Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Magufuli hana ubavu wa kujiongezea muda akitaka kuona nguvu ya jeshi(JWTZ) na mataifa kama Marekani aje ajaribu atabinywa kende mwaka mmoja tu anakimbia Ikulu au anapinduliwa.

Ni vigumu sana kuirudisha nchi ambayo ishaonja mfumo wa democrasia kwenye utawala wa kidicteta wao waendelee tu kumdanganya ila atambue Jeshi halihongwi hata siku moja ukiwapa pesa ndio wanataka zaidi na zaidi tena kwa masharti.

Wanaotegemea jeshi litawasaliti wananchi polen sana, Msimdanganye mwenzenu watu wakaja kumuokota kwenye mtaro siku moja.

Unaota wewe!!

Ameshaikamata jeshi wewe

Wanampenda sana
 
Mkuu hili baraza la maaskofu katoliki (tec) limekuwa kama kikundi cha wahuni kabisa..
Serikali hii ya awamu ya 5 inafanya mambo mengi ya ovyo hasa ya kusigina Katiba na haki za raia lakini wapo kimyaa kabisa..
Lakini wakati wa jk ilikuwa kila siku kumpa presha mzee wa watu..
MUNGU ni wa watu wote na Mungu huwa hachezewi..kuna pigo kuu linakuja kwa utawala huu.

Mbona Kila pasaka wamekuwa wakitoa waraka kuisema serikali au mmesahau??

Spika kwani aliongea lini mpaka muone hawajasema?

Na je watakuwa wanajibizana na maneno ya spika bila kusubiri action?
 
Wakati wa Kikwete hawa walipokuwa wanatoa matamko hamkuwasikia?Wao ni Sawa kumtukana Rais muislam? Lakini akiingia mkristo wao wakikaa kimyaa tuliwauliza vipi?Sisi ndo tuna changanya dini na siasa?
Hujawasikia kina Shay? Mbona wapo wengi Tu? Kumbuka tawala hazilinganishwi hivyo, alivyotawala JK si sawa na anavyotawala JPM.
 
Kwani yale waliokuwa wakipigia kelele na nyaraka kila siku kipindi cha JK, kwani ndiyo hayo hayo yanayofanyika sasa na bwana MAGU?
Hili swali wakukujibu ni umma mohamad, wazee wa udini (kila jambo kwao linawekwa kwenye mtazamo wa kidini)
 
Hoja ya kuwahusisha viongozi wa dini, na hasa Kanisa Katoliki, ni ya msingi.
Sababu ni kwamba kiongozi mwandamizi wa Kanisa Katoliki wakati huo, Kardinali Pengo, alijitutumua sana kukosoa serikali za marais Mwinyi na Kikwete, lakini akawa bubu kwa serikali za Mkapa na Magufuli. Na kwa serikali ya Magufuli ndio kabisaaa Pengo alifikia hatua ya kujitoa ufahamu kabisa, na kuwasifia hata wapambe wa Magufuli, mtu kama Makonda! Kwa nini wawakosoe marais Waislamu tu? Huo ni Udini!
Shida kubwa mliyonayo baadhi ya waislamu ni udini uliopindukia, kila jambo kwenu mnalitazama kwa mlengo wa kidini

Kanisa Katoliki likikukosoa ama kukupongeza ni kwa kutumia facts, mitazamo ya kipuuzi (jicho la udini) iko kwa waislamu 'baadhi'
 
Pengo alishastaafu
Kweli Pengo amestaafu, lakini inaonekana alijenga mtandao wa wenye msimamo kama wake. Hata ukilitizama Kanisa Katoliki la Tanzania hivi sasa, mwelekeo ni ule ule
 
Shida kubwa mliyonayo baadhi ya waislamu ni udini uliopindukia, kila jambo kwenu mnalitazama kwa mlengo wa kidini

Kanisa Katoliki likikukosoa ama kukupongeza ni kwa kutumia facts, mitazamo ya kipuuzi (jicho la udini) iko kwa waislamu 'baadhi'
Jenga hoja, usijifiche kwenye blanketi la stereotyping. Kwa taarifa yako, mimi ni Mkatoliki safi kabisa. Naamini kwa dhati kwamba Kanisa ni Takatifu kwa sababu Bwana Yesu, ambaye ndio kichwa cha Kanisa, ni Mtakatifu. Naamini pia kwamba Kanisa ni lenye Dhambi kwa sababu viungo vya kanisa, waamini, ni wadhambi. Hivyo sishangai kwamba mtu mkubwa kama Kardinali Pengo, anafanya makisa tena hadharani.
Shida kubwa mliyonayo baadhi ya waislamu ni udini uliopindukia, kila jambo kwenu mnalitazama kwa mlengo wa kidini

Kanisa Katoliki likikukosoa ama kukupongeza ni kwa kutumia facts, mitazamo ya kipuuzi (jicho la udini) iko kwa waislamu 'baadhi'
Sasa nikikuambia kwamba mimi ni Mkatoliki saaafi, utasemaje? Usifikiri kila anayekosoa viongozi wa Kanisa kwa makosa wanayofanya dhidi ya marais waislamu, ni muislamu. Mimi ni mpenda haki, nina ndugu zangu waislamu kwa wakristu.

