Pre GE2025 Uropokaji wa Tundu Lissu ni kilema hawezi kubadilika. Tumkatae kabla hajaleta maafa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wafuasi wa Tundu Lissu wamekuwa wakimtetea huyu 'masia' wao kuwa ni mkweli, kanyooka, penye nyeusi anaita nyeusi, ni msafi.

Lakini siku zinavyozidi kwenda inajidhiilisha Tundu Lissu sio mkweli bali ni mropokaji.
Lissu anaropoka jambo lolote ambalo anahisi wafuasi wake watapenda kulisikia na litamuongezea political mileage.

Lissu sio mwanasiasa mwenye mipango madhubuti yeye anategemea mdomo, kuwatukana na kudhalilisha wengine ili yeye akue. Lakini hawezi kufanya mikakati ya kiuongozi na kisiasa.

Viongozi waropokaji kama Tundu Lissu ni hatari kwa usalama wa taifa. Ni wepesi sana kuchochea machafuko ili wapate upenyo wa kushika madaraka hawajui mbinu nyingine za ziada zaidi ya kuropoka na kuchochea vurugu.

Adolf Hitler aliingiza dunia kwenye vita ya dunia kwa sababu ya kuropoka sana na kuchochea ubaguzi. Alipata alichokitaka.

Nduli Iddi Amini nae alikuwa mropokaji mzuri sana ilifikia wakati aliichimba mkwara mpaka Uingereza na mashabiki wake walikuwa wanamshangilia sana. Lakini Nyerere alimpa kinachomstahili.

Hapa Tanzania tulikuwa na Mtikila alikuwa ni mropokaji kama Lissu na Lissu ni kama anaenda kuwa Mtikila mpya baada ya huu uchaguzi wa Chadema. Mtikila ilifikia wakati akaaminisha mashabiki wake kuwa wahindi ndio tatizo kwenye hii nchi yani uwepo wa wahindi ndio unasababisha waswahili wasiendelee. Mtikila mpaka anafariki alikuwa mwanasiasa wa hovyo kabisa sababu ya uropokaji.

Sasa huyu tulie nae anaitwa Tundu Lissu ni tatizo sio tu kwenye chama chake cha Chadema bali ni tatizo kwa taifa. Huyu jamaa anaropoka sana mpaka amepitiliza. Sijui hata wafuasi wake kama wanapata picha huyu jamaa ataenda kuongozaje chama kwa tabia za namna hiyo. Kwa uropokaji wa Lissu hawezi kuongoza chama kikawa kimoja hajui kuunganisha watu anachoweza ni kubomoa.

Ameshatoa kauli zinazoenda kuua chama anachotaka kukiongoza lakini kama haitoshi ametoa kauli nzito zinazoweza kuhatarisha umoja na amani ya taifa letu.

Kauli zake kuhusu kikao cha faragha na viongozi wa kidini zinatosha kabisa kusema huyu mropokaji hafai kuwa kiongozi na ni hatari na ikiwezekana akapimwe utimamu wa ubongo wake maana hii sio kawaida.

Shukrani Mbowe kwa maono yako, umechagua maslahi ya taifa over upepo wa mihemko.

Mkishammaliza uko chadema kazi yake huku nje ni nyepesi. Maana hatopata tena platform ya kufanya uropokaji wake na akachukuliwa serious.

#KataaMropokaji
Sio Lisu pekee mbona Kuna mwingine Aliwahi kuwa Rais,mlikuwa wapi kumkataa mapema?
 
Kama ni mropokaji na mlijua hilo, Abdul alikwenda kutafuta nn kwake??? Watz siyo wajinga.
Abdul alienda kwake kwa sababu alikaribishwa akuvamia.

Alafu Lissu sio kiongozi wa kwanza nchi hii kuongea na mtoto wa Rais. Yeye ni mropokaji ndio maana kaona ni ajabu.

Viongozi wa upinzani wanaongea na marais, wanaongea na viongozi wa dini, wanaongea na mabalozi, wanaongea na watu wa juu wa usalama. Ila wanakausha kiume.

Lissu kwa uropokaji ule huwezi kuwa na trust ya kuongea nae jambo lolote la siri.
 
Ni mkweli asiyepindisha maneno, watu wa ukweli wanamtaka. Ya nini kuwa na kiongozi mwenye siri za ajabuajabu? Wenye makandokando wanamuogopa sana huyu mwamba lissu
Top secrets ndio zinaongoza nchi kama unakuwa kiongozi ila hauna koromelo basi hufai kabisa kuongoza taasisi yoyote kubwa.
 
huko juu hajafika, akifika anajua code zinazoongoza nchi, kuna siri hutakiwi kuzitoa hata kidogo mpaka unakufa
 
Lissu ameshakuwa public figure anajiandaa kuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani na mgombea urais maana yake ikitokea bahati mbaya anaweza kuangukia kwenye urais. Kama hawezi kutunza siri in a process maana yake hico ni kilema hakitakaa kipone hivyo ni hatari kwa national security.
 
Itakuwa ajabu na wendawazimu ikiwa wajumbe wa mkutano mkuu watakengeuka na kuamua kumchagua mgombea anayeungwa mkono na washindani wao kisiasa na wakamuacha huyo wanayemuhofia.Wajumbe mkifanya hivyo dhambi hiyo haitawaacha salama itawatafuna mpaka kizazi chenye cha tatu
 
Nipo tayari kwa mdahalo na yoyote muda wowote.
Peleka upuuzi mdahalo na lissu akimbie mbowe we sisimizi utaweza?!.
Team Nkurunzinza mmeumia sana baada ya lissu kuanika madhaifu ya bwana enu eeh mlitaka asiseme ukweli
Kama kusema ukweli ni kuropoka ndio tunamtaka kiongozi wa aina hii tofauti na msiri mbowe anayetuuza kwa mama abdul.
 
