Urusi kupeleka majeshi yake na silaha nzito nchini Cuba na Venezuela kama Marekani itaendelea na kujiingiza Ukraine

Nchi zote za NATO ziliunga na zinaunga mkono mipango ya kumtoa Assad madarakani, wanachotofautiana ni level of commitment baina ya nchi moja na nyingine kuhakikisha huo mpango unafanikiwa.

Nchi zilizokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Assad anatoka ni Marekani, Britain, France, Turkey na Israel wakisaidiwa na Saudi Arabia, UAE na Qatar.

Kwa case ya Britain, serikali yao ilisema bungeni kuwa inafadhili na kufundisha vikundi vya kigaidi wenyewe wanaviita "moderate rebels" kwa ajili ya kupamba na ISIL na kuitoa serikali madarakani( kimsingi ndio lengo kuu).
https://questions-statements.parliament.uk/written-questions/detail/2018-04-13/135396
hili ni jibu la waziri bungeni. Pia kuna Case mshtumiwa wa ugaidi ilibidi waendesha mashtaka wa Uingereza waifute kwa kuwa mshutumiwa huyo wa Ugaidi alikuwa sehemu ya vikundi vinavyofadhiliwa na serikali ya Uingereza kumtoa Assad.

Nchi zote nilizotaja hapo juu zinafadhili hivi vikundi kwa ajili ya kumtoa Assad.

Pia unaweza kupitia hii "Operation Timber Sycamore" iliyoendeshwa na Marekani kumtoa Assad kwa kufadhili na kufundisha makundi ya kigaidi"moderate rebels".Timber Sycamore - Wikipedia

Kilichombakiza Assad madarakani kabla ya kuingia Mrusi ni jeshi la Syria, vikundi vya kikurdi na vikundi vinavyofadhiliwa na Iran.
Hiki unachosema hapa ni covert operations. Mimi sijazungumzia covert operations bali nimezungumzia direct military intervention kama ambavyo swali lilivyokuwa likiuliza. Nazungumzia military intervention kama ile ya NATO nchini Libya. Rejea swali la mchangiaji niliyem-quote awali.

Swali linauliza kwamba, kwanini Marekani na washirika wake walishindwa kuiangusha serikali ya Syria kama walivyofanya Libya?

Kilichofanyika nchini Libya ili kuiangusha serikali ya Libya ni military intervention iliyofanywa na NATO.

Turejee Syria:
Sababu kubwa ya military intervention ya NATO kutofanyika nchini Syria kama ambavyo ilifanyika Libya ni kwa sababu mpango huo haukuungwa mkono kikamilifu miongoni mwa NATO member states kama nilivyosema hapo awali.

Mwaka 2013, Waziri Mkuu wa Uingereza wakati ule, David Cameron alipeleka azimio bungeni ambalo lingeruhusu Uingereza kujiunga pamoja na Marekani katika military action ama intervention nchini Syria dhidi ya Assad baada ya ile issue ya silaha za sumu. Azimio lake lilikataliwa bungeni (House of Commons) baada ya kupigiwa kura. Baada ya hapo, Cameron akasema kuwa atayaheshimu maamuzi ya bunge.

Pitia taarifa hii:

Hiyo issue ya Marekani uliyoisema sio direct military intervention bali ni covert operation. Military intervention ya Marekani ilikuwa ifanyike mapema zaidi, mwaka 2013 kati ya mwezi Agosti na Septemba ukifuatilia ile issue ya "red line" ya Obama. Hata hivyo, Obama hakui-approve hiyo intervention kitu ambacho kilimsababishia ukosoaji mkubwa sana ndani ya Marekani.

Kumbuka hicho ndicho kipindi ambacho azimio la Cameron wa Uingereza lilikataliwa bungeni.

Nchi pekee ambayo inatajwa kuwa ilikuwa mstari wa mbele kuhusiana na suala la kumuondoa Assad ni Ufaransa. Ndiyo nchi iliyopendekeza mara kadhaa direct military intervention nchini Syria dhidi ya Assad lakini ilikosa uungwaji mkono kutoka mataifa mengine ya NATO hasa Marekani na Uingereza.

Pitia taarifa hii:
France's policy towards the war in Syria has been more forward than any other western country. It was early in calling for President Bashar al-Assad to step down, still insists he must go, and recently joined airstrikes inside Syria against the Islamic State - unlike the UK, which has not taken that step.

Kwa kuhitimisha tu, haya yote yalikuwa yakifanyika kabla ya interventions za mataifa mengine kama Urusi. Nafikiri nimeeleweka vyema!
 
