kt the irreplaceable
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 2,375
- 4,893
Tupe ukweli jasus.... basi ule ulikua uasi wa kidigital..UONGO
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupe ukweli jasus.... basi ule ulikua uasi wa kidigital..UONGO
UONGO, uchambuzi uchwara.Hajapelekwa uhamishoni
Ni vikosi vimehamishwa kijanja kuwekwa Belarus kwa ajili ya kujiandaa kuivamia Kiev kiurahisi[emoji4]
Ukweli ni ule uliouna na kuusikia na ulioonwa live na kila mtu, hakuna haja ya kupewa.Tupe ukweli jasus.... basi ule ulikua uasi wa kidigital..
Siyo kuungana naye tu, hata tako mpe tu.Mimi mwenyewe naungana na putin ardhi ya warusi lazima ilindwe kwa nguvu zote.
Namaanisha mashabiki sio ukraine halisi.Wapi uliwaona Ukraine wakishangalia??
Kuna tatizo gani ukishangilia adui yako wanapovurugana??
NATO hapo inahusikaje?. Vita ni kati ya Ukraine na Urusi. Pia lazima ujue vita ni mipango. Huwezi kumuingia moja kwa moja mpinzani wako ksbb tu umemuona ameishiwa nyimbo,amebaki na ngonjera. Lazima umuingie kwa hesabu.Vichekesho hivi, sasa NATO na Ukraine wanashindwa nini kuwamaliza hao waliishiwa morali?
Kwani mkuu duniani ni putin peke yake ndio ana mabomu ya nyukilia? Hao wengine vipi?NATO hapo inahusikaje?. Vita ni kati ya Ukraine na Urusi. Pia lazima ujue vita ni mipango. Huwezi kumuingia moja kwa moja mpinzani wako ksbb tu umemuona ameishiwa nyimbo,amebaki...
Hahaha umeishiwa hoja umeanza matusiSiyo kuungana naye tu, hata tako mpe tu.
Hakuna aibu, uasi hautaishia hapo. Putin ameonyesha udhaifu.Utaaibika soon.....
Dunia nzima adhabu ya uhaini ni kifo tu.Hakuna aibu, uasi hautaishia hapo. Putin ameonyesha udhaifu.
Mtu amefanya uasi unatangaza asubuhi kwa dunia, jioni serikali yako inatangaza msamaha kwa waasi.
Na bado hauno tatizo
Samahani mkaka,nakuomba pm.Sema mzee wa Ebeltoft😁😁
Una tabia mbaya sana pm siji na nimeifungaSamahani mkaka,nakuomba pm.
Na uliabika, tulioelewa kuwa ile ni sinema ni tulikaa kimya.Hakuna aibu, uasi hautaishia hapo. Putin ameonyesha udhaifu.
Mtu amefanya uasi unatangaza asubuhi kwa dunia, jioni serikali yako inatangaza msamaha kwa waasi.
Na bado hauno tatizo
Prighozin did a very big mistake...Wapiganaji wa Wagner waelekea Moscow kuuondoa utawala wa kijeshi unaoongozwa na SERGEI SHOIGRU. Kiongozi wa Wagner anadai kwamba majeshi ya urusi yamekuwa yakishambulia kambi zao nchini UKRAINE.
Huu Uzi nitatoa update ya kila kinachoendelea.
=====
Update: Maafisa wa Ukraine wasema watatumia 'mapinduzi ya kijeshi' nchini Urusi kurejesha eneo lililochukuliwa
Katika tishio moja kwa moja kwa mamlaka ya Putin, Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa Wagner, aliishutumu jeshi la Moscow kwa kupiga bomu askari wake na kudhibiti jiji muhimu la Urusi mapema asubuhi.
Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali wa jeshi binafsi maarufu zaidi ulimwenguni aliahidi kwenda kwenye mji mkuu kwa kulipiza kisasi.
Katika hotuba isiyokuwa ya kawaida, Bwana Putin alilitaja tukio hilo kuwa "uhaini" na akasema wale wanaounga mkono vitisho na njia za kigaidi watapata adhabu isiyoweza kuepukika.
Rais wa Ukraine, Zelensky, alivunja ukimya na kusema kuwa hii ni mfano mwingine wa "udhaifu kamili wa Urusi".
=====
Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi waagiza watu kubaki nyumbani
Mamlaka katika eneo la Lipetsk nchini Urusi walitoa wito kwa watu kubaki ndani ya nyumba zao kwa sababu za usalama.
Walitoa onyo hilo kutokana na ripoti kuwa wapiganaji wa Wagner walikuwa wakitumia eneo hilo wakati wa safari yao kuelekea Moscow.
=====
Wagner wateka makao makuu ya jeshi la Urusi ukanda wa Kusini
Gavana wa Voronezh, nchini Urusi alisema Jumamosi kuwa huduma za dharura zilikuwa zikijaribu kuzima tanki la mafuta linalowaka katika kituo cha mafuta.
Zaidi ya askari zimamoto 100 na vifaa 30 vya kuzimia moto walikuwa wakifanyia kazi katika eneo hilo, alisema Gavana Alexander Gusev kupitia Telegram.
Awali Jumamosi, chanzo cha usalama nchini Urusi kiliiambia Reuters kuwa wapiganaji wa Wagner walidhibiti vituo vya kijeshi katika jiji la Voronezh, umbali wa kilomita 500 (maili 310) kusini mwa Moscow. Reuters hawakuweza kuthibitisha madai hayo.
=====
NDEGE YA RAIS YADAIWA KUONDOKA MOSCOW, WAGNER WAKIDAIWA KUKARIBIA MJI
Inadaiwa Wapiganaji wa Wagner wameendelea na mapambano na sasa wamefika katika Mkoa wa #Lipetsk, takriban Kilometa 450 kutoka Moscow
Aidha, inaelezwa kuwa Ndege za Kivita za Urusi zimeshambulia misafara ya Wapiganaji wa #Wagner na tayari Wanajeshi wameshajipanga katika nafasi za kuulinda Mji Mkuu, Moscow
Kiongozi wa Wagner, Yevgeny #Prigozhin amedai kuwa Wapiganaji wake wamepokelewa kama 'Wakombozi' na kuwa waliweza kuchukua Makao Makuu ya Kijeshi huko #Rostov bila mapigano
Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Ndege ya Rais imeonekana kuondoka #Moscow, hata hivyo Ikulu imedai kuwa Rais #Putin bado yupo katika Mji Mkuu huo
Wagner wasitisha kwenda Moscow wakidai hawawezi kumwaga damu ya Warusi
Kiongozi wa kundi la Wagner amesema kwenye chanel yake ya Telegram kwamba wamekubaliana kuacha kupeleka vikosi vyake Moscow.
Prigozhin amesema wapiganaji wanarejea kwenye kambi za Ukraine na hawataki kumwaga damu za warusi.
Makubaliano ya ghafla ya kuondoa hali ya sintofahamu yanakuja baada ya kiongozi wa Beralus, Alexander Lukashenko kufanya maongezi na Prigozhin kulingana na channel ya Kirusi ya Rossiya 24