa chama Tawala wapo wengi mno japo baada ya uchaguzi hawataki tena kujionesha maana wanajua yajayo yanatisha.Hapohapo pita pita mtaani uliza ambao hawakupiga kura sababu ya kukata tamaa wapo wengi mno
 
Namfahamu vizuri,katika ofisi yao wale wote wanaofanya kazi pamoja naye Ni yeye tu ndio yupo ovyo na hajajiandaa kwa namna yeyote ile kwa maisha ya badaye.
Usiseme kwamba unamfahamu vizuri ndugu.Manufaa siyo lazima yawe yanayoonekana kwa muda huo.Wengine wanaishi kwa matumaini ya ahadi kemkem walizoahidiwa. Wengine wanapata ajira kutokana na huo ushabiki n.k.Mambo ni mengi rafiki.
 
Back
Top Bottom