Jibu jepesi tu ndugu.tuambie ni silaha gani ambayo Urusi alitumia kwenye ww2, aliyopewa msaada na Mmarekani.mfano tunajua Warusi walikuwa wantumia vifaru vyao ain ya T-34.
Umeisoma hiyo "The Lend-Lease Act" ya mwaka 1941?

Miongoni mwa silaha walizopatiwa ni pamoja na ndege za kivita aina ya Bell P-39 Airacobra, pia walipatiwa vifaru kwa maelfu aina ya Medium Tank M3 almaarufu M3 Lee pamoja na Medium Tank M4 almaarufu M4 Sherman.

Bila kusahau malori ya kijeshi takribani 400,000. Mojawapo ya aina za malori hayo linafahamika kama Studebaker US6. Kampuni iliyounda haya malori ilikwisha fungwa.

Moja ya aina za vifaru vya Mmarekani walivyotumia Wasovieti ama Warusi katika WWII ni hiki hapa chini (M4 Sherman):

1644269022128.png
 
Hapana,unarely kwenye habari zilizopitwa na wakati.

Moja,unakosea unaposema anachofanya uingereza Syria sio direct military intervention labda uje na maana ya hili neno lakini kama serikali inasema bungeni kuwa wanafundisha waasi Syria pamoja na kufanya airstrike (kwenye nchi ambayo hawajaalikwa)hiyo inakuwaje sio direct military intervention?

Uingereza ilianza kutumia waasi pamoja na mashambulizi ya anga miaka ya 2014 baada ya bunge kugoma kupeleka wanajeshi. lakini pia bunge la uingereza kuanzia 2015 limeruhusu mashambulizi mengi ya anga Syria na kama hiyo haitoshi UK special forces(hawahitaji idhini ya bunge) walikuwa chini kupambana na ISIL( kwa mujibu wa taarifa rasmi) pamoja na kumtoa Assad.
picha za magari na wanajeshi wa uingereza Syria.

Mwaka 2016 Marekani pamoja na washirika wake akiwepo Britain waliwashambulia na kuwaua wanajeshi wa syria pamoja na raia.
US: Air strikes killing dozens of Syrian troops legal

Kwa ishu ya Libya mazingira ya kudondoshwa kwa utawala wa Gadaffi hamna utofauti mkubwa na Syria. Marekani pamoja na washirika wake walitumia zaidi waasi kwa ardhini kupambana na Gadafi huku wenyewe wakishambulia kutokea juu. Gadafi hakuwa na msaada wa vikundi vilivyo na uzoefu kupambana na waasi kama ilivyokuwa kwa Assad.

Kwa Marekani, Operation Timber Sycamore ilikuwepo na bado inaendelea. Nitakupa mifano,

Jake Sullivan kwenye moja ya email yake kwenda kwa Hillary Clinton anasema wazi kuwa wametumia zaidi ya dollar milion 500 kwa waasi lakini bado wamefeli kumdondosha Assad (source Wikileaks). Nitakutafutia hiyo email.

Hillary Clinton nae kwenye leaked email yake anasema wazi kabisa wapo pamoja na Al qaeda(wikileaks).Nitakutafutia.

Pia, kumtoa Assad na kusupport waasi haukuwa mpango wa siri hivyo kwa sababu zifuatazo,
1) Marekani iliivamia Syria na kuanza kushambulia ISIL, jeshi la nchi na vikundi vinavyoungwa mkono na Iran. Katika mazingira ya kawaida tu huwezi kwenda nchi ya watu kijeshi bila ruhusa alafu ukawa na lengo tofauti na kuutoa utawala uliopo madarakani. Haya yalitokea kipindi cha Obama.

2) utawala wa Obama uliomba milioni 500 kwenye bunge la Congress kwa ajili ya kusupport waasi. https://www.cnn.com/2014/06/26/politics/syria-us-opposition-funding/index.html
 
Umeisoma hiyo "The Lend-Lease Act" ya mwaka 1941?

Miongoni mwa silaha walizopatiwa ni pamoja na ndege za kivita aina ya Bell P-39 Airacobra, pia walipatiwa vifaru kwa maelfu aina ya Medium Tank M3 almaarufu M3 Lee pamoja na Medium Tank M4 almaarufu M4 Sherman.

Bila kusahau malori ya kijeshi takribani 400,000. Mojawapo ya aina za malori hayo linafahamika kama Studebaker US6. Kampuni iliyounda haya malori ilikwisha fungwa.