Lissu ameshakuwa public figure anajiandaa kuwa mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani na mgombea urais maana yake ikitokea bahati mbaya anaweza kuangukia kwenye urais. Kama hawezi kutunza siri in a process maana yake hico ni kilema hakitakaa kipone hivyo ni hatari kwa national security.
akiwa rais ataapa kulinda siri za nchi. Why aropoke kutoa siri za nchi wakati ana maofisa usalama wa taifa? Kwenye huu mtifuano ni kampeni tu ajiweke front vew kwa wapiga kura wake dhidi ya mpinzani wake
 
Tundu Lissu ni mropokaji sio mkweli, angekuwa mkweli tungemsikia kwenye uchaguzi wa 2015 kwenye mchakato wa kumkaribisha Lowassa kwenye chama kulikuwa na mambo mengi ya hovyo lakini kwa kuwa alikuwa sehemu ya wanufaika pesa ilimfumba mdomo wake mrefu.
Ukipata kusikia hiyo ya 2015 ndipo utahamishia Timu yake kabisa. Kilichofanyika na kukubali kutokubaliana ili taasisi iendeleee
 
Kabla hajaanza kumuumbua dikteta uchwara Mbowe mbona haujawahi kusema Lissu ni mropokaji?
 
Inawezekana kweli ndivyo alivyo ila kwa watu smart hiyo ni mbaya.Wakigundua friji lako haligandishi watakukwepa.tatzo la watanzania tunapenda kuongea zaidi kuliko kutenda.yaani mtu ukijua kupiga mdomo vizuri ndio unaonekana unafaa kua kiongozi bila kujua kuongea na kuongoza ni vitu tofauti.Wafuasi wake wanaamini kelele zake zitawaogopesha ccm wanasahau kua ccm haiogopi wapiga kelele.Mtikila alikua mpiga kelele na mjenga hoja mzuri na jasiri kuliko lissu na ccm waliishia kumtazama tu abwabwaje uku wakifanya mambo yao.Labda wengine walikua hawajazaliwa ndo maana wanamuona lissu kama tumaini lao.ngoja tuone muda utatuambia zaidi.
 
Wafuasi wa Tundu Lissu wamekuwa wakimtetea huyu 'masia' wao kuwa ni mkweli, kanyooka, penye nyeusi anaita nyeusi, ni msafi.

Lakini siku zinavyozidi kwenda inajidhiilisha Tundu Lissu sio mkweli bali ni mropokaji.
Lissu anaropoka jambo lolote ambalo anahisi wafuasi wake watapenda kulisikia na litamuongezea political mileage.

Lissu sio mwanasiasa mwenye mipango madhubuti yeye anategemea mdomo, kuwatukana na kudhalilisha wengine ili yeye akue. Lakini hawezi kufanya mikakati ya kiuongozi na kisiasa.

Viongozi waropokaji kama Tundu Lissu ni hatari kwa usalama wa taifa. Ni wepesi sana kuchochea machafuko ili wapate upenyo wa kushika madaraka hawajui mbinu nyingine za ziada zaidi ya kuropoka na kuchochea vurugu.

Adolf Hitler aliingiza dunia kwenye vita ya dunia kwa sababu ya kuropoka sana na kuchochea ubaguzi. Alipata alichokitaka.

Nduli Iddi Amini nae alikuwa mropokaji mzuri sana ilifikia wakati aliichimba mkwara mpaka Uingereza na mashabiki wake walikuwa wanamshangilia sana. Lakini Nyerere alimpa kinachomstahili.

Hapa Tanzania tulikuwa na Mtikila alikuwa ni mropokaji kama Lissu na Lissu ni kama anaenda kuwa Mtikila mpya baada ya huu uchaguzi wa Chadema. Mtikila ilifikia wakati akaaminisha mashabiki wake kuwa wahindi ndio tatizo kwenye hii nchi yani uwepo wa wahindi ndio unasababisha waswahili wasiendelee. Mtikila mpaka anafariki alikuwa mwanasiasa wa hovyo kabisa sababu ya uropokaji.

Sasa huyu tulie nae anaitwa Tundu Lissu ni tatizo sio tu kwenye chama chake cha Chadema bali ni tatizo kwa taifa. Huyu jamaa anaropoka sana mpaka amepitiliza. Sijui hata wafuasi wake kama wanapata picha huyu jamaa ataenda kuongozaje chama kwa tabia za namna hiyo. Kwa uropokaji wa Lissu hawezi kuongoza chama kikawa kimoja hajui kuunganisha watu anachoweza ni kubomoa.

Ameshatoa kauli zinazoenda kuua chama anachotaka kukiongoza lakini kama haitoshi ametoa kauli nzito zinazoweza kuhatarisha umoja na amani ya taifa letu.

Kauli zake kuhusu kikao cha faragha na viongozi wa kidini zinatosha kabisa kusema huyu mropokaji hafai kuwa kiongozi na ni hatari na ikiwezekana akapimwe utimamu wa ubongo wake maana hii sio kawaida.

Shukrani Mbowe kwa maono yako, umechagua maslahi ya taifa over upepo wa mihemko.

Mkishammaliza uko chadema kazi yake huku nje ni nyepesi. Maana hatopata tena platform ya kufanya uropokaji wake na akachukuliwa serious.

#KataaMropokaji
Tofautisha kati ya kuropok na kuongea facts. Mi nachojua lisu hapepesi macho kwenye rushwa yoyote hata rushwa za mbowe kwa mademu wale atasema tu
 
Inaonekana TAL kama anawachachafya sana..... Kila wakati mnamwandama....
 
Back
Top Bottom