Upweke umewaanza vijana mapema, Uzeeni sijui itakuwaje. Ni janga kubwa

Upweke mara nyingi huwapata watu wanofanya mambo kutoka katika msukumo wa nje na sio ndani.

Vijana wengi husukumwa na msukumo wa nje na sio wa ndani hivyo wamejikuta wanakimbizana na mambo ambayo hayana maana kwao wakiamini yatawapa furaha na faraja.

Kuwa innocence , ndo watibeli kuishikilia Haki, Upendo ndo unyongofu. Na huwezi kurogwa na MTU yeyote wala kuuona upweke.


Na kuwa Guilty ni njia rahisi ya kushusha layer , kuwa mpweke hadi kurogwa kirahisi.



Innocence = The meaning life and ur presence

Guilty= Absence and the all negativity under the roof of depression
 
MTIBELI🙂....treekengele
 
Vijana kwa Kiasi kikubwa wanaona pesa ndiyo kila kitu. Ni shida kubwa mnooo ina tutesa.
 
Ule utulivu wa akili niupatao kila nirudipo nyumbani kutoka kwenye mizunguko yangu sipo tayari kuuza kwa gharama ya ndoa. I can't imagine nirudi nyumbani alafu mtu aanze kuniongelesha ongelesha unless niwe nimelewa
 
Siwezi kua mpweke wakati wanawake wazuri (nyumbu) wenye shape wamejaa mtaani[emoji23][emoji23] mapigo na mwendo
 
Mkuu,

Kwanini kuchukua mifano yenye matokeo hasi tu na si pamoja na ile yenye matokeo chanya?, je mama yako, au baadhi ya ndugu zako wa kike wote ni matapeli kama unavyoamini?.

Ni kweli kuna changamoto ya ndoa kwa kizazi cha sasa haswa ukizingatia ukuaji wa teknolojia, utandawazi na kuporomoka kwa maadili katika jamii. Hili jambo linawakumba watu wa jinsia zote, wake kwa waume. Ndo maana unashangaa vijana wanakwambia hakuna wanawake wa kuoa kwa sasa, na mabinti nao wanalalamika hakuna wanaume wa kuolewa nao kwa sasa.

Kikubwa katika haya maisha ni kufanya sala kwa imani yako, tumia utashi wako vizuri na naamini utampata aliye bora.

Sio kila uwezalo lifanya sasa ukiwa unatembea mzima, utalifanya ukiwa mgonjwa kitandani. Sio kila kitu watakusaidia ndugu na wazazi wako au jamaa zako, au wauguzi. Kuna wakati pesa haiwezi kufanya kila kitu, na katika hayo inayoweza kufanya hayatakuwa kwa upendo.

Ukipata changamoto za ugonjwa na umri mkubwa hilo unaweza lielewa. Kuna wakati watu hawatakuwa na time na wewe, watafocus na maisha yao. Upweke is real.
 
Ujinga tu mnajazwa mitandaoni.

Tupe historia ya maisha ya NDOA ya wazazi wako kabla hujasoma NDOA haifai,

Ukute chanzo ni familia uliyokulia.
Nadhani watu wengi wanao angukia katika kundi hili ni matokeo ya past trauma alizoziona akikua, au ni issue za family background, au ni mambo aliyoyapitia yeye mwenyewe.

Kuna wakati watu wakipitia hali hii wanapaswa kupata utabibu wa kisaikolojia.
 
Ukipata changamoto za ugonjwa
ndiyo maana kuna hospitali mzee
kwa ivyo mnaoa ili msaidiwe mkiwa wagonjwa ?
Afrika bana

mwenzako huyu hapa kaliwa nusu ya mali zake kwa upumbavu wa ndoa

 
Wengi wamepigwa na kitu kizito kichwani.
Japo pia,walio na ndoa ama familia pia wapo wanaohangaika mpaka wanatamani siku zingerudi nyuma waanze upya kwenye kuchagua wenza.

Unakuta familia Ina Kila kitu,ila Mwanaume kurudi home usiku,kutoka alfajili na mapema.

Anakaa masaa kama 5.
Hivyo msongo kama upo Kwa mgawanyo mkuu.
Kikubwa amini kile kinachokufaa.
Maisha ni mahesabu.
 
Wewe umelichukulia kwa upande wa ugonjwa. Hiyo ni sehemu kidogo sana ya maana nzima ya yaliyo andikwa. Hospital zipo na zinatibu wagonjwa, sijui kama umewahi kuwa na mgonjwa anayehitaji huduma ya karibu na ukamuhudumia akiwa hospitali au hali hiyo kukupata wewe?.

Nimeuliza, je mama na ndugu zako nao unawaweka kwenye kundi hilo hilo?, kwa maana ni kweli mzazi wako wa kike alikuwa na tabia unazotuambia kuwa wanawake wote wanazo?, je ni kweli ndugu zako wote wa kike wana tabia kama za wanawake unawazungumzia?.

Je unajua umuhimu wa makuzi ya baba ndani ya nyumba/jamii (father figure). Amini nakwambia, kuna wakati tunachangia kutengeneza jamii dhaifu ya vizazi vijavyo kwa ajili tu ya mitazamo yetu hasi kuhusu hii taasisi.


Labda uniambie kwa mtizamo wako, huna sababu ya kuoa na wala huna sababu ya kuwa na watoto. Kama una sababu ya kuwa na watoto, embu wape nafasi ya kulelewa katika nafasi ya kuwa na mwanaume kiongozi katika maisha yao.

Hii inaenda hata kwa wale wanaosema nitazaa tu, nitalea mwenyewe kwakuwa ninajiweza. Tunatengeneza jamii ambayo baadaye itapata changamoto nyingi sana huko mbeleni.

Hili unaweza kuliona lina mantiki kama hatuta lizungumza kwa ushabiki.
 
Ndoa zilikuwa zamani
Sasa Ni Utapeli , Ni Ujambazi na ni Wizi mtupu
Wacha wajinga wapigwe
 

Sahihi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…