Moja ya aina za vifaru vya Mmarekani walivyotumia Wasovieti ama Warusi katika WWII ni hiki hapa chini (M4 Sherman):

View attachment 2111968
Niambie ni vita vya kugombania eneo gani vilitumiwa ivyo vifaa na warusi?.maana warusi walikuwa wanatumia silaha zao wenyewe sasa weka wazi ni wapi zilitumika.
Halafu icho chanzo unaona kabisa ni chnzo cha upande gani.Warusi wenyewe wanasema asilimia 80 ya ushindi wa ww2 umetoka kwao
 
Urusi hupewa mpaka sifa za uongo, ila ushindi katika vita vyote vya dunia, yani WWI na WW2 vilitegemea kwa kiasi kikubwa mchango wa US.
Huyo Marekani alianza hizo vita lini?Kama sio kuvizia watu wameshachoka yeye ndio anakuja kupigana in late 1940's tena baada ya kuona interests zake zinapotea.Mbabe wa wakati huo alikua ni mjerumani pekee yeye ndiye aliyeanzisha vita zote mbili na kuleta machafuko ya dunia.

Macho yangu now yapo kwa kiduku maana siku atakapoibuka kichaa Kama alivyokua Adolf Hitler,WWIII uhakika.
 
akiwa huko cuba na venezuela kwenye shughuli zake nyingi ataendelea kutumia dola ya marekani. urusi ambacho uwa kinamshinda kwa marekani ni nguvu ya kiuchumi na allies wa marekani ambao pia wako vizuri kiuchumi. unaweza kuwa na silaha ila njaa ikakufanya ushindwe vita. wakiminya uchumi wa urusi dakika anayoosha mikono.
Hakuna kitu kama hicho mkuu zile ni black propaganda.Juzi kati Joe baiden alimtishia Urusi kumuekea vikwazo vya kiuchumi kisa kutaka kuivamia Ukraine alafu jana Urusi bado anamipango ya kuivamia Ukraine basi watoe hivyo vikwazo.Kumbuka Urusi ana ushirika na China ambayo inaichallenge Marekani katika Uchumi kwakua China imewekeza vilevile katika Uchumi Katika mataifa mbalimbali.

In short Marekani ataweza kuweka vikwazo kwa nchi kama zimbabwe na nyinginezo in third and second income countries lakini sio kwa Urusi ambaye ni taifa la 3 kwa nguvu in general sectors ambaye ana mshirika China ambaye ni namba 2.

Vita vya Marekani na China vitakua vile vya ukimwaga mboga,ninamwaga ugali.
 
Kupeleka Jeshi nje ya Russia ni gharama kubwa sana
Na sasa nchi zote za Ulaya zinajipanga kususia gesi kutoka Russia.
Putin sio mjinga kupeleka wanajeshi Cuba kuigharimu bila sababu, hizo akili ndio ziliuwa USSR kwa kufanya vitu kiushabiki bila kuwa na mkakati wa kiuchumi.
Uchumi wa Russia kidunia ni sawa na nchi ya Spain,
Kama unazungumzia uchumi wa budget pekee basi zingatia na idadi ya watu pamoja na GOVERNMENT EXPENDITURE on the services of the people.Ila Kama unaongelea uchumi in general term as socially, politically, technologically,millitarlly you are totally wrong.
 
Vita ya nuclear haiitaji silaha nyingi kama risasi,ukiwa na mabomu yako kumi tuu yanatosha kuangamiza Dunia.
Kwa hiyo ndio kusema?

In short Urusi na Marekani wote ni mafahali wawili wasio kaa zizi moja.Is just a matter of timing for someone to destroy the other.
 
Hapana,unarely kwenye habari zilizopitwa na wakati.

Moja,unakosea unaposema anachofanya uingereza Syria sio direct military intervention labda uje na maana ya hili neno lakini kama serikali inasema bungeni kuwa wanafundisha waasi Syria pamoja na kufanya airstrike (kwenye nchi ambayo hawajaalikwa)hiyo inakuwaje sio direct military intervention?

Uingereza ilianza kutumia waasi miaka ya miaka ya 2014 au 2015 baada ya bunge kugoma kupeleka wanajeshi. lakini pia bunge la uingereza kuanzia 2015 limeruhusu mashambulizi mengi ya anga Syria na kama hiyo haitoshi UK special forces(hawahitaji idhini ya bunge) walikuwa chini kupambana na ISIL( kwa mujibu wa taarifa rasmi) pamoja na kumtoa Assad.
picha za magari na wanajeshi wa uingereza Syria.

