FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Hiki unachosema hapa ni covert operations. Mimi sijazungumzia covert operations bali nimezungumzia direct military intervention kama ambavyo swali lilivyokuwa likiuliza. Nazungumzia military intervention kama ile ya NATO nchini Libya. Rejea swali la mchangiaji niliyem-quote awali.Nchi zote za NATO ziliunga na zinaunga mkono mipango ya kumtoa Assad madarakani, wanachotofautiana ni level of commitment baina ya nchi moja na nyingine kuhakikisha huo mpango unafanikiwa.
Nchi zilizokuwa mstari wa mbele kuhakikisha Assad anatoka ni Marekani, Britain, France, Turkey na Israel wakisaidiwa na Saudi Arabia, UAE na Qatar.
Kwa case ya Britain, serikali yao ilisema bungeni kuwa inafadhili na kufundisha vikundi vya kigaidi wenyewe wanaviita "moderate rebels" kwa ajili ya kupamba na ISIL na kuitoa serikali madarakani( kimsingi ndio lengo kuu).
https://questions-statements.parliament.uk/written-questions/detail/2018-04-13/135396
hili ni jibu la waziri bungeni. Pia kuna Case mshtumiwa wa ugaidi ilibidi waendesha mashtaka wa Uingereza waifute kwa kuwa mshutumiwa huyo wa Ugaidi alikuwa sehemu ya vikundi vinavyofadhiliwa na serikali ya Uingereza kumtoa Assad.
Nchi zote nilizotaja hapo juu zinafadhili hivi vikundi kwa ajili ya kumtoa Assad.
Pia unaweza kupitia hii "Operation Timber Sycamore" iliyoendeshwa na Marekani kumtoa Assad kwa kufadhili na kufundisha makundi ya kigaidi"moderate rebels".Timber Sycamore - Wikipedia
Kilichombakiza Assad madarakani kabla ya kuingia Mrusi ni jeshi la Syria, vikundi vya kikurdi na vikundi vinavyofadhiliwa na Iran.
Swali linauliza kwamba, kwanini Marekani na washirika wake walishindwa kuiangusha serikali ya Syria kama walivyofanya Libya?
Kilichofanyika nchini Libya ili kuiangusha serikali ya Libya ni military intervention iliyofanywa na NATO.
Turejee Syria:
Sababu kubwa ya military intervention ya NATO kutofanyika nchini Syria kama ambavyo ilifanyika Libya ni kwa sababu mpango huo haukuungwa mkono kikamilifu miongoni mwa NATO member states kama nilivyosema hapo awali.
Mwaka 2013, Waziri Mkuu wa Uingereza wakati ule, David Cameron alipeleka azimio bungeni ambalo lingeruhusu Uingereza kujiunga pamoja na Marekani katika military action ama intervention nchini Syria dhidi ya Assad baada ya ile issue ya silaha za sumu. Azimio lake lilikataliwa bungeni (House of Commons) baada ya kupigiwa kura. Baada ya hapo, Cameron akasema kuwa atayaheshimu maamuzi ya bunge.
Pitia taarifa hii:
Syria crisis: Cameron loses Commons vote on Syria action
MPs vote against possible military action against Syria, ruling out involvement in US-led attacks, while France says the vote does not change its resolve to act.
www.bbc.com
Hiyo issue ya Marekani uliyoisema sio direct military intervention bali ni covert operation. Military intervention ya Marekani ilikuwa ifanyike mapema zaidi, mwaka 2013 kati ya mwezi Agosti na Septemba ukifuatilia ile issue ya "red line" ya Obama. Hata hivyo, Obama hakui-approve hiyo intervention kitu ambacho kilimsababishia ukosoaji mkubwa sana ndani ya Marekani.
Kumbuka hicho ndicho kipindi ambacho azimio la Cameron wa Uingereza lilikataliwa bungeni.
Nchi pekee ambayo inatajwa kuwa ilikuwa mstari wa mbele kuhusiana na suala la kumuondoa Assad ni Ufaransa. Ndiyo nchi iliyopendekeza mara kadhaa direct military intervention nchini Syria dhidi ya Assad lakini ilikosa uungwaji mkono kutoka mataifa mengine ya NATO hasa Marekani na Uingereza.
Pitia taarifa hii:
France's policy towards the war in Syria has been more forward than any other western country. It was early in calling for President Bashar al-Assad to step down, still insists he must go, and recently joined airstrikes inside Syria against the Islamic State - unlike the UK, which has not taken that step.
France more active than rest of the west in tackling Syria
France has been dogged in its approach toward Assad and Isis, with Islamist group referring in Paris attacks claim to airstrikes by French fighter jets
Kwa kuhitimisha tu, haya yote yalikuwa yakifanyika kabla ya interventions za mataifa mengine kama Urusi. Nafikiri nimeeleweka vyema!