Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Uchaguzi 2020 Upinzani, msiende mahakamani wala msihamasishe watu kuingia barabarani. Tuacheni Wananchi tuyaone wenyewe

Upinzani inabidi wasome alama za nyakati tu kwa sasa, hapa Tanzania hatuna upinzani wa ukweli ni kelele tu zisizo na tija. Mtu anakwenda bungeni kupiga kelele na kuleta bifu ili aandikwe mitandaoni lakini hana msaada wowote jimboni kwake, mfano Halima Mdee, Sugu, Zitto Kabwe, Lissu, na wapuuzi wengine. Tunataka upinzani wa ukweli hapa Tanzania.
sasa watavurugana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama chao,mitandao ya kusaka urais inaanza soon mwenyekiti hatakuwa na nguvu kuyadhibiti makundi ndani ya chama chake,daima upinzani upo upo tu hata ndani ya chama chake.

Hakuna alichokifanya kuua upinzani,kafanikiwa kudhibiti miamba ya upinzani isiwepo bungeni wataibuka wa chama chake humo humo ndani huku yeye akijiandaa kumaliza muhula wake wa pili
 
Upinzani inabidi wasome alama za nyakati tu kwa sasa, hapa Tanzania hatuna upinzani wa ukweli ni kelele tu zisizo na tija. Mtu anakwenda bungeni kupiga kelele na kuleta bifu ili aandikwe mitandaoni lakini hana msaada wowote jimboni kwake, mfano Halima Mdee, Sugu, Zitto Kabwe, Lissu, na wapuuzi wengine. Tunataka upinzani wa ukweli hapa Tanzania.
Kweli tupu.
 
Elimu ndogo kwa wapiga kura nayo imechangia kupunguza kura kwa wapinzani,wengi wao neno UPINZANI wanalielewa vibaya,wanaona ni kitu cha hatari sawa na ugaidi,mpiga mwenye uelewa mdogo hapigii kura mpinzani anaona anachagua kitu hatari.Elimu ya uraia ni ndogo kwa wapiga kura wengi
 
sasa watavurugana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama chao,mitandao ya kusaka urais inaanza soon mwenyekiti hatakuwa na nguvu kuyadhibiti makundi ndani ya chama chake,daima upinzani upo upo tu hata ndani ya chama chake.Hakuna alichokifanya kuua upinzani,kafanikiwa kudhibiti miamba ya upinzani isiwepo bungeni wataibuka wa chama chake humo humo ndani huku yeye akijiandaa kumaliza muhula wake wa pili
Sidhani kama anajiandaa kuishia muhula huu huu tu.Bunge lote kijani.Unadhani kwa ajili gani?
 
Miaka 5 inafikiri ni mchezo? Hawa watumishi waliosaidia ccm kufanya uharamia huu ndyo watapata pigo la kwanza.
Watu wanaoipa ushindi CCM siku zote Ni hawa.
1.Watumishi wa Serikali hasa wale wa kuteuliwa wanaokula keki ya nchi.Hapa toa watumishi wa ngazi za chini.

2.Wapinzani wote ambao huwa wanapuuzia zoezi la kupiga kura.Hawa nao wanapaswa kulaumiwa kwa kuhujumu Upinzani.

3.Bodaboda,madereva Bajaj na wamachinga,wamama watu wazima nao wamechangia pakubwa.

4.Watu wengi wasiojua kusoma,wanyonge wote ambao upatikanaji wa mkate kwao Ni kwa kuunga unga hawa wengi wanapigia chama Tawala.

Siku tukipigika kuzidi maelezo ndio tutapata akili
 
Huku mtaani tunafahamu tulio wapigia kura lakini siyo waliotangazwa. Cha kukubali hapa ni kuwa Magufuli aapishwe kama Mfalme wa Tanzania na awe amateur wasaidizi wake kuanzia serikali za mitaa. Tutaokoa pesa nyingi katika maigizo ya uchaguzi.

Tukikubali hali hii it akirudi a tena 2025.
Mkuu licha ya kuwa huenda kulikuwa na uchakachuzi lakini Kuna kundi kubwa la watu wasiopiga kura linapaswa kulaumiwa.Ujue Kama mtu hupigi kura unampa nguvu na kiburi mchakachuaji kufanya yake
 
Tukubali:
1.Hatuwezi tena kukosoa,bali kila kitu itakuwa unaambiwa ni 'maelekezo toka juu'
2.Ukiwa na wazo mbadala,utaambiwa ni 'msaliti'
3.Hakuna tena mtu wa kuidhibiti 'Serikali',hapo ni "ndiooo",hata kama kiongozi anakosea!!!
Unampa mawaz mbadala mtu mjuaji ya Nini?
 
Sina mengine zaidi ya hayo, heading inajieleza vizuri.

Ni kweli mtakosa mapato, lakini mnaweza kujibidisha na kupata shughuli nyingine hata ikiwezekana kilimo....
Kukosekana maendeleo nchi nzima kusababishwe na upinzani! Hao wananchi wanaojitambua wako wapi?
 
Mkuu licha ya kuwa huenda kulikuwa na uchakachuzi lakini Kuna kundi kubwa la watu wasiopiga kura linapaswa kulaumiwa.Ujue Kama mtu hupigi kura unampa nguvu na kiburi mchakachuaji kufanya yake
Hapo ndo tungeshuhudia idadi ya wapiga kura kufikia Milioni 70+.Kwa kilichofanyika hata watu wangejitokeza kupiga kura kwa wingi kiasi gani bado shida ingekuwa kwenye kutangaza matokeo ambapo ni kazi inayofanywa na vichwa vichache.Wengine tunakuwa wasikilizaji tu.
 
Mkuu licha ya kuwa huenda kulikuwa na uchakachuzi lakini Kuna kundi kubwa la watu wasiopiga kura linapaswa kulaumiwa.Ujue Kama mtu hupigi kura unampa nguvu na kiburi mchakachuaji kufanya yake

Lakini ktk kuhesabu kura ni nyingi sana pamoja na watu kuto kwenda Mungu fundi
 
Jana nimepanda daladala Kuna mama mmoja kachoka tu,kapiga kelele daladala nzima akisifu ushindi na kuuponda vikali Upinzani,jinsi Yule mama alivyochoka hakuna abiria hata mmoja alithubutu kumjibu, daladala ikawa dead silence Kimya Kama tupo kwenye tafakari kuu.

Mama akaona hakuna sapoti yeyote akabaki anajiongelesha Kama chizi mwisho akashuka bila abiria yeyote kuongea
 
Back
Top Bottom