Mwaka 2016 Marekani pamoja na washirika wake akiwepo Britain waliwashambulia na kuwaua wanajeshi wa syria pamoja na raia.
US: Air strikes killing dozens of Syrian troops legal

Kwa ishu ya Libya mazingira ya kudondoshwa kwa utawala wa Gadaffi hamna utofauti mkubwa na Syria. Marekani pamoja na washirika wake walitumia zaidi waasi kwa ardhini kupambana na Gadafi huku wenyewe wakishambulia kutokea juu. Gadafi hakuwa na msaada wa vikundi vilivyo na uzoefu kupambana na waasi kama ilivyokuwa kwa Assad.

Kwa Marekani, Operation Timber Sycamore ilikuwepo na bado inaendelea. Nitakupa mifano,

Jake Sullivan kwenye moja ya email yake kwenda kwa Hillary Clinton anasema wazi kuwa wametumia zaidi ya dollar milion 500 kwa waasi lakini bado wamefeli kumdondosha Assad (source Wikileaks). Nitakutafutia hiyo email.

Hillary Clinton nae kwenye leaked email yake anasema wazi kabisa wapo pamoja na Al qaeda(wikileaks).Nitakutafutia.

Pia, kumtoa Assad na kusupport waasi haukuwa mpango wa siri hivyo kwa sababu zifuatazo,
1) Marekani iliivamia Syria na kuanza kushambulia ISIL, jeshi la nchi na vikundi vinavyoungwa mkono na Iran. Katika mazingira ya kawaida tu huwezi kwenda nchi ya watu kijeshi bila ruhusa alafu ukawa na lengo tofauti na kuutoa utawala uliopo madarakani. Haya yalitokea kipindi cha Obama.

2) utawala wa Obama uliomba milioni 500 kwenye bunge la Congress kwa ajili ya kusupport waasi. https://www.cnn.com/2014/06/26/politics/syria-us-opposition-funding/index.html

Kwanza kabisa, inaonesha kuwa mgogoro wa Syria umeanza kuufuatilia miaka ya karibuni. Kama habari za mwaka 2013 kuhusu mgogoro huo unasema kuwa ni habari zilizopitwa na wakati, ni dhahiri kwamba mgogoro huo umeufahamu juzijuzi.

Ukitaka kuuzungumzia mgogoro wa Syria kwa ufasaha inakubidi ufuate timeline kuanzia mwanzo wa mgogoro huo. Huwezi kuzungumzia mambo yaliyotokea karibuni kisha ukapuuza yale ya kabla ya hapo na kuyaita kwamba yamepitwa na wakati. Utabaki ukiwa haufahamu mambo mengi.

Jambo la pili: haufahamu kabisa maana ya direct military intervention. Again, umeongelea habari ya Uingereza kuanza kutumia waasi mwaka 2014. Hiyo ndio 'direct military intervention' kwa ufahamu wako? Operation Timber Sycamore ni direct military intervention ya namna gani?

Umeandika kwamba, bunge liligoma kupeleka majeshi. Hilo ni kweli kabisa! Hayo majeshi ndiyo maana halisi ya 'direct military intervention' na ndiyo ambayo yangetakiwa kwenda kufanya intervention mapema kabisa nchini Syria mwaka 2013 endapo bunge lingekubali. Hiyo ni kabla hata ya hizo habari ulizoleta hapa za kutumia waasi. Habari ya bunge kugoma kupeleka majeshi mwaka 2013 imepitwa na wakati kwa kiasi gani?

Je, unafahamu kwamba hilo suala la bunge kukataa kupeleka majeshi mwaka 2013 ndio mara ya kwanza kabisa kwa serikali ya Uingereza kugomewa na bunge kuhusu kufanya maamuzi ya kijeshi? Hilo sio suala dogo na wala sio jambo la kupuuzwa.

Bunge la Uingereza kwa mara ya kwanza liliruhusu mashambulizi ya anga nchini Syria dhidi ya ISIL mwaka 2015 baada ya mjadala wa saa takribani kumi (10) bungeni. Hiyo ni zaidi ya miaka miwili baada ya lile azimio la Cameron la mwaka 2013 kushindikana. Mpaka Uingereza inafikia maamuzi hayo mwaka 2015, tayari mataifa mengine kadhaa yalikuwa yamekwisha fanya interventions zao nchini Syria.

Kabla ya kuzungumzia mambo ya mwaka 2015, 2016 na kuendelea, rudi miaka ya nyuma zaidi, kwa sababu mpango wa intervention wa Uingereza nchini Syria haukuanza mwaka 2015 wala 2016. Mpango wa intervention ulikuwepo, isitoshe, ulikuwa mpango wa wazi kabisa kabla hata ya hiyo miaka uliyoitaja, lakini, mpango huo ulikosa kuungwa mkono kikamilifu kama nilivyosema hapo awali.
 