Hujaona katika sakata la maandamano kupinga ubaguzi dhidi ya watu weusi duniani, kuna idadi kubwa ya " whites" ambao ni wapenda haki, wameguswa na hizo dhulma?

Hizo facts unazosema, zinatakiwa ku apply kwa wote.
Kanisa Katoliki halijakosoa chochote katika utawala huu. Kulikuwa na Waraka wa Kwaresima mwaka juzi, ambao ulifanya kile tulichotarajia, lakini Kardinali Pengo akaukana, na kuukosoa kwamba hauko sahihi.
 
Sahihi kabisa, wanataka sadaka zetu lakini hawakemei uovu! Ni wanasiasa wa madhabahuni
Bila kukemea uovu pa kichafuka je watapata wapi sadaka.
Eas Africa viongozi wa dini wapo Kenya, angalau Congo walipiga kelele Kabila akaona aibu.
Wangewatenga na kuwafuta uumini na kuwapiga marufuku kuingia nyumba zao za ibada, wangeacha uovu.Mtu muovu usipomtenga ataendelea kufanya uovu wake bila hata kuogopa madhabau au mimbari.
 
Sahihi kabisa, wanataka sadaka zetu lakini hawakemei uovu! Ni wanasiasa wa madhabahuni
Uovu Hadi ufanywe na ambae sio mkatoliki
Akiwa mkatoliki wanakaa kimyaa
 
Naona chadema mmeamua mtutegemee waislam na bakwata kumziwia magufuli polen sisi tunasema ivi hii nchi haina din tumuache magufuli atawalale
 
Kweli kabisa jeshi haliwez kuwasalit Wana nch pia haliwez kupinga maoendekezo ya wananch so nyie msubir tu dawa iwaingie
Magufuli hana ubavu wa kujiongezea muda akitaka kuona nguvu ya jeshi(JWTZ) na mataifa kama Marekani aje ajaribu atabinywa kende mwaka mmoja tu anakimbia Ikulu au anapinduliwa.

Ni vigumu sana kuirudisha nchi ambayo ishaonja mfumo wa democrasia kwenye utawala wa kidicteta wao waendelee tu kumdanganya ila atambue Jeshi halihongwi hata siku moja ukiwapa pesa ndio wanataka zaidi na zaidi tena kwa masharti.

Wanaotegemea jeshi litawasaliti wananchi polen sana, Msimdanganye mwenzenu watu wakaja kumuokota kwenye mtaro siku moja.
 
Izi Uzi zinazid kuonyesha NI kwa jinsi gani chadema mmebaki wenyewe kwenye mapambano yenu kila mtu kawadharau tayar
 
Unataka waraka kila kunapokuwa na jambo, mbona taasisi zipo nyingi wasipotoa wao watatoa wengine. Kama nakumbuka vizuri TEC walitoa waraka wakati wa kwaresma, hilo unalo lizungumzia limetokea lini? Na unadahani kila jambo TEC watalitolea waraka kesho yake asubuhi? TEC ni taasisi yenye maaskofu 33, huwezi ukawakusanya maaskofu wote hao kwa usiku mmoja. Kama ni suala linalogusa maslahi mapana ya taifa watazungumza tu, muda ndo hakimu mzuri. Mara ya mwisho nakumbuka waliongelea kuhusu haki sawa katika uwanja wa siasa. Subiri
 
SUBUTU, Marekani mwenyewe anagwaya maana hatuombi msaada kwake! na hilo la Jeshi sahau kabisa, majaribio yote yaliyofanywa wakati wa Nyerere yaliishia wapi? Unafikiri JPM ni mjinga kushindwa kulidhibiti jeshi mapema?
Hizo ARV unazopewa na marekani sio msaada, na vip zile billion za corona ulizopewa na marekani, na unajua project anazofanya USAID Tanzania ni nyingi sana usingeongea huo Ujinga ulioongea

Nyerere mambo yalimshinda akang'atuka 1985, inaonekana kiumri ni mdogo na hujui mambo mengi
 
pole sana; jaribu kusoma post yangu tena kwa makini, soma katikati ya mistari - JPM siyo mjinga.................
 
Back
Top Bottom