Niambie ni vita vya kugombania eneo gani vilitumiwa ivyo vifaa na warusi?.maana warusi walikuwa wanatumia silaha zao wenyewe sasa weka wazi ni wapi zilitumika.
Halafu icho chanzo unaona kabisa ni chnzo cha upande gani.Warusi wenyewe wanasema asilimia 80 ya ushindi wa ww2 umetoka kwao
Kwanza, hiyo habari kwamba Warusi walikuwa wakitumia silaha zao wenyewe umeitoa wapi? Kwa taarifa yako, walitumia silaha za mataifa mengi tu. Walitumia silaha za Mmarekani, walitumia silaha za Muingereza, walitumia silaha kutoka Canada n.k. Isipokuwa, idadi kubwa ya misaada ilitoka Marekani. Na sio misaada ya silaha na vyakula tu, ni pamoja na misaada ya kiintelijensia.

Misaada ya silaha ilitumika katika vita ya kuyaondoa majeshi ya Hitler yaliyokuwa yameuteka mji wa Stalingrad, kisha kuelekea Berlin baada ya uvamizi wa Ujerumani wa iliyokuwa Soviet Union uliofanyika mwaka 1941.

Soma historia kuhusiana na Battle of Stalingrad ya mwaka 1942. Mji wa Stalingrad ulikuwa mji muhimu sana wa kiviwanda wa Soviet Union. Hii vita ndio ilimzuia Mjerumani kuingiza majeshi yake ndani zaidi na kuteka maeneo mengi zaidi ya USSR.

Stalin amewahi kunukuliwa publicly akisema kwamba, isingekuwa kwa silaha za Wamarekani, ushirika wetu usingeweza kushinda vita ya pili ya dunia. Sio huyo tu, pia baadhi ya majenerali wa jeshi, watu maarufu na wanahistoria wa Urusi wamewahi kusema hivyo. Miongoni mwao ni aliyekuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Soviet Union, Nikita Khrushchev pamoja na Jenerali Georgy Zhukov aliyeiongoza Red Army ya USSR dhidi ya majeshi ya Hitler. Hiyo asilimia 80 wewe umeitoa wapi?
 
Kwanza kabisa, inaonesha kuwa mgogoro wa Syria umeanza kuufuatilia miaka ya karibuni. Kama habari za mwaka 2013 kuhusu mgogoro huo unasema kuwa ni habari zilizopitwa na wakati, ni dhahiri kwamba mgogoro huo umeufahamu juzijuzi.

Ukitaka kuuzungumzia mgogoro wa Syria kwa ufasaha inakubidi ufuate timeline kuanzia mwanzo wa mgogoro huo. Huwezi kuzungumzia mambo yaliyotokea karibuni kisha ukapuuza yale ya kabla ya hapo na kuyaita kwamba yamepitwa na wakati. Utabaki ukiwa haufahamu mambo mengi.

Jambo la pili: haufahamu kabisa maana ya direct military intervention. Again, umeongelea habari ya Uingereza kuanza kutumia waasi mwaka 2014. Hiyo ndio 'direct military intervention' kwa ufahamu wako? Operation Timber Sycamore ni direct military intervention ya namna gani?

Umeandika kwamba, bunge liligoma kupeleka majeshi. Hilo ni kweli kabisa! Hayo majeshi ndiyo maana halisi ya 'direct military intervention' na ndiyo ambayo yangetakiwa kwenda kufanya intervention mapema kabisa nchini Syria mwaka 2013 endapo bunge lingekubali. Hiyo ni kabla hata ya hizo habari ulizoleta hapa za kutumia waasi. Habari ya bunge kugoma kupeleka majeshi mwaka 2013 imepitwa na wakati kwa kiasi gani?

Je, unafahamu kwamba hilo suala la bunge kukataa kupeleka majeshi mwaka 2013 ndio mara ya kwanza kabisa kwa serikali ya Uingereza kugomewa na bunge kuhusu kufanya maamuzi ya kijeshi? Hilo sio suala dogo na wala sio jambo la kupuuzwa.

Bunge la Uingereza kwa mara ya kwanza liliruhusu mashambulizi ya anga nchini Syria dhidi ya ISIL mwaka 2015 baada ya mjadala wa saa takribani kumi (10) bungeni. Hiyo ni zaidi ya miaka miwili baada ya lile azimio la Cameron la mwaka 2013 kushindikana. Mpaka Uingereza inafikia maamuzi hayo mwaka 2015, tayari mataifa mengine kadhaa yalikuwa yamekwisha fanya interventions zao nchini Syria.

Kabla ya kuzungumzia mambo ya mwaka 2015, 2016 na kuendelea, rudi miaka ya nyuma zaidi, kwa sababu mpango wa intervention wa Uingereza nchini Syria haukuanza mwaka 2015 wala 2016. Mpango wa intervention ulikuwepo, isitoshe, ulikuwa mpango wa wazi kabisa kabla hata ya hiyo miaka uliyoitaja, lakini, mpango huo ulikosa kuungwa mkono kikamilifu kama nilivyosema hapo awali.
Kwenye maelezo yako ya awali umesema kwamba sababu za kutokuwepo kwa direct military intervention syria ni mabunge kadhaa ya ulaya kugomea uvamizi ukatoa mfano wa bunge la uingereza na kura ya kupinga. Mwisho wa maelezo yako umesema wazi kuwa mgomo huo ulikuwa kabla ya kuingia majeshi ya nje ya NATO kama Urusi. Kipi sijaelewa hapa?

Nimekujibu kwa kutambua na kuikubali taarifa uliyoileta lakini imepitwa na wakati kwa kuwa mwaka 2014 na 2015 kabla ya kuingia majeshi ya Urusi tayari Uingereza ilikuwa imeshaanza kupiga mabomu Syria na kutrain waasi. Pia haya yametokea kabla ya bunge kuidhinisha mashambulizi ya anga, Waziri mkuu alikuwa anatoa taarifa za shughuli za majeshi ya Uingereza huko Syria.

Na Marekani pia nimekujibu tangu 2014 wanapiga mabomu Syria. Majeshi ya Urusi yalikuwa hayajafika kipindi hiki.

Nimekataa ulivyosema huu uvamizi wa Uingereza siyo direct military intervention na nimekupa sababu kuwa jeshi la Uingereza bila kujificha limelipua maeneo mbalimbali Syria na kufund waasi.Haya yote yalikuwa yanatolewa taarifa na waziri mkuu kwa general public.

Nimeona umetumia muda mwingi kukataa na kunipinga kwamba ilichofanya Uingereza siyo direct military intervention lakini mimi nimetoa sababu na nikakwambambia utoe hiyo maana ya direct military intervention na ilianza lini? Hujatoa hiyo definition hadi sasa lakini unakomaa kukataa nilichokueleza.
 
Kwenye maelezo yako ya awali umesema kwamba sababu za kutokuwepo kwa direct military intervention syria ni mabunge kadhaa ya ulaya kugomea uvamizi ukatoa mfano wa bunge la uingereza na kura ya kupinga. Mwisho wa maelezo yako umesema wazi kuwa mgomo huo ulikuwa kabla ya kuingia majeshi ya nje ya NATO kama Urusi. Kipi sijaelewa hapa?

Nimekujibu kwa kutambua na kuikubali taarifa uliyoileta lakini imepitwa na wakati kwa kuwa mwaka 2014 na 2015 kabla ya kuingia majeshi ya Urusi tayari Uingereza ilikuwa imeshaanza kupiga mabomu Syria na kutrain waasi. Haya yametokea kabla ya bunge kuidhinisha mashambulizi ya anga, Waziri mkuu alikuwa anatoa taarifa za shughuli za majeshi ya Uingereza huko Syria.

Na Marekani pia nimekujibu tangu 2014 wanapiga mabomu Syria. Majeshi ya Urusi yalikuwa hayajafika kipindi hiki.

Nimekataa ulivyosema huu uvamizi wa Uingereza siyo direct military intervention na nimekupa sababu kuwa jeshi la Uingereza bila kujificha limelipua maeneo mbalimbali Syria na kufund waasi.Haya yote yalikuwa yanatolewa taarifa na waziri mkuu kwa general public.

Nimeona umetumia muda mwingi kukataa na kunipinga kwamba ilichofanya Uingereza siyo direct military intervention lakini mimi nimetoa sababu na nikakwambambia utoe hiyo maana ya direct military intervention na ilianza lini? Hujatoa hiyo definition hadi sasa lakini unakomaa kukataa nilichokueleza.
Hapo awali ulisema: "Hapana, unarely kwenye habari zilizopitwa na wakati". Sidhani kama hii ni statement ya kutambua na kukubaliana na taarifa niliyoileta kama alivyosema sasa. Definitely, hiyo ni statement ya kutokukubaliana na kile nilichosema ndio maana nimeijibu kwa namna niliyojibu.

Nilisema na inafahamika kuwa Uingereza ilianza mashambulizi nchini Syria kwa idhini ya bunge Disemba mwaka 2015. Hiyo ndiyo 'direct military intervention' ya kwanza kabisa ya Uingereza nchini Syria dhidi ya ISIL. Kabla ya hapo, Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa akipeleka mapendekezo ya intervention bungeni na hakuwahi kufanikiwa.

Mpaka mwezi Septemba mwaka 2014, Waingereza walikuwa wakijadili uwezekano wa Uingereza kufanya military intervention nchini Syria katika siku zijazo. Pitia taarifa hii ya Septemba 26, 2014 hapa chini:

Chochote kinachohusiana na masuala ya kijeshi ambacho kiliwahi kufanyika Syria kabla ya hapo hakikuwa 'direct military intervention' bali zilikuwa ni 'covert operations'. Hata hayo mafunzo ni covert operations pia. Ushahidi wa hili ni katika ile taarifa uliyoleta awali iliyo na statement ya yule waziri wa zamani.

Kuna taarifa kadhaa haziko wazi kuhusiana na kauli hiyo. Kuna mahali panasema hivi: "For security reasons, we do not disclose the names of those moderate opposition groups supported". Mpaka hapo tayari hiyo ilikuwa ni covert operation sababu hata hayo makundi yaliyosapotiwa ni classified. Hayafahamiki wazi.

Point ya msingi ni kuwa, mpango wa military intervention ya kimataifa hususani NATO nchini Syria ulikuwepo kwa muda kabla ya interventions za nchi zingine kama Urusi, lakini, mpango huo ulikosa kuungwa mkono kikamilifu na nchi kadhaa zenye ushawishi mkubwa katika jumuiya hiyo.
 
Kwa kipekee kabisa, hii ni miongoni mwa definitions za neno 'intervention'.

Intervention, in terms of international law, is the term for the use of force by one country or sovereign state in the internal or external affairs of another. In most cases, intervention is considered to be an unlawful act but some interventions may be considered lawful.

Source: Wikipedia
 
Hapo awali ulisema: "Hapana, unarely kwenye habari zilizopitwa na wakati". Sidhani kama hii ni statement ya kutambua na kukubaliana na taarifa niliyoileta kama alivyosema sasa. Definitely, hiyo ni statement ya kutokukubaliana na kile nilichosema ndio maana nimeijibu kwa namna niliyojibu.

Nilisema na inafahamika kuwa Uingereza ilianza mashambulizi nchini Syria kwa idhini ya bunge Disemba mwaka 2015. Hiyo ndiyo 'direct military intervention' ya kwanza kabisa ya Uingereza nchini Syria dhidi ya ISIL. Kabla ya hapo, Waziri Mkuu wa Uingereza alikuwa akipeleka mapendekezo ya intervention bungeni na hakuwahi kufanikiwa.

Mpaka mwezi Septemba mwaka 2014, Waingereza walikuwa wakijadili uwezekano wa Uingereza kufanya military intervention nchini Syria katika siku zijazo. Pitia taarifa hii ya Septemba 26, 2014 hapa chini:

Chochote kinachohusiana na masuala ya kijeshi ambacho kiliwahi kufanyika Syria kabla ya hapo hakikuwa 'direct military intervention' bali zilikuwa ni 'covert operations'. Hata hayo mafunzo ni covert operations pia. Ushahidi wa hili ni katika ile taarifa uliyoleta awali iliyo na statement ya yule waziri wa zamani.

Kuna taarifa kadhaa haziko wazi kuhusiana na kauli hiyo. Kuna mahali panasema hivi: "For security reasons, we do not disclose the names of those moderate opposition groups supported". Mpaka hapo tayari hiyo ilikuwa ni covert operation sababu hata hayo makundi yaliyosapotiwa ni classified. Hayafahamiki wazi.

Point ya msingi ni kuwa, mpango wa military intervention ya kimataifa hususani NATO nchini Syria ulikuwepo kwa muda kabla ya interventions za nchi zingine kama Urusi, lakini, mpango huo ulikosa kuungwa mkono kikamilifu na nchi kadhaa zenye ushawishi mkubwa katika jumuiya hiyo.
Mbona hata hiyo post ya pili nimekwambia hiyo taarifa imepitwa na wakati pamoja na kuitambua.

Lengo la kukwambia hiyo habari imepitwa na wakati ni kwamba, baada ya bunge kugoma kuidhinisha jeshi kuvamia Syria tulitegemea jeshi la Uingereza lisionekane Syria kwa operation yoyote hadi hapo 2015 baada ya bunge kuidhinisha mashambulizi ya anga lakini hali haikuwa hivyo.

covert operation kwa tafsiri ya kawaida tu ni operation za siri. Sasa kuna usiri gani wakati jeshi la anga la Uingereza lilipokuwa linawapiga mabomu ISIL na makundi mengine kabla ya bunge kuruhusu na wakati huohuo serikali kutoa taarifa za mashambulizi hayo. Kilichobadilika baada ya bunge kuruhusu ni jeshi kuongeza mashambulizi ya anga na kutohitaji kujitetea baada ya mashambulizi hayo.

Hata ukija kwa hao moderate rebels, usiri pekee ni serikali kutotoa majina ya hayo makundi lakini kila kitu kipo wazi kwa general public kwamba serikali inafadhili magaidi kumuondoa Assad. Hata tukiambiwa hayo majina na serikali inaongeza nini?

Pili, Moderate rebels waliopo Syria wanajulikana sababu ndio haohao wanaotumika na Marekani na Israel. sijaona hiyo taarifa kama ina usiri huo hadi kuiita hiyo ni covert operation.

Kwa maana hiyo ya intervention uliyoileta, majeshi ya uingereza yana uhalali gani kwa yanayotokea Syria?
 
Naomba unitajie operation moja tu ya wazi ya jeshi la anga la Uingereza dhidi ya ISIL na mahali ilipofanyika ndani ya Syria kabla ya approval ya bunge Disemba mwaka 2015. Sihitaji Operation Shader ya Iraq, nahitaji ya Syria. Moja tu iliyofanyika kabla ya approval ya bunge mwaka 2015.

Maana umedai hapa kuwa hakukuwa na usiri katika hizo missions. Hivyo basi, naomba unitajie moja tu!
 
Asante sana!

Hii sio operation ya wazi kama ambavyo nimeomba unipatie, bali ni mfano mzuri sana wa covert operations nilizozisema hapo awali.

Katika hiyo taarifa, kuna kauli ya Waziri Mkuu inasema hivi: "The strike had been approved at a meeting of "the most senior members" of the National Security Council, and authorised by Defence Secretary Michael Fallon".

Umeuona huo usiri hapo? Operation imeamuliwa katika kikao cha siri cha baraza la usalama, taarifa imekuja kutolewa baada ya operation kufanyika. Hakukuwa na uwazi wowote ule wakati hiyo operation inaanza ama wakati inafanyika. Hiyo ndio maana halisi ya covert operation.

Ukienda chini zaidi katika hiyo taarifa ya BBC, kuna upinzani mkubwa tu juu ya hilo shambulizi lililofanywa. Hasa katika hicho kipengele kinachoanza na maneno "Secret strikes". Nadhani umepaona hapo!
 
Kwanza, hiyo habari kwamba Warusi walikuwa wakitumia silaha zao wenyewe umeitoa wapi? Kwa taarifa yako, walitumia silaha za mataifa mengi tu. Walitumia silaha za Mmarekani, walitumia silaha za Muingereza, walitumia silaha kutoka Canada n.k. Isipokuwa, idadi kubwa ya misaada ilitoka Marekani. Na sio misaada ya silaha na vyakula tu, ni pamoja na misaada ya kiintelijensia.

Misaada ya silaha ilitumika katika vita ya kuyaondoa majeshi ya Hitler yaliyokuwa yameuteka mji wa Stalingrad, kisha kuelekea Berlin baada ya uvamizi wa Ujerumani wa iliyokuwa Soviet Union uliofanyika mwaka 1941.

Soma historia kuhusiana na Battle of Stalingrad ya mwaka 1942. Mji wa Stalingrad ulikuwa mji muhimu sana wa kiviwanda wa Soviet Union. Hii vita ndio ilimzuia Mjerumani kuingiza majeshi yake ndani zaidi na kuteka maeneo mengi zaidi ya USSR.

Stalin amewahi kunukuliwa publicly akisema kwamba, isingekuwa kwa silaha za Wamarekani, ushirika wetu usingeweza kushinda vita ya pili ya dunia. Sio huyo tu, pia baadhi ya majenerali wa jeshi, watu maarufu na wanahistoria wa Urusi wamewahi kusema hivyo. Miongoni mwao ni aliyekuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Soviet Union, Nikita Khrushchev pamoja na Jenerali Georgy Zhukov aliyeiongoza Red Army ya USSR dhidi ya majeshi ya Hitler. Hiyo asilimia 80 wewe umeitoa wapi?
Lete source ya taarifa yako kuhusu hayo maneno ya stalin
 
Back
Top Bottom